Hotuba aliyoitoa Prof. Mark Mwandosya (MNEC) kwenye Kikao cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM huko Mugumu, Wilaya ya Serengeti
Ndugu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Sengereti,
Ndugu Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Serengeti
na Katibu Mwenezi wa Sekretariati ya CCM Wilaya,
Ndugu Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya
CCM Wilaya ya Serengeti,
Meshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Sengereti,
Waheshimiwa Madiwani,
Mabibi na Mabwana,
Nianze kwa kufanya jambo la kistaarabu, nalo ni kuwashukuru, kwa dhati kabisa kwa kukubali kuja kuonana na mimi pamoja na kwamba taarifa ya mkutano huu nimeipata muda mfupi uliopita. Nikisema nipo Mugumu kwa ziara ya Kichama wote mtatikisa kichwa, ishara ya kutokubaliana na mimi. Katibu na Mwenyekiti wanawaza 'mbona hatujapata taarifa kutoka kwa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mara kuhusu ujio wako?’

Najenga hoja ya kuja kwangu kiChama kama ifuatavyo: - Chama cha Mapinduzi kina 'Mkataba wa hiari' na wananchi wa Tanzania. Mkataba huo 'uliposainiwa' ulikipa Chama cha Mapinduzi ridhaa ya kuunda Serikali ya Awamu ya Nne. Mkataba huo umo katika kijitabu kidogo chenye rangi ya kijani na manjano kiitwacho Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2005. Nimekuja kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama, hivyo basi nimekuja kufanya kazi ya Chama kupitia serikali yake.
Kwa kuwa muda umetupita kando nitazungumza nanyi kwa kupitia, kwa haraka mambo matano yafuatayo:-
Mosi,tumshukuru Muumba wetu, Mwenyezi Mungu kwa kutuvusha kutoka mwaka 2009 kuingia 2010. Tumshukuru kwa kuwa sisi tuliovuka, hatujafanya maajabu makubwa ya kutuwezesha kupewa bahati hiyo. Hakika hatujawazidi wale waliotutangulia. Wengine wameitwa mbele za haki siku ya mwisho wa mwaka 2009. Mmoja wao ni Mzee wetu, Mwasisi wa Taifa hili, Simba wa Vita, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Mwenyezi Mungu ailaze roho yake, na wote waliotutangulia mahala pema peponi, Amina.

Hata bila ya kuwa waumini sana, nadhani Mwenyezi Mungu ameturuhusu tuvuke kuingia 2010 ili tuendelee kuwatumikia wananchi, wana Serengeti, na wananchi wa Tanzania. Pamoja na yote haya niliyosema, nawapa hongera na nawatakia heri na fanaka za mwaka mpya, 2010.
Pili,nawapongeza kwa ushindi mkubwa mlioupata katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Novemba mwaka 2009. Pamoja na kutotamka asimilia ya ushindi, naamini ulikuwa kati ya asilimia 90 na 97 au juu zaidi. Kibinadamu huu ni ushindi wa kusherehekea.
Lakini mimi naona vinginevyo. Naona kama vile Chama kimepewa mzigo mzito. Wananchi wanapokupa imani kubwa namna hiyo, inatetemesha. Wana matarajio makubwa na Chama chetu. Hivyo basi wakati huu, badala ya kusheherehekea, ni wakati wa kutafakari ili tujibu swali muhimu 'tutawafanyia nini wananchi wa Tanzania kuwarudishia Imani waliyotupa! Hoja ninayojenga hapa ni kwamba tuwe wanyenyekevu katika ushindi mkubwa na tutafakari tutaweza vipi kutimiza matarajio ya wananchi.
Tatu,linalofanana na suala la pili linahusu uchaguzi. Mwaka 2010 ni mwaka wa uchaguzi mkuu. Uchaguzi unaweza ukawa wa balaa unaweza ukawa wenye baraka, unaweza ukaleta balaa lakini uchaguzi unaweza ukaleta neema na baraka tele. Mifano ni wingi. Tubakie hukuhuku kwetu Afrika ya Mashariki. Tujiulize ni nini kinachofanya uchaguzi Kenya kila mara uwe ni balaa, na kwetu uwe wa amani na baraka?

