

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hongera Anko kwa kumsaidia huyo mtoto, mimi mwezi january nilikuwa vokesheni hapo Bongo, siku moja nilikuwa Posta na Rafiki yangu akanifuata Dada 1 hivi yupo smart kabisa akasema anaomba nimsaidie hela ya kula mimi sikusita nikangia mfukoni nikampatia chochote kitu, ila yule rafiki yangu wa bongo kuona vile baada ya kuwa yule dada kaondoka akanikanya nisirudie tena kumpa mtu pesa barabarani, kwani siku hizi watu wanaibiwa kila siku kwa stail hii, yani pesa unayotoa inaondoka na zingine zote ulizokuwa nazo. mimi nilikuwa na pesa nyingi kidogo mfukoni, basi nilipata sana hofu, kila dakika nilikuwa nahakikisha kama pesa zangu zipo, lakini hazikuondoka japokuwa mimi mwenyewe pia nilikuwa siamini kama zitaondoka, mimi binafsi nilisaidia sana watu bongo lakini sikuwahi kuibiwa. wenyewe wanaita chuma ulete. kweli kaka michuzi ipo kweli hii?
ReplyDeleteNi kweli ankal lakini tutaendela hivi hadi lini? Je, NGOs mbona hela wanajengea nyumba tu bila kusaidia walengwa?
ReplyDeleteKuwapa TZS 500/= si kuwasaidia. Twende kwenye root causes. Hawa watu wanakaa mtaani lkn wanazaa watoto wengi kuliko watu wenye kazi nzuri na uwezo. Wanazaa watoto wengi kuliko Mkapa, Clinton, Obama.... Hawa watu wanahitaji elimu na kazi ili waweze kujitegemea. Na hiyo kimsingi ni kazi ya serikali. Siyo kuwa-support waendelee kuishi na kula barabarani. Hiyo support yako ndiyo inafanya watoto wa aina hii wazidi kuongezeka siku hadi siku. Baadae wakifikia umri wa kubarehe wanavuta bangi na kuwa vibaka au majambazi. Watoto hawa wameongezeka miaka ya hivi karibuni na ujambazi umeongezeka! Mikakati ya muda mrefu ambayo iko nje ya uwezo wa mtu mmoja mmoja inahitajika.
ReplyDeleteMwalimu wangu wa Uchumi enzi zile nipo sekondari alituambia umasikini unarandana na birth rate kubwa, so mdau wa Sun Feb 14, 01:21:00 PM kuzaa watoto wengi ni sababu ya kutokua na shughuli nyingi za kufanya,ambazo zinahusisha matumizi makubwa ya akili. Ukienda uswahilini mida ya asubuhi siku za jumamosi au j pili halafu nenda mitaa ya wenye nazo mwenyewe utakubali. Lakini hili tatizo la ombaomba ni la kidunia si Tanzania tu
ReplyDeleteMichuzi toa NDOANO Sio SAMAKI!
ReplyDeleteHuyu mtoto na ombaomba wengine wananikumbusha kanchi fulani hapa duniani!!
ReplyDelete...kabla ya kushangaa kuwa na ombaomba hawa, tujiulize, ni kwa nini nchi ni Ombaomba miaka yote hii tunayojitawala??
Asilimia 40 tunalishwa na wafadili?? Kuna tatizo gani, are we "wachanga" au "crippled".
WATOTO HAWA NI JUKUMU LA SERIKALI KUWASAIDIA.WATOTO HAWA WANAOMBA NA WAZAZI WAO WAKO KIVULINI WANAWASUBIRI. UKISHAWAPA PESA WANAWAPELEKEA NA UKIWANYIMA WENGINE WANAKUTUKANA AU KUKUTEMEA MATE.MI NADHANI KWA KUWAPA PESA TUNAWAENDELEZA,WATIMULIWE WARUDI WALIKOTOKA NA KAMA MISAADA IWAFUATE HUKO HUKO. NA WENGINE SIKU HIZI WANASAFISHA VIYOO VYA MAGARI, UKISEMA SITAKI KUSAFISHIWA WANATOA SITE MIRROW YAKO WAKATI TAA ZIMERUHUSU YAANI HAWANA TABIA NZURI HATA KIDOGO. SERIKALI KWA KUPITIA NGOs IWASAIDIE. WATU WANAPENDA SANA KUTOA MSAADA LAKINI SI KWA NAMNA HII.
ReplyDeleteNafikiri kwa kuwapa fedha sio kuwasaidia,sana sana serikali ichukue jukumu la kuangalia jinsi ya kuwasaidia na kuwaondoa kabisa mana najua inao huo uwezo ila ni ufuatiliaji tuu sio mzuri
ReplyDelete