Na Raymond Mihayo, Maswa
MAHAKAMA ya wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga imemhukumu kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi 600,000 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Haki na Ustawi Tanzania(CHAUSTA)Tanzania Bara,Slyvester Kasulumbayi baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kuua kwa maneno Katibu tawala wa wilaya ya Maswa,Antony Masili..
Akisoma hukumu hiyo leo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Thomoson Mtani alisema kuwa ameridhishwa bila kuacha shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka dhidi ya mshitakiwa huyo.
Hukumu hiyo iliyosomwa takribani masaa matatu huku mahakama hiyo ikiwa
imefurika watu mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wilayani humo ilisema kuwa kitendo kilichofanywa na mshitakiwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Ipililo si cha kiungwana ikizingatia kuwa ni kiongozi katika jamii.
Mshitakiwa alipotakiwa na mahakama hiyo kutoa utetezi wake ili apunguziwe
adhabu alisema kuwa anaiachia mahakama kutoa uamuzi wake kwani haoni sababu ya kujijitetea.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Mkaguzi wa polisi,Pili Fobe aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili liwe fundisho kali kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Hata hivyo mshitakiwa huyo alilipa faini hiyo baada ya wananchama wake
pamoja na viongozi wengine wa vyama vya upinzani waliokuwepo mahakamani hapo kuchangishana na kulipa fedha hiyo.
Awali ilidaiwa kuwa Mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 21,2009 majira ya
saa 7.00 mchana katika jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Maswa ambapo
alimweleza Katibu tawala huyo kuwa atamkata kichwa chake mara baada ya
kuwaengua wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa serikali za
mitaa mwaka jana na kukitembeza kwenye sinia katika mitaa yote ya mji wa
Maswa jambo ambalo lilisababisha uvunjifu wa amani kinyume cha sheria.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...