Tatizo la msongamano wa magari
Dar es Salaam na kwingineko:
Kuingia barabara kuu (Highway intersections)

Naomba nami nichangie mjadala wa tatizo kuhusu msongamano mkubwa ma magari Dar es Salaam ambalo kwangu ni sababu KUU mojawapo ya kupendelea kukaa mikoani na kufanyia shughuli huko.
Na mimi nchi yangu inanisikitish kitu kimoja, kupenda kutatua matatizo wakati wa maafa (crisises?) yakitokea. Tunakaa wee likiharibika ndio twaanza kufikiri. Mengi yamesemwa lakini mimi nitapenda kuchangia sehemu mojawapo ambayo naona haijatajwa (kama imetajwa binafsi sijaona) katika mdahalo huu, nalo ni kuingia kwa magari kutoka barabara za mitaani (ntaita za kitaa) na kwenda kwenye barabara kuu (highway intersection points) na kutoka.

Yametolewa mapendekezo kuwa tatizo ambalo linasababaisha traffic kubwa ni kwenye mataa (traffic lights). Hapa wadau wamependekeza fly overs ili magari yasisubiri (fine). Pia mdau katoa kero inayosababishwa na matuta barabara ya morogoro hususan morogoro road eneo la Stop over na mengine mengi.

Lakini wakubwa huko mipango wanashindwa (Sijui hawataki kufikiri au wanakaa tu kimya makusudi) kutambua ya kuwa barabara kama ya Morogoro au Port access (Mandela kwa sasa nafikiri), pia Bagamoyo (Ali Hassan Mwinyi), na kwa mikoani kama Tanga (niliko na uzoefu nako) ile inayoingia Tanga mjini kutoka mikoani zote hizi ni BARABARA KUU (HIGHWAYS).

Sasa, kama ni highway ni kuwa magari yakipita muda wote yanakwenda kwa spidi angalau ya juu ya Km 80 kwa lisaa na zaidi muda wote. Nafikri kunatakiwa kuwe na kiwango maalumu cha spidi, hususan ya juu. Cha ajabu hapa kwetu hizi barabara zote zina matuta. Tena mengine ni ya kufa mtu!
Nakumbuka siku moja natoa gari Dar bandarini napeleka Tanga, jana yake kumbe waliweka matuta kuingia sehemu moja inaitwa Hale. Ilikua ssa moja moja hivi kigiza kimeingia, yaani we acha tu! vituta viliwekwa vile vifupi ujazo kama saizi ya nguzo za umeme, alafu vipyaa vitatu!!. Na wala kulikua hakuna alama kuwa tuta lipo..pata picha.

Nionavyo tatizo lililo kubwa ni kuwa magari yote yanayotoka katika barabara za ndani (Kitaani) pande zote mbili, kwa mfano, pale Kimara temboni, Suca, mbezi mwisho, pabaya sana ni stopover, zote gari inatoka ndani moja kwa moja inaingia highway gafla! Hii moja kwa moja inaleta foleni na hata kusababisha ajali.
Ukiangalia kwa wenzetu, kwa picha hiyo hapo chini utaona kua gari linapotoka kitaani hata sikumoja haliingi moja kwa moja gafla kama hapa kwetu. Lazima kuwe na ustaarabu wa kuingia ili usimbuguhudhi Yule aliyeko highway na spidi zake lazima aingie kwa spidi yenye kuendana na ile ya highway. Inabidi uchochee kasi ndipo uingie. Hata Yule aliyeko haighway moja kuingia nyingine, lazima aingie kwa spidi ya aliyemo.

Vilevile, kwa magari yanayotoka highway kuingia kitaani lazima kuwe na exits (mitoko) za kistaarabu. Kwa wenzetu unatayrishwa kabisa, kwamba baada ya kilometre moja exit (mtoko) ya kimara inakuja, then unaambaa taratibu kushoto (kwa wale right handed kulia) unatoka zako ndipo unakutana na mataa/traffic lights sasa za kukukaribisha kitaani.
Sisi solution iliyotolewa ni kuweka matuta kabla ya kufika kwenye barabara ya kuingia kitaa. Hii ppia iangaliwe. Zamani mtu ukitoka Tanga unatumia masaa manne kamili kwa basi. Lakini kwa sasa ni masaa matatu mpaka kibaha, na matatu au hata manne mpaka pale Ubungo stendi kutokana na matuta au kusubiri gari lililoko mbele yako liingie kitaa chake mbele. Naona hakuna haja ya kuhamisha stendi mpaka mbezi, ni kurekebisha barabara tu. Wengine watasema ziwekwe double road kila mahala. Sawa, lakini ustaarabu wa kuingia highway lazima uwepo.