Watu ni wale wale. Hakuna kitu cha kiasilia au kibinadamu kinachotufanya sisi tuwe tofauti na wao. Hebu fikiria, Je kuna tofauti yoyote kati ya mjaluo wa Kisumu na yule wa Rorya? Je kuna tofauti yoyote kati ya Mkurya wa Tarime na Mkurya wa Kuria Kenya? Nauliza kuna tofauti yoyote kati ya Mmasai wa Loliondo na yule wa Narok au yule wa Longido na yule wa Kijiado? Na mdigo je? Yule wa Mkinga na yule wa Kwale, wana tofauti yoyote? Lahasha.
Sisi sote ni watu walewale, tuliotengwa na mipaka ya utawala iliyowekwa na wakoloni. Hatupishani mila wala desturi, utamaduni wala lugha. Lamsingi hakuna lile la kiasilia, iwe ni 'gene' au vinasaba kinachotutenganisha sisi na wao. Pamoja na hayo uchaguzi Kenya mara nyingi huwa balaa na Tanzania huwa ni neema.
Hoja ninayotaka kujenga ni kwamba kama kwa asili yetu, kiutamaduni, na kihistoria sisi ni walewale, maana yake linalowezekana Kenya linaweza kutokea Tanzania. Vile vile linalotokea Tanzania linaweza kutokea Kenya. Hivyo basi kwa kuwa uchaguzi kwetu siku zote umekuwa wa amani, tuna wajibu wa kuenzi ile misingi na sababu zinazotufanya tufanikiwe: umoja, mshikamano, upendo, amani na uzalendo.

Tuna wajibu wa kutunza 'zawadi' hizi kama tunavyotunza mboni za macho yetu. Kwa kutumia mfano mwingine tutunze hizi 'zawadi' kama vile tunavyotunza mayai ambayo mimi na wengi wetu tunavyotendewa tukienda vijijini. Akina mama hutupa zawadi ya mayai mawili au matatu. Ili kuyatunza huwa tunayaweka kwenye bakuli dogo lililo na maharage au mchele. Bila kufanya hivyo, katika safari, mayai hugongana na hupasuka.
Suala la nne lina uhusiano mkubwa na nililolizungumza na linahusu pia uchaguzi. Uchaguzi wowote ule una gharama. Chama kinagharimia vipi uchaguzi ni changamoto inayovikumba vyama vyote duniani. Wanasiasa mashuhuri duniani wameanguka kutokana na kutokuwa makini katika suala hili. Vyama vingi duniani vimeingia matatani na kupoteza umaarufu kutokana na kukiuka katiba na sheria, kanuni na taratibu hasa katika masuala ya matumizi ya fedha wakati wa uchaguzi. Lakini nani alipie gharama za uchaguzi? Nionavyo mimi huu ni wajibu muhimu wa mwanachama.

Kwa kuwa tunaingia Chama kwa hiari, kutokana na kuikubali Katiba, kukubali Kanuni zake na Imani yake, wanachama tuna wajibu wa kuchangia kukifanya Chama kiwe hai. Uchaguzi unahuisha Chama na kukifanya Chama na wanachama kuwa hai.
Wahenga wanasema ‘asilia haipendi ombwe’ (vaccum), au ‘utupu’. Chama kikiwa na ombwe linalotokana na kukosa uwezo wa kugharamia uchaguzi, ombwe hilo hakika litajazwa. Linajazwa na nani? Hapo ndipo waingiapo wachache, wenye uwezo mkubwa wa kifedha, matajiri na kawaida wafanyabiashara, wawe wamepata fedha zao halali au haramu.

Tatizo linajitokeza pale wengi wao, si wote, na nasisitiza wengi wao, wanapojaza hili ombwe kwa matarajio yaliyo tofauti na yale ya Chama na wanachama. Wengi, na ni kibinadamu, wanategemea kwa kuwa wamekichangia Chama basi Chama kinaweza kuwalinda. Wengine wana matarajio ya kujiongezea sifa ili biashara zikue. Wanafanya hivyo ama kwa kugombea nafasi za uongozi ili waingie katika ulingo wa siasa au wawe na ushawishi juu ya nani awe kiongozi, Baya zaidi ni pale wanapotaka kumwongoza kiongozi! Ni mara chache sana kupata wachangiaji ambao ni mfano wa ‘Msalaba Mwekundu’ au ‘Nusu Mwezi Mwekundu’. Lakini wapo wachache ambao hutoa kwa moyo na kwa upendo kwa Chama chao. Tufanye nini? Hili ndio swali.
Kwa kuwa wanachama ni wengi, ni vema katika kuchangia gharama za kuendesha Chama ikiwa ni pamoja na uchaguzi, kiwango kikawekwa cha chini, kile ambacho mwanachama wa kawaida anaweza kukimudu. Na iwe kwa kila mwanachama bila kujali uwezo ili kutoa nafasi kwa wanachama wa kawaida ambao ni wengi, kujiona wanahusika na Chama chao.

