KAKA MICHUZI POLE NA MAJUKUMU NA HONGERA KWA KAZI NZURI UNAYOIFANYA ,MMI HUWA NI MPENZI SANA WA BLOG YA JAMII TATIZO NILIKUWA SIFAHAMU UKITAKA KUTUMA HABARI UNAFANYAJE ILA LEO NIMEINGIA ASUBUHI NIKAONA ANUANI YA EMAIL JINSI YA KUTUMA.
NAOMBA KUWATAHADHARISHA WADAU; JANA NIMEWEKA SHELI MAFUTA YA SH 10,000/= SAA 12 JIONI, HIYO SHELI IKO MTAA WA AZIKIWE KAMA UNAELEKEA MWENGE MAENEO YA POSTA MPYA.
JAMANI CHA KUSHANGAZA LEO ASUBUHI NAENDA KAZINI MSHALE UNAONYESHA UMESHUKA KABISA IKABIDI NIPITE SHELI TENA KUONGEZA MAFUTA KIDOGO MSHALE UKANYENYUKA SASA WADAU TUTAFIKA???????????????
NISAIDIENI MDAU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. MDAU TUNAONA UNAANZA KULALAMA BILA KUELEZA MAFUTA YAMEISHAJE! KWANI ULITEMBEA KILOMETA NGAPI? UNA GARI GANI? ULIKAA FOLENI MUDA GANI? HIVYO NDIVYO VIGEZO VINAWEZA TUNYESHA KUWA UMETUMIA MAFUTA KIASI GANI. NINYI NDIO WATU MNAOSEMA "NIKIWEKA MAFUTA YA 30,000/- NAKAA NAYO WIKI NZIMA" SWALI LINAKUJA SASA KAMA UKIENDA MOROGORO NA KURUDI NDANI YA MASAA MANNE (SIO WIKI MBILI) UTAFIKA? MAFUTA YANATUMIKA KWA UMBALI UNAOENDESHA , KWENYE FOLENI,UKUBWA WA ENGINE, UCHAKAVU WA GARI NA AINA YA UENDESHAJI, NK.
    BADO HUNA USHAWISHI KWANGU KUWA UMEPUNJWA, FAFANUA VIZURI KWANZA.


    MZOZAJI

    ReplyDelete
  2. kaka jaribu kuwa more specific na si kukurupuka 2, hujaeeleza umetoka posta kuelekea wapi unapokaa, isitoshe mafuta ya sh 10000 ni madogo sana kama unatumia petroli ni lita zisizozidi 6 na que ya magari huchangia mafuta kutumika zaidi coz gear inayotumia ni kubwa yaani moja na mbili

    ReplyDelete
  3. wauza mafuta wezi sana hao sana hao mimi huwa naendaga na kidumu changu cha mafuta nikifika naweka then naondoka zangu.pole sana bongo kweli tambarare.
    mdau UK.

    ReplyDelete
  4. mi naendaga na kidumu.
    mdau ukerewe!!!!

    ReplyDelete
  5. Kaka gari si yako hiyo, mshale wa mafuta unaangaliwa asubuhi baada ya kutumia! Ungesema baada ya kuweka mafuta mshale haukuinuka angalau ungeeleweka na pia hujatwambia ulitembea umbali kiasi gani? Hata hivyo mafuta ya shilingi elfu 10 si issue ya kutafuta maoni kwenye blog, haijatulia hiyo, lete kisa kingine.

    ReplyDelete
  6. Wadau waliotangulia wametoa maelezo ya kutosha, Shs 10,000 ni kidogo sana kama lita 6 au 7 tu sasa wewe ulitaka uyatumie kwa muda gani? Kama unaweka mafuta ya kiasi hicho wewe nadhani hutakiwi kuendesha gari, hiyo ni bajeti ya pikipiki au bajaj!!!!

    ReplyDelete
  7. Hayo mambo mengi sana hapa mjini. Mimi nafanya kama mdau wa Ukerewe hapo juu. Naenda na kidumu cha lita tano ambacho nimechora mstali kuonyesha pale lita tano zinapoishia. Lazima wajaze mpaka kwenye mstali.

    Huniibia kirahisi ndugu yangu, nilishachoka.

