Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein kulia, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Pembe Juma katikati, Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakisoma Dua ya pamoja kwenye eneo la Makaburi ya Wazee baada ya kumaliza kusoma Hitima maalum iliyoambatana na Maulid yanayosomwa kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa kwanza kushoto, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa pili kushoto, Rais mstaafu wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi wa pili kulia, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Pembe Juma, wakielekea kwenye eneo la Makaburi ya Wazee walitangulia mbele ya Haki mara baada ya kusoma Hitima maalum kwa ajili ya Marehemu hao katika Msikiti Mkuu wa kijiji cha Kidombo uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, ambapo Dua hiyo iliambatana na Maulidi ya nayayosomwa kila mwaka kijijini hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi wa kwanza kushoto, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa pili kushoto na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, wakisoma Dua ya pamoja baada ya kumalizika Dhifa maalum ya Maulid ilioyoandaliwa na Dk. Salimin Amour, inayofanyika kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kulia, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour katikati, na Rais mstaafu wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi, wakisoma Hitima maalum ya kuwaombea Wazee mbalimbali waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika jana katika msikiti wa kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja leo. Picha na mdau Amour Nassor




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Leo ndo namwona Salmin. Kushika madaraka ya kuongoza nchi bado kijana taabu yake ukishamaliza muda wake una bado muda mrefu wa kukaa unaangalia wengine wanavyovanya mambooz. Afadhali kuanza tawala una miaka 50 unapostaafu unakuwa mzee wa kushauri

    ReplyDelete
  2. Ni kweli Dk. salmin Amour haoni?!! au maneno ya watu!!

    ReplyDelete
  3. du salmin kumbe anaoona sasa duu
    mungu mkubwa,mheshimiwa muombe sana toba mola wako.

    ReplyDelete
  4. jamani kulikuwa na tetesi kwamba mheshimiwa mstaafu raisi salmin yuko kipofu haoni sasa mbona huyo anaona au ametibika kwa kuwamba waliomtenda radhi.

    ReplyDelete
  5. ndugu ama hakika kifo hakina mjadala maana kila mmoja wetu atakipitia maadamu amezaliwa. cha kusikitisha hapa naona hata dua hizi za MUNGU siasa ingali inapewa kiupa mbele wakati siasa ni uongo mtupu mara nyingi. sababu ya kusema haya sioni wananchi wengine ila vigogo tu je jamani hata MADUA YA MUNGU KUNA MA GROUP. JAMANI TUMUOGOPE MUNGU DUNIA NI YA KUPITA NA NDIYO MTUME MOHAMMAD SAW ALITUAMBIA TUZURU MAKABURI ILI KUKUMBUKA KUWA SISI NI VIUMBE WAKUPITA HIVYO SIYO KUKUMBUKA TU BALI KUTENDA MEMA AMBAYO TUNATAKA KWA WATOTO WETU NA SISI BASI IWE KWA KILA KIUMBE. TUONDOE TAMAA ZA DUNIA KWANI SIYO ZA KUDUMU BALI NI MUDA NA WAKATI WOWOTE TUNAWEZA KUTOWEKA. MUNGU ATUJALIE TUWEZE KUFUATA AMRI ZAKE KWA MATENDO NA SIYO KWA KWA FAIDA YA KIBINAFSI. WASALAMU NDUGU YENU MOHAMMED

    ReplyDelete
  6. Jamani hata kusafisha kidogo hayo makaburi???!!

    ReplyDelete
  7. Mdau Tarehe Mon Mar 08, 06:12:00 AM, hakuna siasa hapa. Kwani wamekutana wakaamua waende pale labda baada ya kumaliza shughuli fulani waliyokuwa wanafanya pamoja. Na wewe na wenzio mwawezafanya hivyo hakuna kizuizi. Lakini pia kuna tabia ya watu kutaka kujichulia umaarufu kama yule aliyempiga Mzee wetu kibao bila sababu

    ReplyDelete
  8. mdau tarehe monday mar 08, 01:3600pm hakika unatoa mpya itakuwaje wote wawe vigogo tu hiyo siasa. naona unashangaza sana picha yote imeonyesha vigogo halafu unasema siyo siasa sina shida ya umaarufu ya kumpiga binadamu mwenzangu kwa kutaka umaarufu huo siyo umaarufu mzuri bali ni mbaya. muhimu mimi na wewe hatujui anayejua ni MUNGU NA WAO NA TUNAOMBA KHERI TUFANYE YALIYO NA KHERI AMEN wasalamu mohammed

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...