John Mnyika

Natangaza rasmi dhamira ya kugombea ubunge 2010
Ni wakati wa mabadiliko ya kweli; tuwajibike

Utangulizi

Wapendwa wananchi wezangu na marafiki zangu ndani na nje ya jimbo la Ubungo. Ninayofuraha kuwatangazia rasmi dhamira yangu ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Nimefikia uamuzi huu baada ya kusikia maoni ya wengi wenu na kuisikiliza pia nafsi yangu katika kipindi cha kuanzia mwishoni mwa mwaka 2009 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2010.

Wakati wa kampeni bado, hivyo sitazungumzia kwa sasa ahadi zangu kwenu wala ilani ya chama; lakini inatosha kuwaambia tu kwamba: ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike. Naamini katika kuwa na uongozi bora wenye dira na uadilifu wa kuwezesha uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za umma ikiwemo kodi zetu na mali asili za nchi yetu kwa ajili ya kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote.

Kuusoma ujumbe wote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ukiwa mwanasiasa unawafanya watu wote watoto wadongo. Umesema moja ya misingi ya ubunge ni kuisimamia na kuiwajibisha serikali na viongozi wake. Sasa kwa mfano CHADEMA ikashinda uchaguzi na wewe ukachangulia kuwa mmoja wa viongozi wa serikali sasa utaiwajibisha vipi hiyo serikali na viongozi wake? Wewe omba tu kula na sisi tutaamua kama tukupe au tukunyime acha porojo. Mwanakijiji kaa mkao wa kula nitarudi hivi karibuni.

    ReplyDelete
  2. Nanukuu sehemu ya hotuba ya Mnyika
    1. Mwaka 2005 Mwezi Machi kama huu nilipochukua fomu kwa mara ya kwanza kugombea ubunge, CHADEMA haikuwa na mtandao imara katika jimbo la Ubungo tofauti na sasa ambapo ina mtandao madhubuti na ipo fursa bado ya kuufanya kuwa mzuri zaidi. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.

    Hivyo Disemba 2005 (pamoja na kukubalika kwa wananchi) baada ya mvutano wa siku kadhaa matokeo ya uchaguzi yalitangazwa kwa shuruti bila kupitia utaratibu wa kupitia na kujumlisha kituo hadi kituo na kufanya jumla ya wapiga kura waliotangazwa kupiga kura katika ubunge kuzidi wale waliopiga kura za urais kwa zaidi ya kura elfu thelathini (30,000) katika uchaguzi uliofanyika katika siku moja.

    Kutokana na hujuma hizo na nyinginezo zilizohusisha pia ufisadi katika uchaguzi niliamua kufungua kesi namba moja ya mwaka 2006 katika Mahakama Kuu kupinga matokeo hayo. Kesi ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikipigwa danadana za kiufundi bila kuingia katika kusikiliza msingi wenyewe wa kesi.

    Wakati najiandaa kutangaza rasmi dhamira ya kugombea nikitazama mbele kwa matumaini, nimepokea simu toka kwa Wakili wangu katika kesi hiyo Ndugu Tundu Lissu akinieleza kwamba hatimaye Mahakama Kuu imepanga kuwa kesho tarehe 22 Machi 2010 ndio siku ambayo mahakama itatoa hukumu juu ya kesi hiyo.

    2. Naweza nikalazimika kutangaza upande wa kugombea

    Tunahitaji mabadiliko ya uongozi na mfumo wa utawala ili kutumia vizuri kodi za wananchi na rasilimali za taifa kuwa na miundo mbinu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kuwezesha ustawi wa wananchi.

    Badala ya kuelekeza nguvu zaidi katika azma hii, serikali ya sasa inaongeza nguvu katika matumizi ya anasa na mzigo mkubwa wa gharama za utawala na sasa inajadili kuongeza zaidi idadi ya wabunge.

    Mathalani mwaka wa fedha 2009/2010 kiasi cha bajeti kilichotengwa kwa ajili ya Bunge ni shilingi bilioni 62 ambayo ni sawa na wastani wa zaidi ya milioni 190 kwa kila mbunge kwa mwaka. (Pato la mtumishi wa umma wa kima cha chini halifiki hata asilimia 1% ya fedha hizo).

    Ndio maana binafsi siungi mkono ongezeko la majimbo lisiloangalia tija na ufanisi wa wabunge katika kutimiza majukumu ya msingi ya kibunge. Kwa mtizamo wangu, tunapaswa kupunguza idadi ya majimbo ya uchaguzi badala ya kuyaongeza kwa kufanya wilaya za sasa za kiutawala ndio ziwe kitovu cha mgawanyo wa majimbo.