Na mikoani kwenye kila kituo, kabla ya kufika matuta yamejaa tele, hakuna hata raha ya kuendesha gari. Ni kosa nafikiri kwa highway kuwa na matuta. Sikuizi miji inapanuka pembezoni mwa highways zetu.
Watu nao wanaongezeka. Basi mtu akigongwa tu wanalala barabarani mpaka waletewe matuta, na ndicho kilichotokea barabara ya Tanga kuanzia Segera. Ilikua kati ya barabara bora kuliko zote kutengenezwa Tanzania, mpaka leo haijaharibika vile. Ni matatuta ndio yameiharibu.
Kama watu wanagongwa (kwanza kusiwe na crossing ya watu kwenye highways) ama wapite juu au chini kwa mpangilio unaofaa. Pia, kwa nini kila kimji kiwe na barabara ya kuingia highway? Kila baada ya kakilometa kuna kakituo pembezoni tu mwa “highway”, ukiongeza na ustaarabu wa daladala wa kuingia na kutoka kituoni kuingia highway nalo tatizo linazidi la foleni na ajali kwani mtu yuko highway basi laingia gafla. Ingefaa vituo vyote view kama cha pale kibaha au ndani zaidi, na kuingia kwao highway waingie kwa kasi inayofaa. Kama vipi tubadilishe maana ya barabara zetu, kama ile ya morogoro, je ni highway au kwa sasa inafaa (qualify) kuwa ya kitaa? Kuanzia kibaha ndio iitwe highway kwa maana ya highway yenye spidi.

Kwa watani wa jadi hapo Nairobi nimeona wamejaribu lakini highway intersection zao ziko very tricky, yaani ni fupi mno. Haimpi mtu nafasi ya kuchochea spidi mpaka kuingia highway hivyo nao bado ajali ni nyingi.

Ila mdahalo wa foleni pia ni mpana na unataiwa kuboresha sehemu nyingi tu, kama kuboresha public transport ili watu wasinunue magari, hii ni mjadala mwingine tena.

Wengine wataboresha haya niliyoandika, mathalani maana, mpangilio na matumizi, hasa ya neno barabara kuu.

Ni hayo tu kwa leo
Mdau Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Umesema vema mjumbe. Lakini nina mawazo tofauti kidogo. Unapozungumzia highway kwa maana ya ''highway'' ninayoijua mimi pengine tunauelewa tofauti ama mtazamo tofauti kidogo.

    Kwangu mimi Highway ni barabara ambayo magari hutakiwa kwenda kwa mwendo kasi uliopendekezwa ama pungufu yake kidogo - mara nyingi mwendo unaopendekezwa ni mkubwa kidogo (kama 80/100/120km n.k kwa saa). Then dereva anayetokea kwenye ''intersection'' anatakiwa kwenda na mwendo almost sawa na mwendo wa highway. Kwa barabara za bongo nadhani hakuna ''intersections'' to the highway(s) kwa maana kwamba dereva hawezi kupinda na kujiunga toka barabara hizo akiwa na speed karibu sawa na ya highway (ili asi-disturb- waliokatika highway. Nadhani barabara zilizopo along morogoro road ni interseptions lakini si interseptions to highway kwa jinsi nielewavyo mimi.

    Kubwa zaidi, highway halisi haiwezi kupita ndani ya mji kamwe kwasababu barabara ndani ya mji ama sehemu zilizojengeka inawatumiaji wengi mno - waenda kwa miguu, baiskeli, maguta, magari n.k. Kuweka mwendo kasi wa juu ni kuhatarisha maisha katika maeneo haya. Pia uelewa wa watumiaji wa barabara ni mdogo sana. Hawataki kwenda kuvuka kwenye maeneo yaliyotengwa. Manzese kwa mfano. Utawasaidiaje kama si kwa kuweka matuta?

