Kaka Michuzi,
Nimeona watu wanabisha ile picha ya Addis Ababa, eti ni photoshop, basi wawekee na hii wajionee hawa 'macho ndogo' wa Bangkok walivyotupiga gepu! Hii ni sehemu tu ya barabara za Bangkok zinavyoonekana nyakati za usiku.
Mdau wa Bangkok

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. i have flown over Bangkok a couple of times...and i can testify to this image!! Hao sio wenzetu hata kidogo!!


    mtoto

    ReplyDelete
  2. Hawa watu tulikua nao ngoma dro wakati wa uhuru. We must run jamani.

    ReplyDelete
  3. Michu,

    Longo longo hatutaki hebu mbishi agofye hapa mwenyeweeeeee

    http://nazret.com/blog/index.php?title=ethiopia_construction_of_gotera_intercha&more=1&c=1&tb=1&pb=1


    Wabongo wabishiiiiiiiiiiiiiiiiii !

    ReplyDelete
  4. Ize!! ...tukitoa makamasi kwenye ubongo, tukaweka akili zetu kazini, miaka kumi ni mingi, tunakuwa na mazuri zaidi ya haya!!

    Asiyeamini na ajinyonge!!

    ReplyDelete
  5. Huku bongo hata taa tu barabarani zimetushinda, ni Sam Nujoma tu ndo taa zinafanya kazi na hizo nna wasiwasi 2yrs to come itakuaje. Vigogo kila siku wanaenda nje na kula perdiems tu hawaleti hata kitu kipya wakitoka huko wao ni kula good time tu. Jamani tuweni wazalendo.Nice photo

    ReplyDelete
  6. wenzetu wametuacha mbali sana, ila huwezi linganisha Bangkok na Bongo.. bado sana..tujaribu kulinganisha nchi zingine za kiafrika tena majirani zetu alafu tumtoe huyo pepo mchafu anayekwamisha maeendeleo yetu.. viongozi wetu wanayafumbia macho hayo..kule Kigamboni lingetakiwa lipigwa daraja kali sana...ila siasa sasa...ila labda siku moja vizazi vijavyo ndio wanaweza badili huo mfumo wa Bongo..tuanze na elimu bora kwanza na sio bora elimu.

    ReplyDelete
  7. Mdau hakuna aliyekataa existance ya hiyo "mikunjo na mikwaju", watu tumesafiri pia kidogo na tumeziona pia kwani the world's first flyover was constructed in 1842!
    Unataka nikuwekee ya Feri Dar es Salaam?

    ReplyDelete
  8. eehhee hapo sasa ndio addis ababa na sio picha ya post iliyopita

    ReplyDelete
  9. Kumbe hata Ehiopia kwenyewe hujafika sasa ulikuwa unapiga kelele za nini, na huyo wa Bankok naye ni sawa wewe tu.

    ReplyDelete
  10. we unayesema umesafiri umefika mpaka wapi..wacha bwana.wenzetu wanajenga hizo flyover sio kuonyesha kuwa nchi ina uwezo la.. ni kurahisisha maisha na kuinua uchumi.. mahali pa kusafiri hapo Bongo kwa 1hr wenzetu wamerahisha kwa kuweka hicho kitu unakiita flyover withing 20min wamefika si uchumu wa nchi utapanda!!! na kazi zitafanyika.. au unataka kutumia siku nzima kusafiri ndani ya jiji... kweli naona umesafiri sana...lol..

    ReplyDelete
  11. Hiyo Mikunjo ni mikwara tu, MIchuzi na wewe watolee kitu chetu cha Ubungo. sisi umeme wakuwasha taa tu za ndani tunapewa mgao je barabara tutaweza kweli?

    ReplyDelete
  12. sio kila msongamano unahitaji flyover!
    Kwa hesabu za 2007, Tz ilikuwa na magari kama 700,000 +/- tu.
    Soln: Tawanya/Hamisha huduma za jamii zilizosongamana DBD, Badilisha 2 lanes kwenda 4 lanes na weka service Roads, Weka Dar Outer Ring Road(s) i.e sio lazima kupitia Mwenge ukitoka Kimara kwenda Tegeta, imarisha barabara za ndani ndani, i.e Sinza-Mwananyamala, improve quality ya public transport, baada ya hapo fikiria flyover!
    Ukipiga flyoer bila kuweka mambo sawa, hizo gari zikishuka zinaenda barabara gani?

    ReplyDelete
  13. WABONGO MANENO MENGI TUU, MPAKA RAIS WENU ANAWA ACCUSE KWA UDOKOZI , HAMFIKI POPOTE NYIE.
    FROM MKENYA KEMPINSKI

    ReplyDelete
  14. Hii ni changamoto kwetu ikiwa tunathubutu,inawezekana.

    ReplyDelete
  15. watu wengine vicha maji kweli au ndio tuseme wabongo tumedata kiaina

    hivi kweli unaweza kufananisha bankok na bongo ?????????

    bongo jifananisheni na burundi rwanda kenya eti mnajifananisha na bankok hahahaha kaaazi kweli kweli

    mnajifananisha na nchi ambazo wana uwezo wa kutengeneza kila kitu wao wenyewe kuanzia magari mashine za kila aina

    mnajifananisha na bankok?????? waaaaaaaaat?????

    bongo hata miwani haitengenezi

    ankal mzee wa konoz na libenekez mambo kama hayo usikubali kuyatoa humu eti kufananisha bongo na bankok kweli tuna akili ??