    ReplyDelete
  8. pale ndo zao pamoja na ile sheli ya pale kinondoni mwanamboka looo wanakwiba sana tuu nyingine iko kulee shekilango na pale sea view zinafahamika kwa uchori we unadhani kwa nini wakati wa kujaza mafuta watu wengine huwa wanashuka kuhakikisha kama kweli jamaa anakamua viinginevyo ni changa la macho tu! au unatakiwa uangalie ile mita yenye namba jinsi inavyosoma wakati anakamua vinginevyo kama uko bize na kiselula unaliwa laivu

    ReplyDelete
  9. Na we Michuzi bwana uwe unawaambia watu wa post habari kamilifu... asema kama ana bajaj tujue.. kha! Sasa utasababishwa watu watukanwe bure humu

    ReplyDelete
  10. kama gari yako ni navigator au escalade lazima yaishe

    ReplyDelete
  11. Kuna wataalamu wa idara inaitwa 'Weights and Measures' wanajiita Industrial Metrologists wanatakiwa kufuatilia hili kujua kama wese lako lililiwa na foleni au vipimo feki. Najua wanatembelea globu ya jamii, kazi kwenu kufuatilia na kurudisha mlishonyuma.

    ReplyDelete
  12. HAPO UMEKURUPUKA,HAUJAIBIWA BALI INATEGEMEA NA AINA YA GARI LAKO.
    KUNA MAGARI AMBAYO HATA GAUGE YA MAFUTA IKIFIKA CHINI MAFUTA BADO YANAKUWEPO.
    NAMAANISHA HIZO GARI ZINAHIFADHI KIASI FULANI CHA MAFUTA KABLA YA GAUGE KUANZA KUSOMA.
    KAMA GARI LIMETUMIA MAFUTA MENGI KARIBIA KWISHA UKIWEKA MAFUTA YA 10000 GAUGE INAPANDA KIDOGO SANA NA UKITEMBEA KM KADHAA INASHUKA(GARI YANGU ILIISHIWA MAFUTA NIKAJAZA LITA 6 KWA VIDUMU KWA HIYO NINACHOONGEA NI CHA KWELI).HUJAIBIWA BALI KILICHOKUTOKEA WEWE NI HICHO NILICHOKISEMA.
    JIFUNZE HILI USITAKE KUHARIBU BIASHARA YA T..PETROL STATION

    ReplyDelete
  13. Mdau atakaekusaidiaMarch 19, 2010

    Jamani msiwalaumuwauza mafuta kwa ujinga wenu wa sintofahamu ilikuwaje sio kila tatizo una lalamika japo michezo iko ya kuwekewa hewa badala ya mafuta,eleza mafuta ya elfu kumi uliystumiaje?ulikumbuka kuwa wewe bahili unapokuwa kwenye foleni uzime injini
    MM NAUZA MAFUTA KILA KUKICHA NACHUKIZWA NA WENZETU WANAOWAJAZIENI HEWA,,WEKA ANUANI YAKO NIKUSAIDIE KAMA KWELI KUNA USHAHIDI MM NDUGU WA MUHISIKA WA HIYO SHELI KAMA KUNAMFANYAKAZI ALIFANYA HIVYO KUMBUKA MUDA NA TAR

    ReplyDelete
  14. Jaman naungana na huyo mdau wa Fri Mar 19, 04:56:00 PM kweli pale kinondoni mwanamboka wanaiba ile kiroho mbaya,mim ninatabia ya kuongeza mafuta kila geji inapofikia kiwango fulani na nimeshaizoea gar yangu, nilishawah kwenda pale nikaweka mafuta ya shilling 20,000/= nakuambia geji haikujigusa nilishindwa namna ya kufanya manake nilipomwuliza alinijibu akaniambia labda geji yangu mbovu nilichoka.Na pale ukienda na kidumu wanachukia sana,lakin nasikia hawa jamaa matajir zao wanawakabiz lita kazaa za mafuta wanawaambia tunataka hesabu kiwango fulani sasa ni juu yao kuchacharika ili waweze kupata kiwango cha ziada na wajikwamue na umaaskin,moja ya mbinu ambayo wanatumiaga ni kuwa wakati wakikuekea mafuta wanapress pump wakati mafuta yakianza kuflow wanaachia gafla kuzuga kama wanaweka sawasawa mdomo wa pump ukiona hivyo ujue imekula kwako manake akifanya hivyo anaruhusu upepo kuingia sasa akipress mara ya pili geji ya pump itaanza kusoma bila mafuta yoyote kuingia mpaka ule upepo uishe,kuna swali ambalo linaulizwaga na watu wengi sana na mpaka sasa jibu halijapatikana kwa nini hiz pipes za mafuta wasiweke ambazo ni transparency mteja uweze kuona mafuta yakiflow in?.Halaf hawa jamaa kwa mchezo wao huo mchafu wanapata fweza bwana,kuna baadhi ya mafuel attendants ambao nawafahamu wanamajumba ya kutisha ukiyaona utafikiri ni ya mafisadi wa EPA.

    ReplyDelete
  15. Nadhani wewe ni mshamba sana, mafuta ya elfu 10 ndio unageuza mada hapa kwenye blog tukufu. Ankal mada kama hizi uwe unazimwaga tu, zinatupotezea wakati wa kuzijadili. Mafuta ya elfu 10 ni lita km 6 tu, sasa unadhani gari ni bajaji, usione magari mengi mjini hapa, kuyaweka barabarani sio kazi nyepesi.

