Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda akifuatana na Bi Amina mlemavu asiyeona alipotembelea makazi ya wazee na watu walioathirika na ukoma kijiji cha Sukamahela, wilayani Manyoni leo.
Naibu Waziri akisalimiana na mmoja wa wakazi wa makazi hayo katika nyumba zilizokarabatiwa hivi karibuni na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya wakazi wa makzi hayo pamoja wa wananchi wa kijiji cha Sukamahela wakicheza ngoma ya Kigogo katika mkutano wa hadhara ulofanywa na Naibu Waziri Dk. Aisha Kigoda.
Wananchi wa kijiji cha Sukumahela wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizra ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Aisha Kigoda kwenye mkutano wa hadhara ulofanyika kwenye viwanja vya makzi ya wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ya Sukamahela.Muuza mafagio alisitisha kutembeza bidhaa yake akajumuika kumsikiliza.
Naibu Waziri akisalimiana na Bi Christina Lameck makazi wa kijiji cha Maweni, katika hospitali ya Kilimatinde,Hospitali ya Kilimatinde iliyoanzishwa mwaka 1929 na inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana hutoa huduma za afya wa wakazi wengi wa wilayani hao.
Picha zote na Mdau Cathy Sungura







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kijiji cha sukumahela!! watu hapo hawatunzi hela?

    ReplyDelete
  2. Uchaguzi mkuu Oktoba unakaribia. Tukae mkao wa kula. Ni hayo tu

    Mdau wa Mbezi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...