Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akikata Utepe wakati wa Uzinduzi wa Mahakama ya Rufaa (Wa kwanza kushoto) anaeangalia ni Jaji Mkuu Mhe. Augustino Ramdhani. Jengo hili jipya, ambalo limepewa jina la Jaji Mkuu wa Kwanza mzalendo, Hayati Augustine Saidi, lipo nyuma ya Jengo la Mahakama ya Rufaa ambalo zamani lilikuwa Forodhani Hotel jirani na NDC
Mke wa JAJI MKUU WA KWANZA MZALENDO WA MAHAKAMA YA RUFAA HAYATI AUGUSTINE SAID, Mama Elizabeth Said, akiangalia Sanamu ya Mumewe iliyoandaliwa kumkumbuka wakati wa Uzinduzi wa Mahakama ya Rufaa iliyozinduliwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda jijini Dar Jaji Mkuu Mhe. Augustino Ramadhani akizungumza na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kwenye Ofisi ya Mahakama ya Rufaa kabla hajazindua Mahakama hiyo jijini Dar
Jaji Mkuu Msaafu Mhe.Barnabas Samatta (wa kwanza kushoto) na wa pili kushoto ni Jaji Mkuu wa Mahakama Mhe. Augustino Ramadhani wakizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda kwenye Ofisi ya Mahakama ya Rufaa kabla ya uzinduzi wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar
5Wwaziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (Alievaa suti) na Jaji Mkuu( wa kwanza kushoto) Mhe. Augustino Ramadhani na (wa pili kshoto) ni mke wa hayati Augustine Said wakiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mahakama ya Rufaa jijini Dar
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (Wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mke wa hayati Jaji Mkuu wa kwanza wa Mahakama ya Rufaa mhe. Augustine Said Bibi Elizabeth Said wakiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wakuu wastaafu akifuatiwa na Barnabas Samatta (wa tatu kulia) na Lewis Makame( wa pili kulia) na nyuma ni Sanamu ya hayati Augustine Said ,wakati wa Uzinduzi wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar
Mke wa hayati Augustine Said Bibi Elizabeth Said (Wa tatu shoto) pamoja na familia yake na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda leo jijini Dar
Mke wa hayati Augustine Said Bibi Elizabeth Said (Wa kwanza Kushoto) pamoja na familia yake wakisikiliza hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda leo jijini Dar es Salaa.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Prosper muro 2nd row? au huyu mama ni ndugu wa eva?

    ReplyDelete
  2. Sikujua Jaji mkuu wa kwanza alikuwa Augustino Said mimi nilifikiri ni Francis Nyalali. asante kwa kunielimisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...