Viwango vikubwa vinavyotolewa na wachache vinaua ari ya wanachama wa kawaida kuchangia. Kwa mtindo huu wa wachache kuchangia kiwango kikubwa, pamoja na tahadhari nilizozitaja kuna athari ya Chama kuwa na matabaka mawili, sisi wenye fedha, na wao walio wengi. Nionavyo mimi, na Mwenyezi Mungu apishe mbali, kuna siku wao watasema ‘tunawaachieni Chama chenu’, au watasema tunaondoka na Chama chetu’.
Hoja ninayojenga hapo ni kwamba tuwahusishe wanachama wa kawaida, kwa michango ya viwango vya kawaida, ili wajione wao ni Chama. Tutabakia tumeshika pakacha lililojaa fedha. Nawasihi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Serengeti, muanzishe mfuko wa uchaguzi na mfungue akaunti maalum ya mfuko huo katika benki, kama bado hamjafanya hivyo. Kiwango cha kuchangia kiwe kidogo au cha wastani. Kwa kuwa mko wengi, mtashangaa uwezo mkubwa mlio nao.
Tuepukane vilevile na vitendo ambavyo vinakifedhehesha Chama chetu kila unapofika wakati wa uchaguzi. Vichwa vya habari tena kwa maandishi makubwa vinahusu rushwa au rafu. Tunaishia kuvilaumu vyombo vya habari (mjumbe) badala ya kushughulikia ujumbe. Historia inaonesha vyama vyetu vikubwa vina uwezo mkubwa wa kujimaliza vyenyewe. Imetokea mahali pengi duniani, na karibu na nyumbani Kenya (KANU), Zambia (UNIP), Uganda (UPC) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MPR), na Malawi (MCP).
La mwisho, la tano, ambalo ni la hitimisho linahusu pia uchaguzi. Nimefuatilia kwa makini uchaguzi mkuu wa majirani zetu Msumbiji. Tunakuwa na shauku na uchaguzi Msumbiji kutokana na historia yake ya mapambano dhidi ya ukoloni wa Mreno, na mapigano RENAMO dhidi ya wananchi wa Msumbiji. Katika ujumbe wake kwa wananchi wa Msumbiji Rais Armando Guebuza aliwaasa wana Msumbiji wauchukulie uchaguzi mkuu kama sherehe. Namalizia kwa kuwaomba wana Serengeti na wana CCM Serengeti muuchukulie Uchaguzi Mkuu wa 2010 kama ni sherehe ya mshikamano, undugu, upendo na amani. Na katika hili tuzidi kuombeana baraka za Mwenyezi Mungu.
Namalizia kama nilivyoanza kwa kuwashukuru na kuwatakia heri na fanaka kwa mwaka wa 2010.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

"Profesa Mwandosya Amwaga Cheche Serengeti"
ReplyDeleteSasa cheche ziko wapi hapo?
mbona amezungumza vitu "basic" sana ambavyo kila mwananchi mwenye akili timamu anatakiwa awe anavifahamu?
CCM ni sikio la kufa, halisikii tena dawa.
ReplyDeleteChama ni cha Matajiri; waache wabaki na Chama chao.
Natumai hawa mawaziri wetu wanapoenda kupiga siasa za chama mikoani wanatumia siku zao za likizo. Tunawalipa vizuri wawe mawaziri wetu, sio makada wa chama chochote. Tumewapa hata mazingira mazuri ya kazi kwa kodi zetu.
ReplyDeleteKuuliza si ujinga. Nini maana ya utupu?
ReplyDeleteHakuna cheche hapo. Nafurahi kuona kasisitizia yale yale yaliyosemwa na JK pale Mnazi moja juzi.
ReplyDeleteKitu kitakacho chafua Tanzania ni uongozi mbaya wa viongozi wetu, NA UONEVU PAMOJA NA WIZI WA MALI YA UMMA NA RUSHWA NA KUWASAHAU WANANCHI HII NI HATARI SANA TENA SANA VIONGOZI WASIPOSITISHA ITALETA MACHAFUKO, WIZI NA UJAMBAZI
ReplyDeletehongera prof mwandosya nakufafilia sana...uko juuuuu na tunakukubali kiongozi
ReplyDeletewe want changes!
ReplyDeleteNa Mbuge wa Serengeti sasa ni............
Dear Prof. Mwandosya
ReplyDeleteUgonile ndaga.
Hii hotuba yako ukaipenyeze hata katika vikao vya juu vya nec (Halmashauri kuu) ili wanaotaka kuvuruga amani kwa pesa zao za kifisadi wajirekebisha kama wataweza! Kweli tuko hatarini sanaaaa! Mungu atusaidie. Bahati mbaya sana, mimi naona watu wameanza kuchoka uvumilivu na inawezekana, badala ya kuuona uchaguzi kama sherehe wanaweza kuona kinyume chake. "TUNAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA SANA INJI HII"
The problem with this is: where do we cut the line btn politics and policies.
ReplyDeleteWhere do CCM ends before the govt starts