ankal anaipenda sana sehemu hii ya filamu ya charlie chaplin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kama ilikuwa wakati wa njaa, basi jamaa alijitahidi kubuni namna ya kujipatia chochote kuepuka kufa njaa. Swali ni kwamba hivi kweli ngozi ya kiatu inaweza kutafunwa na kulainika?

    ReplyDelete
  2. Ukiona documentary ya maisha yake utampenda zaidi kwa sababu inakuelewesha kwa nini Charlie Chaplin aliuchukia sana ubepari.

    Je Charlie alikuwa comedian?

    ReplyDelete
  3. Charlie Chaplin alikuwa Comedian. Lakini mara nyingi sinema zake zilikuwa na ujumbe za kisiasa jambo ambayo ilifanya awe blacklisted na ilibidi akimbilie kukaa Ulaya. Someni habari ya McCarthyism mtaelewa zaidi. Mtu ukiwa na njaa utakula kitu chochote. Enzi za Depression miaka ya 1930's nasikia ilikuwa huoni hata njiwa! Walikuwa wanaliwa na wazungu!

    ReplyDelete
  4. Chemi,

    Wewe ni muigizaji na mimi hali kadhalika. Maigizo tunayagawa sehemu tatu: Tragedy, Comedy na Melodrama. Naomba tuangalie tena sinema za Charlie Chaplin halafu tuchunguze tena tunaweza kuzicategorize katika kundi gani Tragedy, Comedy au Melodrama.

    Sinema za Charlie Chaplin zinachekesha, zinafikirisha, au zinahuzunisha?

    ReplyDelete
  5. Charlie hakukimbilia Ulaya bali alifukuzwa America na kupewa deportation order akiwa ndani ya meli akielekea Ulaya. Alifia Uswizi.

    Alimpandisha zaidi J Edgar Hoover hasira alipomdhihaki mbele ya ya kadamnasi kwenye tafrija. Hoover kwa kutumia mamlaka yake ndiye aliyyemfukuza Charlie toka Marekani.

    Hata kwao Uingereza Charlie alikuwa na matatizo na utawala na ndiyo maana Charlie hakuwahi kutuzwa hadhi na ufalme wa Uingereza.

    Sasa naomba kukuuliza wewe binafsi Chemi je filamu za Charlie Chaplin unaweza kuziweka kundi gani: comedy, melodrama, au tragedy?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...