    Mathalani, wilaya ya Kinondoni badala ya kuwa na majimbo matatu ya Kawe, Kinondoni na Ubungo iwe na jimbo ni jimbo moja tu la Kinondoni. Badala yake Halmashauri ya Kinondoni bila kushirikisha vyama vya siasa ilipeleka mapendekezo kwa Baraza la Mashauriano la Mkoa (RCC) wa Dar es saaalam ambalo nalo limepeleka mapendekezo ya kugawa majimbo kadhaa ya mkoa huu likiwemo jimbo la Ubungo.

    Kwa mujibu wa mapendekezo yao Kata za Kimara, Makuburi, Mbezi na Kibamba zimependekezwa kuwa kwenye jimbo la Kibamba toka Jimbo la sasa la Ubungo. Kwa msingi huo wanapendekeza sasa jimbo la Ubungo libaki na kata za Mabibo, Manzese, Makurumla, Ubungo, Sinza na Mburahati na kuongezewa pia kata ya Kigogo (ambayo kwa sasa iko ndani ya Jimbo la Kinondoni).

    Kwa hiyo, pamoja na kutangaza dhamira yangu ya kugombea ubunge katika eneo ambalo ni Jimbo la Ubungo; haiwezekani kwa sasa kutangaza kwa hakika nitagombea katika jimbo gani mpaka pale Tume ya Uchaguzi itakapotangaza maamuzi yake kuhusu mgawanyo wa majimbo baada ya kupokea mapendekezo hayo toka kwa serikali. Iwapo Tume ya uchaguzi italigawa jimbo la Ubungo nitalazika kutangaza upande ambao nitagombea. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike.

    Hitimisho, mnyika tunakukubali sana ila uweke ulinzi sana wakati wa kuhesabu kula, nakumbuka sana yaliyotokea mwaka 2005.
    Kila la kheri kaka, tupo pamoja.
    Mdau Kimara

    ReplyDelete
  3. Pat-MagazetiMarch 22, 2010

    Swali kwa chadema,

    Kama leo wakishinda uchanguzi:

    Nani atakuwa waziri mkuu?
    Nani atakuwa makamu wa rais?
    Nani atakuwa waziri wa fedha?
    Nani atakuwa waziri wa ulinzi?
    Nani atakuwa waziri wa mambo na nje?
    Nani atakuwa waziri wa mambo ya ndani?
    Nani atakuwa mwanasheria mkuu?
    Nani atakuwa waziri wa sheria?

    Kuuongoza nchi siyo kazi rahisi. Chadema kwanza kuwa na "shadow minister" sasa watu wakiona viongozi wenu wanaongelea wizara zao sasa watu wanaweza kufikiria kama kunauwezo wa kuongoza nchi. Kama cha tawala yamewashinda kwa kweli tutaweza?

    ReplyDelete
  4. We mdau ju kwanza unaonekana roo yako mbaya na upeo wako ni mdogo na vile vile ujuwi taifa rako wapi linapo kwenda sisemi ni razima umpigie kura uyu jamaa au ujiunge na chadema au cuf au upinzani ila ccm pia wapo watu wenye uchungu na taifa unapo tuma ujumbe kaa na kufikilia sio kuongea tu kama mtu alie shikwa na tumbo la kualisha au we unawezekana ni familia ya mbunge wa sasa wa jimbo analotaka kugombea nini ? kama ni hivyo msulie uko uko jimboni kwenu alafu umuulize maswali yako sisi wenzako tunaipenda nchi yetu au wewe ni mtu mzima [mzee] atukwambii ujiunge na wapinzani ila kuwa na uchungu na taifa rako ambalo lina angamia na alijulikani linapo kwenda na kina mama na watoto wa angamia kw sababu ya watu wa chache

    ReplyDelete
  5. ujumbe mfupi wa chadema tumieni YES WE CAN ya Obama haki mutashinda uchaguzi, nendeni kwenye vyuo vikubwa kwa makempeni

    ReplyDelete
  6. yaliyomo yamo.March 22, 2010

    tatizo vyama vya upinzani hamdili na issues, mnawalaumu tu kina lowasa, rostam, na wengine. ndio maana mnashindwa.

    hebu jaribuni ku-address mambo kama umeme, foleni barabarani, afya, pato la mtanzania, mshahara, uanzishaji wa makazi bora, eeh.

    tutawapa kura.

    ReplyDelete
  7. chadema kupata unungo sahauni,chadema hamna uwezo wa kuchukua jimbo lolote dar,atlit cuf kidogo hujipapatua.dar si mchezo,mji wa wajanja huu.hadanganywi mtu na helkopta

    ReplyDelete
  8. hatuwapi division zero ubunge,sahau.

