Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja jenerali mstaafu Ligathe Sande kuwa mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Bahari (DMI) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu Mhandisi Omar Chambo imesema kuwa, Ligathe Sande ameteuliwa kwa mara ya tatu baada ya kushika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita iliyopita na kuongeza kuwa uteuzi huo ulianza tangu tarehe 10 februari, mwaka huu.

Wakati huo huo Waziri wa Miundombinu Dkt Shukuru Kawambwa ameteua jumla ya wajumbe sita ambao ni wawakilishi kutoka Serikalini na Asasi mbalimbali kuunda bodi hiyo ya chuo cha Bahari.

Wajumbe hao ni Bi Tumpe Mwaijande mwakilishi kutoka Wizara ya Miundombinu, Bwana David Lwimbo kutoka Ikulu na Meja generali Said Omar kutoka Jeshi la wananchi kikosi cha Wanamaji.

Wengine ni Bi Tumaini Silaa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Bwana Primus Nkwera kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE – National Council for Techinical Education) pamoja na Bi Rukia Shamte kutoka Chama cha Wakala wa Forodha (TFFA – Tanzania Freight Forwaders Association).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Yaani watu wanastaafu bado wanapewa madaraka bado hawajapata tu? wakati vijana kibao wapo hata mvi hawajaota,Hongera company binafsi kwa kuajiri vijana sasa,hii ni aibu.Kuweni kama romania ni nchi inaendelea lakini viongozi wake ni vijana kuanzia 24 years tu

    ReplyDelete
  2. Mume Wangu, Mikanjuni TangaMarch 19, 2010

    Hapa wanawake wamekamata usukani kwa kuwazidi wanaume 4-3. Hongereni.

    ReplyDelete
  3. Kaka Michuzi naomba kuuliza swali la kuelimishwa.
    hivi Tanzania watumishi huwa wanastaafu kweli/ Maana huwa naona mtu akistaafu hapa anateuliwa kuwa mjumbe au mwenyekiti wa Bodi katika Taasisi nyingine ya Umma kama bodi au Ubalozi huko Nje. Yaani mtu analitumikia Taifa hadi anafikisha miaka 60 anastaafu kwa mujibu wa sheria then anaaza kutumikia taasisi nyingine akiwa mstaafu.
    kama sikosei sasa hivi Tanzania ina takribani watu milioni 41. Na vyuo vikuu vyote vya umma na binafsi vinafyatua wahitimu wa fani mbali mbali....sasa lini hawa wahitimu vijana watapata nafasi ya kuongoza au kuchangia taasis hizi. Nilikwenda kule kwa Mzee Kagame siku moja nikakuta government Officials wengi ni vijana..wako katika nafasi za juu sana mfano ukurugenzi, Ukatibu mkuu, nknk. Na hata nchi nyingi za hapa kusini na kaskazini mwa Afrika hilo nimeliona. tatizo ni hapa kwetu tuu. Unajua ukiwa mzee hata upeo wako wa kufikiri unakuwa duni.., huwezi kuwa innovetivu nk. nk Mimi nadhani kazi kama hizi waandaliwe vijana kidogo kidogo...Mtumishi ukistaafu ustaafu kwelikweli uende nyumbani ukale pensheni....Ndiyo maana ya kustaafu,...
    Ni maoni yangu tu

    ReplyDelete
  4. Hiki chuo cha bahari sijawahi kukisikia.

    ReplyDelete
  5. KAMA MUNGU ANAPENDA KILA MTU ATAFANYA KAZI NA MUDA WAKE UTAFIKA ATASTAAFU. MTU AKISTAAFU INABIDI AWAACHIE WENGINE WAFANYE KAZI. HII YA KUNG'ANG'ANIA KAZI NI TATIZO. NDIYO MAANA NCHI HAIENDELEI. MAWAZO MENGI YA VIONGOZI NI YA KIZAMANI SANA NA HAYANA NAFASI KATIKA ULIMWENGU WA SASA.

    ReplyDelete
  6. Kuna mtalaam mmoja alisema kwamba viongozi wengi wa Afrika ni watu wazee sana. Na hii inachangia kutokuwepo kwa maendeleo katika nchi nyingi za Africa.

    Mtu akistaafu kwani nini asiache kabisa shughuli za serikali? Kama akihitajika aitwe kama mshauri sio kuendelea na mawazo yao ya kizamani kuongeza serikali na taasisi zake.


    Vijana wenye elimu, nguvu, na uwezo wa kufanya hizi kazi wapo wengi tu kwa sasa Tanzania, kwa nini wasipewe nafasi kuendesha nchi yao?

    Kwa kawaida umri wa mtu kuishi miaka 70 mpaka 80. Hii ipo mpaka kwenye vitabu vya dini. Sasa mtu akistaafu ana miaka 60.

    Tunategemea kupata nini kutoka kwa huyu mtu kuhusu mipango endelevu? Itakuwa tu nikuendeleza yale yale ya zamani na hata kuaribu vile vichache vizuri vilivyopo.

    ReplyDelete
  7. nyie endeleeni kupeana ulaji tu endeleeni kukamua tu kinchi chenyewe kimeshafulia nyie mnaendelea kukikamua hadi kibaki juu ya mawe huko ni kubebana tuuu huo ndo ukweli halisi ankali meseji hii iruke bila kwakwaru!

    ReplyDelete
  8. Big UP sana kwa Mh. Rais J.K. maana hao ndo wanaofaa nyinyi si mnakumbuka yule aliyewapa STIKI MATEACHER KULE BUKOBA, SASA TUKIPATA KAMA HAWA ISHIRINI HIVI NCHI ITAKUWA SHWARI... ATEUWE MMOJA ATAKAYE WAPA STIK MAWAZIRI WAZEMBE KAMA HUYU ANAYESIMAMIA MIUMEME

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...