wakongwe wa muziki toka shoto mafumu bilali bombenga, ras inno nganyagwa, carolla kinasha na che mundugwao katika warsha hii waandaaji na washiriki wa warsha hii
Mtaalamu wa hakimiliki ambaye pia ni mhadhiri wa sheria Adam Mambi akitoa mada kuhusu rasimu ya mapendekezo ya sheria mpya ya hakimiliki kwenye warsha ya mada hiyo hoteli ya Lamada jijijni Dar leo. Washiriki ni wasanii na wadau toka sehemu mbalimbali


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mh. Ghonche Materego, akifungua warsha ya kupitia rasimu mpya ya hakimiliki leo katika hoteli ya Lamada jijini Dar. Shoto ni Angelo Luhala wa Rulu Arts, waandaaji wa warsha hiyo na kuume ni Ruyembe Mulimba wa Basata
Mh. Materego na baadhi ya washiriki wa warsha hio wakienda kupumzika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Bwana Michu,naomba muulize Mheshimiwa Materego,hiyo shati ya Batiki kainunua wapi? Nimeipenda sana.
    Chakubanga

    ReplyDelete
  2. Hahahaha Mr Gonche very funny.....ni muda mrefu sana tangu nlipofanya semina na Gonche that was 1999 (UNICEF), miaka kumi na moja sasa ,mzee wa michakato,semina haiboi mkiwa na Gonche na rafiki yake maskini Mungu amweke mahali pema peponi alifariki,anyway nimefurahi kumuona tena baada ya muda wote huo mvi kibao tehteh.

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kazi na mwelekeo mzuri nzuri.
    Taifa letu linahitaji sera za hakimiliki kamilifu na zinazokidhi haja.
    Twapasa wote tuwe wachangiaji wa zoezi hili hususan watafiti na wavumbuzi wa tiba na madawa, wabunifu wa fani za aina mbalimbali km uchongaji, ujenzi, mitindo ya mavazi, mapishi, mbinu za kipekee za kilimo na utunzaji nafaka,ufahamu wa uwepo wa milki ya kipekee ya mimea,wanyama na ndege nchini,uchoraji, ghani za sauti na muziki, nk
    Hakimiliki ni pana na ni maisha ya kipekee. Tuifahamu,tuijali na tuimilikishe.
    MAINA ANG'IELA OWINO.

    ReplyDelete
  4. safi ,shida ya materego na basata kwao wao wa kuwaalika ni haohao kila siku panueni wigo wasanii si hao tu wa kwenye televisheni na radio.toeni tangazo hawa waacheni wakazindue makampeni ili mpate mwazo mapya.ukiibania poa kwani ukiona bango limechanwa ujue ujumbe umefika

    ReplyDelete
  5. RAS INNOOOOOOOOOOO LONG TIME BROTHER. I STILL REMEMBER THOSE DAYS. MISS YOU MAN. NICE TO SEE YOU AGAIN. ALL THE BEST. HOPE TO SEE YOU SOMETIMES IN THE FUTURE.
    Its Me Your FAN.

    ReplyDelete
  6. Hi kaka Issa Michuzi,
    Kwanza napenda kukupongeza kwa kutupasha habari za nyumbani hasa sisi tunaoishi nje ya nchi. Pili ningependa kuchangia machache kuhusu hatua iliyochukuliwa na wasanii wa nyumbani kujielimisha kuhusu sheria zinazolinda haki za kazi zao. Kwa muda mrefu wasanii wa Tanzania wamekuwa wakilalamika sana kuhusu ukosefu wa usimamizi wa kazi zao hasa dhidi ya uuzaji holela wa kazi hizo.Kilichokuwa kinashangaza ni kuwa kati ya wasanii wengi waliopata nafasi ya kulalamika katika vyombo vya habari ni wachache sana waliweza kuzungumzia sheria kiundani na kueleweka na jamii kubwa ya Watanzania. Ukosefu huu wa elimu na uelewa wa sheria kuhusu ajira zao umekuwa ukikwamisha juhudi za COSOTA kuingia katika vita na wauza feki mtaani. COSOTA kwa hakika hawana nguvu kubwa kama wasanii wenyewe hawaelewi kinachoendelea. Mimi nadgani semina hii ni mwanzo mzuri sana wa kuungana na COSOTA na kupambana na watu wachache wanaohujumu jasho la vijana wengi wanaojaribu kujiajiri nchini. Ningependa kusisitiza kuwa huu ni mwanzo tu kwani semina kama hizi inaboidi ziwe za mara kwa mara na zisilenge wasanii tu bali pia vyombo vya dola na hata wanachi wa kawaida kwani wao ndio wanunuzi wa kazi feki mtaani.

    Paul Mbenna (Mr Paul)

    Sydney, Australia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...