    ReplyDelete
  9. dogo tafuta kazi ya kufanya,siasa itakuchokesha kabla ya mda wako,mwenzako mbowe karithi chama kwa baba mkwe.ohoo

    ReplyDelete
  10. Ni jambo linalosthili kuwa ndani ya fahamu za kila mdau kuwa siasa siyo uwanja wa kila mtu na siyo lazima uwe mwanasiasa ndiyo uweze kuitumikia jamii yako.Sasa kila mtu anataka ubunge sina hakika hili jambo linawezekana.

    ReplyDelete
  11. Mwanyika nakuonea huruma sana ulivyojipa kilema cha mdomo wakati wa kuongea kisa kumuiga Mbowe na Mh. Zitto tatizo lako ni nini? Kama umeiga mavazi si yanatosha mdomo kuubenyua benyua unaharibu sura yako tafuta muonekano wako ukiwa unatetea hoja yako. Mimi huwa sipendi kabisa unavyoiga wenzio... be you!

    ReplyDelete
  12. Inasikitisha sana kuona ndugu zangu mna upeo wa chini kiasi hiki. Kijana Mnyika anapaswa kupongezwa kwa hatua hii aliyoichukua na si kupakaziwa mambo ambayo hata hajafanya.

    Kwa mtu yeyote mwenye fikra za kimaendeleo atakubaliana na mimi kuwa ili nchi iendelee tunahitaji kuwa na upinzani wenye nguvu, lakini upinzani huo hauwezi kupata nguvu kama vijana wenye upeo wanapojitokeza, wanaishia kubezwa kama baadhi ya wanandugu wanavyofanya sasa kwa Mnyika. Kama kuna mtu anamjua vizuri Mnyika atakubaliana na mimi kuwa huyu kijana ni mtu makini mwenye uwezo wa kufanya makubwa kama atapewa hiyo ridhaa. Hamna aliyekuwa anajua uwezo wa Zitto mpaka alipoingia bungeni akaanza kuonesha cheche zake. Tusubirie kampeni, tusikie atatuambia nini.

    Sina maana kuwa Chadema au wapinzani ni wazuri sana na CCM hakuna watu wenye lengo sahihi na nchi, lakini kuna haja ya CCM kupata changamoto ya kutosha ili hata kama watashinda wawe makini zaidi katikia uongozi kwani watajua kuwa kitumbua chao kipo hatiani.

    Ni wakati sasa tunapaswa kuacha ushabiki wa vyama na kuchagua watu wanaofaa kutuletea maendeleo. na zaidi kama kuna vijana walio makini wether ni katika upinzani au CCM wanapaswa kupewa support. Nadhani mmeshuhudia hata ndani ya CCM vijana walivoleta changamoto nzuri.

    Naomba kuwakilisha
    Mdau,
    UDSM.

    ReplyDelete
  13. Wewe anon hapo juu uliyezungumzia division ziro naona muosha kinywa tuu sababu hujui unachozungumza. Mnyika ni kichwa huyo dogo angalia what he did back in days

    ReplyDelete
  14. mdogo wangu dar huwezi shinda,nakushauri tafuta kwengine,atlist zito kidogo angetingisha lakini si wewe.

    ReplyDelete
  15. miji mikubwa yote familia nyingi zinaitegemea ccm kwa upande mmoja au mwingine,kuanzia makatibu kata hadi mabalozi wa nyumba kumi,bado wafanyakazi wa ofisi za ccm,ni ngumu kwa chama cha upinzani kisicho na mshahara kuweza kuwashawishi hawa wanaopata japo 500 kwa siku kupitia ccm.nchi yetu masikini sana,kiasi hata raia hawafikiri future,wanataka ya leo leo,so ukija na ahadi bila kitu ni ngumu kupita

    ReplyDelete
  16. watu wanaogopa mabadiliko au michuzi amebana comment? halafu hawa wanaoponda hapa ndio wa kwanza kulalama juu ya serikali. bongo maendeleo ni ndoto ngoja tu niendelee kupiga box langu kwa mtindo huu najilipua wakati wowote siwezi kuishi nchi ya wapofu

    ReplyDelete
  17. Asanteni sana kwa maoni yangu; yote kwa ujumla wake, chanya na hasi. Nawatakia mjadala mwema. Ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike

    ReplyDelete
  18. aliyebuni magwanda yenu hajui GIOTO,maana si joto la dar,haya mambo ya kujifanya kina che guevara mtaiva na hayo magwanda,hivi mnayo mangapi mangapi,maana kama ni kauka ni kuvae sharti uanike nyuma ya friji! na mnaoga mara ngapi kwenye kampeni,GIOTO la dar na hilo MARADUFU!
    MZAZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...