BBC World News, katika mfululizo wa vipindi maalum vya televisheni na radio, vile vile online, wameanzisha shindano la kuandaa makala fupi ya video - iwe ni umeipiga kwa digital camera au mobile phone camera, ruksa!
Zawadi
Video au filamu tano bora zaidi kutoka kila bara - Afrika, Amerika ya Kusini + Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Asia na Oceania, zitaingia katika fainali ambayo itarushwa kupitia matangazo ya televisheni ya BBC World vile vile zitaonyeshwa kwenye tovuti ya BBC.

Mshindi wa jumla atapatikana baada
ya hapo na kupewa zawadi ya
semi-professional HD mini DV camcorder.
Masharti
Masharti muhimu ya kuzingatia ni:
- Kila mshiriki anaweza kuwasilisha filamu/video moja katika lugha yoyote anayotaka kuhusu mada yoyote.
- Washiriki wanatakiwa kuandaa filamu/ video isiyozidi urefu wa dakika mbili (2), na wala isizidi 50MB katika format zifuatazo - avi, mov, wmv, mp4, mpg, flv, 3gp, wav, mp3, na wma.
- Wasilisha video uliyoifanyia kazi mwenyewe, usinakili wala kutumia kazi ya mtu mwingine.
- Tarehe ya mwisho ya kupokea filamu/video ni March 10 (1600 GMT)
Jinsi ya kushiriki
Kwa maelezo zaidi, na jinsi ya kuwasilisha
video yako tembelea wavuti ya BBC World News - My World.
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. haya wazee, siyo kila siku kulalama michuzi anawabania kuweka video zenyu, tuchangamkieni tenda - mambo polepole.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...