    ReplyDelete
  16. unauhakika gani kama tank halijatoboka? au kuna pipe inavujisha?

    ReplyDelete
  17. UNAENDESHA NA GIA NAMBA MOJA KWENYE FOLENI, NDO MAANA MAFUTA YAISHA, SINA UHAKIKA KAMA GIA NAMBA MOJA INAFAA KUENDESHEA KWENYE FOLENI LABDA KARI CHAKAVU

    ReplyDelete
  18. MDAU ACHA UJINGA ULIFIKIRI MAFUTA YA SH 10,000 UTAKAA NAYO MWAKA? UNADHANI MWENYE SHELI ATAKUIBIA WEWE MLALA HOI KWANZA HATA KUWEKA FULL TANK HUMUDU? AU NA WEWE UMESHAJUWA SASA KUTUMA MASSEGE NDIYO IMEKUWA TABU? NI BORA UNGEKAA VILE BILA KUJUWA KWANI UNACHOLEZA NI UTUMBO MTUPU.

    ReplyDelete
  19. WEWE INAONESHA WAKATI UMELALA VIBINGWA WAMECHUKUWA GARI KUTAFUTA VIMWANA HAHAHAHA AU KAMA WANAVYOSEMA UMEIPELEKA UMBALI GANI? USIBANIE PESA WEKA MAFUTAAAAAAAAAAAA.

    ReplyDelete
  20. kwanza tanzania siku hizi hatuna shell (kampuni)
    sema kituo chamafuta gas station au petrol station alafu
    mafuta ya elfu kumi ni less than 10 ltrs sasa ulitaka mshale uwejuu hiyo ni bajaj>>>???? na ulitembea umbali wa wapi kwa speed gani na mengineo meeengi ni yakujiuliza

    ReplyDelete
  21. kaeni kushoto nyinyi mnamrusia madongo mwenzenu ili iweje ovyo sana kama haijakukuta vile hukai bongo au hujaonja joto ya jiwe na sio mjisheue kuwa mna fweza za kutisha mkute na nyinyi mnaweka ya elfu tano nyambafff!! elfu kumi ndo uwezo wake hayo mafuta yanakufikisha popote dar hata kama uko kwenye foleni nzito nikweli wajaza mafuta bongo ni wezi wazuri sanaaaa ilishanitokea nikarudi kwa kishindo wakaongeza manake walijua wameniliza hivyo mkome kutoa kashfa zenu wengine hamjawahi kumiliki hata mikokoteni kazi kutoa maneno ya kashfa tuu kila mtu akitoa ishu yake humu ndani watu wazima ovyooo hamkui??????

    ReplyDelete
  22. Nyie wabeba box acheni kumponda huyu jamaa aliyeweka mafuta ya elfu kumi,mbona mimi mara nyingi tu nawekaga mafuta ya elfu kumi na napiga mizunguko ya kutosha tu na wala si sensi kama nimeweka mafuta kidogo,Siku moja nilienda pale shell ya victoria kufanya service gari yangu nikawa nimebuzbuz karibu na pump zao pale kitu nilichogundua zaidi ya asilimia 50 ya magari yote niliyoyashuhudia walikuwa wanaweka mafuta ya elfu 10 na wengine less than that especially madereva taxi wao ndio vichekesho unakuta wanaweka mafuta ya 2000/=,3000/=,3500/= kwa hiyo huyu jamaa aliyeweka mafuta ya elfu kumi mbona amejipinda sana ukikompea na hao.Mwacheni kabisa mim sijawahi kuweka full tank kama madaladala labda niende mkoani lakini misele ya mijini niweke full tank no please ni hizohizo elfu 10 tu tutaendelea nazo.

    ReplyDelete
  23. KATIKA GARI UKIONA GEJI IKO MINIMUM UJUE MAFUTA YAMEISHA NA SASA UNAANZA KUTUMIA RESERVE NA MARA NYINGI RESERVE FUEL INACHUKUAGA ABOUT 7LTS INADEPEND NA AINA YA GARI,SASA HUYU JAMAA WA ELFU KUMI INAELEKEA ALITUMIA MPAKA RESERVE NA UKITUMIA MPAKA RESERVE UKIJA KUWEKA MAFUTA YANATAKIWA YAJAE KWENYE RESERVE KWANZA BAADA YA HAPO MSHALE WA GEJI NDIO UANZE KUPANDA KWENYE MINIMUM,SASA INAWEZEKANA HUYU MDAU WA ELFU 10 ALITUMIA MAFUTA YOTE AKAENDA SHELL NA ELFU 10 AKIJUA RESERVE ITAJAA NA MSHALE UPANDE NI NDOTO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...