mabango kwa Kakobe yakiwa chini muda huu
Ankal pole na shughuli bro. Sasa hivi katika pita yangu mitaa ya Mlimani city huku Mwenge nimekuta mafundi wa TANESCO na kampuni moja toka JAPAN wanayaondoa mabango ya kanisa la FULL GOSPEL FELLOW SHIP ambalo linaongozwa na Mchungaji Zacharia Kakobe chini ya ulinzi mkali wa polisi bila shaka kuruhusu kupitishwa kwa waya za umeme.

By Mdau,Kashaga Boniphace

Juu na chini ni mabango ya kanisa la Kakobe yakiondolewa kwa winchi
-------------------------
HABARI KAMILI
Hatua hii inakuja baada ya serikali kuliruhusu Shirika la Umeme (Tanesco) kuendelea na mradi wa kupitisha nyaya za umeme wa msongo wa 132KV juu ya eneo hilo, baada ya ya waumini kulinda majengo ya Kanisa hilo la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) kwa takribani miezi mitatu

Waumini hao walikuwa wakikesha usiku na mchana kwa lengo la kuzuia wafanyakazi wa Tanesco kupitisha nyaya hizo juu ya kiwanja cha kanisa hilo lililo jirani na eneo la Mwenge wilayani Kinondoni baada ya mkuu wa FGBF, Askofu Zacharia Kakobe kupinga mradi huo na kutangaza eneo hilo kuwa la hatari kwa wafanyakazi wa shirika hilo la ugavi wa umeme.

Askofu Kakobe anadai kuwa mradi huo wa thamani ya Sh34 bilioni kutoka serikali ya Japan haufai kupitishwa juu ya eneo la kanisa hilo kwa kuwa ni hatari kwa afya za waumini wake na unaweza kuharibu mawasiliano ya ndani wakati wa ibada, ambazo alisema hurekodiwa wakati zikiendelea na pia kudai kuwa utavuruga mawimbi ya televisheni kwa kuwa kanisa hilo lina mpango wa kujenga studio ya runinga.

Askofu huyo alidai mradi huo ulipingwa na wakazi wa maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndio maana ukakwepeshwa hivyo anataka Tanesco pia ikwepeshe nyaya zinazotakiwa kupita juu ya kanisa lake lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma.

Lakini Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alisema kuwa serikali imejiridhisha kuwa mradi huo hautakuwa na athari za kimazingira na afya ya binadamu na hivyo kutupilia mbali ombi la Askofu Kakobe la kutaka nyaya hizo zipitishwe katikati ya Barabara ya Sam Nujoma.

Ngeleja, ambaye wizara yake ilifanya vikao kadhaa na uongozi wa FGBF, alisema eneo la katikati ya barabara hiyo haliwezi kutumika kwa ajili ya nyaya hizo kwa kuwa tayari lina nguzo za taa za barabarani na kuongeza kuwa eneo hilo la kati linakusudiwa kutumika kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. kakobe unatuangusha waumini wako.
    kutushindisha juani miezi yote hiyo, nakutulaza nje halafu unalegea dakika za mwisho!

    ReplyDelete
  2. Asante mdau wetu kwa taswira na taarifa ya kijamii.Naomba wanajamii tupewe majawabu yafuatayo kutoka kwa mamlaka na madhamana wa ardhi.Je eneo hili limetangwa kwa ajili ya kanisa au makazi?Je sehemu inayotumiwa kupitishia nyaya ni sehemu ya hifadhi ya barabara chini ya miliki ya Tanroads?Je haya mabango yanayohamishwa yaliwekwa nje ya mipaka ya kanisa na hifadhi ya barabara au?Ni vema waandishi wa habari wajikite zaidi katika kuelimisha umma katika matukio yenye mguso kwa jamii kuliko kuripoti tu kwenye media.Kwa kuwa tukio tukio hili watu wa media hawajaonyesha wazi haki za kanisa zinaanzia na kuishia wapi na haki za Tanroads kwa niaba ya Tanesco.
    Naomba muelewe kuwa Tanesco wanapaswa kutumia sehemu ya hifadhi ya barabara kwa mujibu wa madokezo ya Tanroads na siyo kuingia kwenye miliki halali ya watu wengine.

    ReplyDelete
  3. Jamaa ameshatupiga bao la mgao wa umeme sasa atatuongezea makali, kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  4. Kakobe bwana,umekuwa mpooooleeee,kelele kibao aahh. Ushakula kitu kdg kimyaaa. Bongo tambarare,tupoze basi na sisi wafuasi wako angalau tupate ya kununua Panadol kwa kuumia kichwa thru Jua kali.

    ReplyDelete
  5. Kakobe sali sala takatifu ili Waziri wa hiyo wizara atimulliwe maana hakuna anachokifanya ni uhuni tu na hiyo Wizara ifutwe...

    ReplyDelete
  6. Asante serekali kwa ujasiri na kuifanya mamuzi ya kupitisha nyiwaya za umeme ili wananchi wanufaike na sio kikundi fulani kinaweka vizuwizi juu ya huduma bora kwa nchi na wananchi kwa ujumla

    Hakuna lisilo wezekana

    ReplyDelete
  7. kakobe ni vizuri akajenge kanisa kwao kwani Dar watu wanamjua yesu wajenge makanisa mikoani kama Mara kwani huko mungu ni ndoto tumechoka na makanisa kajengeni mikoani kwenuuuuu

    ReplyDelete
  8. Mdau namba mbili ulikuwa wapi wakati majadiliano yanaendelea?

    Naona unaturudisha nyuma kwani mjadala huo umeongelewa kwa urefu sana.

    Hilo ni eneo la kupitisha huduma na siyo eneo la Kanisa na hoja za Mheshimiwa Kakobe zilikuwa kwamba wakipitisha nyaya hapo basi waumini wake wataathirika.

    ReplyDelete
  9. hakimu wa mahakimu ni bwana Yesu yeye ataamua

    ReplyDelete
  10. Kama hilo eneo zinapopitishwa nyaya za umeme ni kwa ajili ya huduma za jamii ni asante Tanesco kwa kufuata sheria za nchi.Hao waumini ni mali Mungu kwa imani yao na siyo wa mtu yeyote.Suala la kuathiriwa na upitishwaji huo wa nyaya za umeme linahusu wananchi wote na kamwe tuanze ubaguzi wa kiimani.Kama utetezi uelekezwe kwa wananchi wote na siyo waumini wa eneo moja na kuwaacha wengine bila msaada ufaao.

    ReplyDelete
  11. annon 10:48 pm
    kweli kabisa na amen!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...