    ReplyDelete
  16. JAMANI TUSISIFIE WENZETU KILA SIKU,MKATAA KWAO MTUMWA HATA SIE TUNAVYO VYAKUJIVUNIA. HIZO BARABARA ZISIWAUMIZE KICHWA HUKO KOTE NIMEFIKA NA NIMEISHI,HAMJUI MAISHA YAO MNAONA NJE TU.WEKENI MLIMA KILIMANJARO NA SIE TUNAO KILA CKU MNAWEKA VYA MAJIRANI TU.

    ReplyDelete
  17. HUYU NAYE SASA UNATAKA KUFANANISHA BANGKOK HUWEZI KUIFANANISHA HATA NA NIGERIA NDUGU YANGU KWANZA KUHUSU BARABARA KAMA HIZO HUKO UK UENGEREZA IPO SEHEMU ZA MIDLANDS TU SEMBWESE KWETU. JAMES>

    ReplyDelete
  18. Hizi ndio fikra za kifisadi. Wakulima Mpitimbi wanashindwa kufikisha mazao sokoni kwa sababu ya kukosa hata barabara za kiwango cha vumbi. Leo mnataka mara flyover mara bangcock. Let's get our priorities straight.

    ReplyDelete
  19. AISEE SIS WABONGO NI MWISHO..NILIPATA KUSIKIA KUNA WAFANYAKAZI WASEREKALI WALIPATA KIMWALIKO KWENDA NJE KUONA WENZAO UTENDAJI KAZI..INASEMAKANA KUFIKA KULE KILA MMOJA AKAINGIA MITTAAANI KUPIGA SHOPING YA MAGARI.....SASA KWANAMNA HII HATUFIKI..PILI WENZETU MATUMBO WANAYAPUMZISHA...WANAKULA WAKIJENGA...SISI TUNAKULA TUKIBOMOA FAMILIA ZETU KWA MACHANGUDOA...IMAGINE...MPAKA BUNGENI..KWELI TUTASALIMIKA...AFADHALI MUNGU AMETULETEA JANGA LA UKIMWI UWAMALIZE WAJE WWENGINE WASAWAZISHE.......

    ReplyDelete
  20. NINYI WABONGO KALIENI KULA MAGIMBI TU MKIAMINI KWAMBA BONGO NI POA.NDO MAANA HATA VIONGOZI WENU WEMEJIRIDHISHA NA UTENDAJI WAO WAKIAMINI EVERYTHING IS WELL DONE KWA SABABU NINYI WALA MAGIMBI MNASHABIKIA UBOVU WAO.TEMBEENI MUONE NCHI ZINGINE WALIPA KODI WANAVYOFAIDI KODI ZAO.NINYI WATOTO WENU WANAKAA CHINI MADARASANI,THATS OK,MNAKAA KWENYE TRAFFIC MASAA KIBAO HUKU HAKUNA LOLOTE LINALOSEMWA TOKA KWA WAO VIONGOZI WENU,THATS FINE,AJALI KILA KUKICHA,THATS OK,RUSHWA KILA SEHEMU,THATS WAY OF BONGO LIFE...NOTHING WILL B ARCHIEVED IF YOU GUYS DONT WAKE UP AND DEMAND FOR REAL CHANGE

    ReplyDelete
  21. Mdau wa 01:16 nakubaliana na wewe asilimia 100, Nadhani tunahitaji kuwatoa watawala wenye mtindio wa ubunifu 2010!!

    ReplyDelete
  22. Wabongo mbona vichwa venu avina kitu hizi barabara zinazo jengwa sasa hivi ni za msaada ayo maji tu ktk mji mmoja wa dar unakushindeni au umeme nao ni watabu alafu mnafikilia kuya tembeza magari juu nyie vipi au hizo pesa zakujenga barabara za juu atatoa babu zenu . kwanza malizeni matatizo ya kusambaza maji na umeme hivi nyie amjui kama dar watu bado wanaoga kwa kutumia ndoo. ebu malizeni kwanza matatizo ya viongozi wenu ya kujichotea maji cent na kwenda kuyaweka uraya alafu ndio mfikilie vitu vingine . mtafananishaje thailand na tz nyie weu nini ebu angalieni siasa yao kwanza wenzenu wamefikia hatua ya kumfunga kiongozi wa nchi yao nyinyi makatibu wakuu tu wanakushindeni

    ReplyDelete
  23. Kwanza hilo eneo la kuweka hizo mabarabara hakuna kamji kenyewe kadogo na isitoshe hao makandarasi wataiba hiyo Cement, mara gari zinatua kwenye nyumba za watu, hapa ni kuwapa mshiko waganga wa jadi waje na fly Over zao. Jibu ndo hilo, Semeni jingine

    ReplyDelete
  24. nini kuoga kwa ndo acha iyo kwanza kuna kuyatafuta ayo maji afu maji yenyewe ya ya chumvi ukikosea taimingi hautoki bafuni sabuni ilivyokunasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...