Home
Unlabelled
JK akabidhiwa ripoti ya ukaguzi na matumizi ya serikali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
CAG Kila mwaka anakabidhi riport kama hizi, ila mbona hakuna mabadiliko?. Au report ni kubwa sana kuimaliza kuisoma kwa mwaka mmoja? kabla haijaisha ingine imefika Duh! Kazi kweli!
ReplyDeletesasa hapo wote wachagga....walipendelewa au merits
ReplyDeleteKwa maoni yangu suala sio kupendelewa. lakini upo uwezekana kuwa wamependelewa ndio maana hata wewe umeuliza hilo swali la kizushi. Kwani mbona wapo wasomi wengi tu ndugu yangu acha ushamba! unaonekana ni limbukeni wa kazi za serikali, watu wamesoma na wanafanya kazi zao wenyewe... Amka Bwenge wewe!!
ReplyDeleteAnon, Mar 31,09:10Pm
ReplyDeleteUmeniacha hoi, kinachofanyika ni kusoma utangulizi na walioshiriki kuandaa ripoti kwisha.Inasubiriwa ingine mwaka ujao
Mdau
Jeetu Patel aomba kesi yake ya Epa isitishwe kusikilizwa
ReplyDeleteUpande wa utetezi katika kesi ya wizi wa Sh. bilioni 3.9 za Benki Kuu Tanzania (BoT) katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa), inayomkabili Jayantkumar na wenzake, umeiomba mahakama kusitisha kusikiliza kesi hiyo hadi kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na washtakiwa itakapomalizika.
Aidha, washtakiwa hao walifungua kesi ya kikatiba yenye namba 30, ya mwaka jana wakiiomba mahakama kuwafutia kesi hiyo baada ya kuandikwa katika vyombo vya habari na kuitwa mafisadi.
Maombi hayo yalitolewa jana mbele ya jopo la mahakimu, wakiongozwa na Ignas Kitusi, John Mgeta.
Wakili wa utetezi, Martin Matunda, alidai kuwa washtakiwa walifungua kesi ya kikatiba pamoja na maombi ya kufutiwa kesi hiyo, lakini Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, alirejesha shauri hilo Mahakama ya Kisutu.
Aidha, Jaji Mfawidhi aliagiza maombi ya kusitisha kusikiliza kesi yafanyike kwenye Mahakama ya Kisutu huku kesi ya kikatiba ikisubiri kusikilizwa na kutolewa maamuzi.
Hata hivyo, upande wa mashitaka uliomba muda wa siku moja kupitia nyaraka za kujibu pingamizi la utetezi ambapo watatoa hoja zao kesho.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi kesho itakapoendelea kusikilizwa.
Mbali na Jeetu Patel, washtakiwa wengine ni Devendra Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kughushi, kuwasilisha hati za kughushi, wizi na kujipatia ingizo za fedha katika akaunti zao Sh.3,924,992,009.25 kwa kutumia kampuni ya Bina Resorts ya Tanzania baada ya kudanganya kuwa imehamishiwa deni na Kampuni ya C. Itoh &Company Ltd ya Japan.
CHANZO: NIPASHE
hivi hiyo ripoti ni yakufanyiwa kazi au ni zawadi...maana naona imefungwa kwenye gift paper kabisa...wabongo bwana..taaabu kweli kweli...yaani haya ni mambo ya aibu tu...bwana michuzi plz toa hii picha..haya mambo mengine ya aibu hivi tuyaache bongo kwetu tu..maana sielewi hiyo gift wrap inafanya nini kwenye such a serious report?
ReplyDeleteMAZINGAOMBWE YANAENDELEA..NEXT PLEASE!...HALAFU NA HUYO ASYEEELEWA MWINGINE ANAULIZA KAMA NI WACHAGA ILI IWEJE?KWAMBA WANA AKILI SANA? AU KWA VILE WAMEPELEKA RIPOTI KWA JK BASI NDIO NONGWA,UZUSHI MTUPU HAPO,MAZINGAOMBWE TU HAPO UNAWEKA KITAMBAA ANATOKA NJIWA TUENDELEE TUSIENDELEE PROFESA MATATA,ALITOA TOOOOAAAAA
ReplyDeleteMZAZI CHOPANGA
anon,march31,09:10PM.
ReplyDeleteunaishi nchi gani wewe?mijitu kama wewe ndo haitakiwi kwenye jamii .choka mbaya tu wewe.
anon wa Wed Mar 31, 09:10:00 PM naona unaongea mambo ya kupendelewa kama ukitaka kuelewa cheki CV zao kama hujazimia.Watu wameenda shule we utabaki ukiongea mambo ya upendeleo.
ReplyDeletekumbe makabidhiano ya ripoti hizi yanahitaki mbwembwe za ribbon ties? mimi nilifikiri ni sehemu ya kazi za mtu za kawaida ambazo hazimuhitaji mpiga picha.
ReplyDeleteAnon Mar 31, 09:10 PM asishambuliwe yupo sawa kabisa.
ReplyDeleteMdau ana haki ya kuhoji. Kwa nini baadhi ya watu hawataki issue kama hizi ziguswe. Ukweli ni kwamba kuna watu walishaweka mtandao wa kujinufaisha wao kwa wao.
Kama walio wengi hawalioni hilo leo basi wataliona kesho, ukweli waja.
Nawasilisha.
we michuzi ng'ombe wahed!! umebana meseji yangu ili iweje? narudia tena huyo jamaa suruali imejikunja kama imeliwa na ng'ombe aibu sana
ReplyDeleteukiona vyaelea vimeundwa na dua la kuku alimpati mwewe ukiona mwezio yuko atua tano mbele kuna kitu anafanya cha ziada ambacho wewe ufanyi sasa nenda kajifunze kwake kuanza majungu na vitisho sio suluhu in short know yourself accept yourself and better yourself na ujue mambo mazuri yanataka kusota kwanza wako ngazi kwa ngazi utafika sasa ukifika ukigeuka pembeni unamuona wa karibu yako ehe vp na wewe ni dar es salaaam manake itafika kipindi itakuwa sio ukabila watoto wa mjini mbona wako wengi wanapendelewa kila kitu kiko dar
ReplyDelete