    THEN kutokana na ukweli kwamba madereva wa bongo hawataki kufuata mwendo uliopendekezwa matuta yanabakia kuwa suluhisho. HATAHIVYO, SHERIA IKIWA KALI WANAWEZA KUIFUATA. Katika nchi za wenzetu watu hufuata sheria za barabarani si kwa kupenda as such, bali kwasababu sheria zinawalima sana!!

    Fly-overs zinaweza kuwa suluhisho la hakika. BUT DO WE HAVE THE MONEY? WELL, YES! Wenye dhamana wasizipeleke mifukoni mwao!!

    ReplyDelete
  2. mdau unamaanisha Highway = freeway?
    Freeway = spidi kali bila kuzuia na magari mengine hizi ndio kwa Obama wanaita Interstate Highways; na hapa wajerumani wanaziita Autobahn; na wazungu wengine wanaziite Motorways
    Kwa kiingereza barabara zimegawanywa katika mafungu yafuatayo:
    Freeways
    Major Arterials
    Minor Arterials
    Collectors
    Local Roads
    Morogoro Road Tanzania's Standard inaitwa trunk road... kwahio kufuatana na kazi yake kwa wazungu itaitwa Major arterial.
    Intersection za Major arterials zinaweza kuongozwa kwa taa za magari ama alama ya kusimama (stop) pia zinaweza kuwa na vituta vidogodogo (rumble strips) kupunguza speed kwenye maeneo ya mjini ama vitongoji. Vituta hivyo inabidi viambatane na alama za vitambulisho na kupunguza speed (reduced speed ahead) sasa kama porini Morogoro road is posted 80kph, its limit need to gradually reduced up to 40kph kwenye vitongoji.
    Tatizo lipo na kila mtu analijua (wahandisi na wasiowahandisi)ama (watumiaji na wasio watumiaji). Tatizo kubwa ambalo serikali inabidi kurekebisha ni sera yake ya barabara kwani imepitwa na wakati na haikidhi mahitaji ya watumiaji wa barabara--magari, baisikeli na wapita njia. Na kama ulivyosema si Dar tu hata mikoani.
    Pia ikumbukwe kuwa matatizo ya tanzania ni mengi....sijui tuanzie na lipi...Maji, Umeme, Afya (wajawazito kila siku wanapotea),Elimu, Usalama wa maisha.........yaani kila siku jana afadhali ya leo. Wakati huo huo wachache sana wanaishi maisha ya dunia ya kwanza.

    ReplyDelete
  3. Mawazo mazuri,lakini ni kumpigia mbuzi gitaa!
    Kama kweli wangekuwa wanajali wangeonyesha juhudi kwenye barara mpya wanazojenga sasa hivi.
    kwa mtazamo wangu,flyovers kwenye juctions ni utatuzi wa haraka.

    ReplyDelete
  4. Wadau kwa kweli sisi wanye nchi tuna mawazo mengi tena mazuri na pia tunajitahidi kufikiria namna mbalimbali za kutupunguzia au kuondoa matatizo yetu.
    Tatizo ni kwamba si kazi yetu kufikiri maana wapo watu tumewaajiri, tunawalipa kwa kazi hiyo na wao hawaifanyi hiyo kazi ya "KUFIKIRI".

    Badala yake wanakuwa saa zote wanafikiri jinsi ya kuomba MISAADA.

    matokeo yake kama hatutawabadilisha tuliowaajiri basi tutabakia hivi hivi tunahangaika weeee lakini tunabaki pale pale au tunazidi kurudi nyuma.

    Sasa tutawabadilisha vipi tuweze kuajiri wengine ambao wataweza kufanya kazi ya KUFIKIRI JINSI YA KUTULETEA MAENDELEO BADALA YA KUWAFURAHISHA WAHISANI. MAANA IMF, WORL BANK, EU, USA, JAPAN,UN NK WAKISEMA NDIO WATUMISHI WETU(KWA MANENO MENGINE NI VIONGOZI WETU) HUKIMBIZANA KUWARIDHISHA. LAKINI SISI TULIOWACHAGUA NA TUNAOWALIPA MISHAHARA NA KUWAPA HESHIMA TUKILIA, TUKILALAMIKA, TUKIFA KWENYE HAYA MAAFA YA BARABARANI TUNACHOAMBULIA NI SALAM ZA RAMBIRAMBI SASA HADI LINI?!

