daladala sio tu zikipita juu ya sehemu ya kati inayotenga barabara mbili sehemu za mbagala jijini dar, bali pia zinasimama na kupakia na kupakua abiria. haieleweki madereva hawa walikuwa wana nini vichwani mwao, na wengine kama wao kama alivyoshuhudia mdau mac temba aliyeleta taswira hizi. anasema hii tabia imeota mizizi maeneo hayo hata baada ya kumalizika ujenzi wa barabara ya lami ya njia mbili...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Tatizo ni kwamba tangu wazaliwe hawajawahi kuonana na serikali ambayo iko serious. Sumatra ili-contract majembe ili ku-enforce sheria za barabarani, mara hawa mabaradhuli wakagoma eti wanaonewa! Serikali isiyo serious ikawasimamisha majembe! Mtu akilia anaonewa ujuwe kashikwa kubaya - hapo ndiyo pa kuendelea kushika ili afuate sheria. Lakini wenzetu walioko serikali wanaona mambo ni tambarare tu! Kweli kuna kazi Bongo. Sasa itizame hiyo barabara baada ya miaka 3 hivi, itakuwa haitamaniki. Atakuwa eti anatafutwa mfadhili wa kuitengeneza tena! Nakwambia huko hata ukinihonga Ukurugenzi wa NHC sirudi.... Acha tu nisukume siku hapa taratibu na box langu.

    ReplyDelete
  2. SITORUDI TANZANIA MAISHA YA KIMBUMBUZI BASI, NIHERI UBEBE BOX HUKU KWENYE BUSARA KULIKO KUWA WAZIRI BONGO

    ReplyDelete
  3. Ndugu mdau hapo juu sio baada ya miaka 3 sasa hv imeshakua mbovu..na huu ni uzembe wa serikali (SUMATRA NA TRAFFIC POLICE)Barabara yenyewe tumejengewa kwa msaada wa kodi za wananchi wa Japan,yaani hao washenzi wa dalala wanaiharibu makusudi na akikamatwa traffic anapozwa na buku 2 tu! kweli tutafika?

    ReplyDelete
  4. Watanzania tumezoea kutofata sheria,jamani tujitahidi watoto wetu wawe more responsible sio mpk tuwekewe traffic barabarani wasipokuwepo tu basi kila mtu anajiona ana haraka.

    Hiyo barabara now ishaanza kuchoka, jamani watanzania mbona hatupendi vitu vizuri kwa kuvitunza?

    ReplyDelete
  5. Serikali ikiamua kuinvest kwenye upuuzi wa daladala kwa njia ya kujikusanyia PENALTIES....yani mbona hatutahitaji pesa ya mfazili kwa ajili ya the so called FLYOVERS.

    ReplyDelete
  6. Huu ni ujinga na uwendawazimu.

    Hapa mtu ameshindwa kuchagua lipi jema lipi mbaya.

    Yaani kwa maana nyingi akili zao ni kama za kandoo au ng'ombe tena wa kufuga ndani ambaye analalia kinyesi na mkojo wake.

    Maendeleo Tanzania ni ndoto.

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana na mdau hapo juu kuwa watanzania wengi wamezoe maisha ya kimbuzimbuzi. Hii ina maana hawana akili za kufikiri na kuwa waastarabu.

    ReplyDelete
  8. Bloggers wenzangu,tatizo halipo upande wa serikali(Police,Sumatra,traffic police),tatizo lipo kwa wabongo wenyewe,hatuna utamaduni wa kujali na kuthamini mali au miundombinu iliyowekwa na serikali,ndio maana kuna usemi usemao,waafrika wengi kama ngozi zetu kama za tako!,
    Askari hawezi wakalinda kila sehemu,hii tabia ikiendelea tutahitaji askari hata manyumbani kwetu ili kuzuia watu wasinye au kukojoa kwenye kuta za nyumba zetu,au bustanini,
    Hiyo picha ni just mfano mdogo wa tabia za kishenzi zinazofanyika na sisi wenye ngozi kama ya tako.Ule uwanja wa taifa wa mpira serikali imegharamia zaidi ya bilion 200 Tsh,lakini ukiingia vyooni unaweza kulia jinsi jamaaa wanavyoharibu miundo mbinu,sink zinageuzwa urinals,jamani hivi wabongo tumerogwa? Daraja la mto Kibiti limegharimu zaidi ya bilion 30 ,wabongo wanaiba vyuma vilivyowekwa pembezoni mwa daraja,wanauza as scraper,jamani,nani alaumiwe serikali au raia?

    Nchi za wenzetu,kukojoa au kutema mate ovyo huwezi ona vinafanyika na ukikamatwa ,sheria kali zinachukuliwa,lakini kwetu watu wanafanya uhalibifu wa miundombinu na mazingira bila ya kuionea huruma nchi yao,
    Namalizia kwa kusisitiza kwamba ulinzi wa mali za serikali au mazingira kwa ujumla ni jukumu letu sote,ukiona mtu anafanya vile basi wewe ripoti kwenye vyombo husika au muelimishe kuwa anakosea,bila sisi kuwa na utamaduni huu,basi serikali pekee haitoweza,kwani raia ndio tunawajua hawa watu,
    "Tukatae kufananishwa na ngozi ya makalio"

    mdau Kisenga

    ReplyDelete
  9. Bw Kisenga,

    Nchi yenu ya Tz inahitaji u-dictator fulani. Raia wa kawaida tu kama mimi na wewe hawawezi kufanya u-dictator huo ambao unahitajika kubadilisha watu. Ni serikali na vyombo vyake ndiyo vinaweza. Ndio, kila raia ana wajibu lkn katika hali ambayo nchi yenu imefikia sasa hivi, mimi na wewe - wawili ama watatu - wenye moyo wa utu na kuelewa tutafanya nini? Mathalani, sasa kama wewe unawaona madereva wenzio 50-100 hivi wanaamua kuanzisha "lane" pembeni mwa barabara ambako magari hayastahiri kupita utafanya nini? Utashuka kwenye gari na kuanza kuwahubiria? Nadhani Mr Kisenga ni vizuri fikiria vitu ambavyo ni practical kuliko kutoa generalised impractical solutions za kisiasa siasa ambazo hazisaidii.

    ReplyDelete
  10. mzee kasenga uko makini,
    ukisema mwafrika una-reflect uchafu kila kona ya nchi, ujinga, uongozi mbovu serikalini,watu wasiotaka kutekeleza majukumu yao wakiwa makazini,elimu mbovu na isiyojaliwa,ujambazi na unyang'any'i, wananchi wasiotaka mabadiliko hata kama ukweli wanauona,masikini na uvivu, udokozi na mambo mengine yanayofanana na hayo.

    ReplyDelete
  11. Mdau Kisenga unajua hata hao walioendelea ustaarabu haukuja kama ndoto naomna hiyo. Utamaduni na ustaarabu unajengwa siyo unajiotea tuu. Tunailaumu serikali kwa kutosimamia sheria kikamilifu, wao kazi yao ni kuzitunga tuu basi sasa watu wanafuata au hawafuati the don't care. Serikali ina nafasi kubwa sana katika kuhakikisha sheria zinafuatwa na adhabu kali zinatolewa ili kukomesha tabia hizo baadae watu watazoea kuwa kuna adhabu nitapata na tabia itajengeka. Hatuwezi tuu kuamka siku moja kila dereva akafuata sheria ni lazima kulazimisha hii tabia..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...