Mh. Mwandosya akitoa zawadi ya kinyago kwa Waziri wa Madini, Nishati na Utalii wa Australia anaendelea na ziara ya kikazi nchini Australia. akifuatana na Bw. Simon Sayore (Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA) na Bw. Haruna Masebu (Mkurugenzi Mkuu wa EWURA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Prof. M.J. Mwandosya yuko katika ziara ya kikazi nchini New Zealand kuanzia tarehe 12 hadi 17 Machi 2010. Hivi sasa Mheshimiwa Mwandosya anaendelea na ziara ya kikazi nchini Australia. akifuatana na Bw. Simon Sayore (Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA) na Bw. Haruna Masebu (Mkurugenzi Mkuu wa EWURA). Mheshimiwa Mwandosya alilkutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya mawaziri wan nchi hizo.
Akiwa nchini New Zealand, pamoja ma mambo mengine, Mheshimiwa Mwandosya amekutana na kufanya mazungumzo na mawaziri wawili. Tarehe 15 Machi 2010, Mheshimiwa Mwandosya alikutana na Mheshimiwa Dkt. Nick Smith (Mb), Waziri wa Mazingira na Maji. Tarehe 17 Machi 2010, Mheshimiwa Mwandosya alikutana na Mheshimiwa Gerry Brownlee (Mb), Waziri wa Mandeleo ya Uchumi, ambaye pia ana dhamana ya masuala ya nishati na madini.
Akiwa Australia Mh. Mwandosya alianza ziara ya kikazi nchini Australia Machi 18, ambapo pamoja na shughuli nyingine, alikutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Martin Ferguson (Mb), Waziri wa Madini, Nishati na Utalii. Vile vile alipewa heshima ya kuhudhuria kikao cha Bunge la Wawakilishi nchini humo, akiwa kama msikilizaji.
Prof naona anawakilisha wazee wa Vinyago
ReplyDeleteTunataka kila bomba iwe na maji safi mjini Dar!
ReplyDelete