    STAND UP, STIR UP, STAND UP FOR YOUR RIGHT...ALISEMA BOB NAFIKIRI
    Mzawa

    ReplyDelete
  5. Candid ScopeMarch 21, 2010

    We Anomy wa kwanza umechemsha hapa. Hujaelewa maana ya Highway. Highyway ni barabara kuu kwa kiswahili na inamaanisha inaunganisha wilaya, mikoa na hata nchi zaidi ya moja. Tusichanganye express highway au free way ambayo hakuna traffic lights au vizuizi vingine barabarani na marufuku kusimama isipokuwa kama gari limekuwa disabled you have to pull close to the cub ili kuruhusu mengine yaendelee kwa kasi ile ile.
    Kuna Highway nyingi tu ambazo hazipo kwa kiwango cha express way na ndo highway zetu za tanzania.

    Kujenga flyover kwa sasa ni ndoto za mchana kwani hela kama tunazo bora tuongeze barabara nyingine zinazokosekana. Tusifikiri haraka kuhusu kujenga barabara zinazopishana kwa madaraja wakati tunajua wazi gharaza za kujenga daraja moja ni sawa na kutengeneza barabara mpya zaidi ya tano za urefu wa km 10.
    Tujenge hoja kwa misingi ya kiuchumi ndo upembuzi yakinifu

    ReplyDelete
  6. Mjumbe mawazo yako ni mazuri lakini matuta sio lazima.Mfano Manzese na sehemu nyingine zenye msongamano wa watu wangeweka Fence kuhakikisha hakuna mtu ambaya anaingilia barabara kubwa hiyo ikiwa ni pamoja na wanyama n.k

    Kwani ripoti za polisi zinaonyesha kwamba watu ado wanagongwa japo kuna matuta.Mfano mikumi kuna matuta mengi tu lakini bado wanyama wanagongwa .

    Njia sahihi ni kuhakikisha kuna sheria kali kuhusu madereva na waenda kwa miguu hii nikiimaanisha Fine au kunyanganywa leseni kama unasababisha ajali kwa makusudi au kwa uzembe.

    Mjusi

    ReplyDelete
  7. hivi haya MATUTA barabarani ni sheria/kanuni ya wapi?maana hapana kwakweli

    njooni mwanza muone vituko tuta usawa wa wimbi la baharini (mabatini/nyakato)adi gari linagonga kwakweli,arusha sasa ndo kituko kingine

    nielimishwe

    ReplyDelete
  8. likiwezekana hili kweli ndo tutakuwa na viongozi dhabiti na wa maana,kuanzia rais adi mkoani

    watu kazi per diems tuuu

    ReplyDelete
  9. Kwa kifupi wote wa hapo juu hamna mtaalam wa barabara ila ni watu waliokaa majuu wanajaribu kutoa hoja, Kuna mambo mengi sana ya kiuhandisi katika kuboresha traffic flow bila kuwa na hizo bottle necks.

    Jambo la kushangaza hamna aliyesema kuhusu traffic lights junctions ambako kila siku zinakuwa na polisi, huu ni upuuzi na ni moja ya sababu kubwa ya traffic bottle necks.

    Traffic lights huwa zina kuwa programmed kiasi kuwa ukitoka junction moja hadi nyingine mara nyingi husimami (ka kizungu synchronisation) sasa wewe afande ataweza wapi kusychronise huku anaangalia rushwa itatoka wapi!!!upuuzi mtupu...umona wapi nchi zilizoendelea kuna trafiki.... tengeneza kwanza taa za trafiki zifanye kazi kama zilivyokusudiwa, pili kuna kitu kinaitwa traffic count, nne unaweka kwenye simulation program inakwambia pengine uongeze lane, au u reprogrammtraffic lights to have smooth flow au weka fly overs na inakupa scenario katika mida mbali mbali, ndio baadae unafanya maamuzi.

    Kwa kifupi utaalamu wa kiuhandisi hamna zipo siasa na trafiki polisi...kazi kwenu..wahandisi wa tanroads mpo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...