Marehemu Martha Alu Alute enzi za uhai wake

Familia ya Mzee Augostino Lissu Mughwai wa Mahambe, Singida inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa,Martha Alu Alute kilichotokea tarehe 30 Machi, 2010 huko Dar es Salaam, Tanzania.

Maandalizi yanafanywa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Mahambe, Singida kwa mazishi.

Marehemu alizaliwa mwaka 1932 Ighuka, Singida. Ameacha mume na watoto nane: Alute Mughwai wa Arusha, Tundu Lissu, Mjengi Lissu na Christina Lissu wa Dar es Salaam, Rose Masesa wa Songea, Peter Muro Mughwai wa Kondoa, Mateo Mughwai wa Singida na Vincent Lissu Mughwai wa Connecticut, Marekani.

Vile vile marehemu ameacha wajukuu 20, na vitukuu 6.

Kwa marafiki wa wafiwa wanaokaa nje ya Tanzania (Marekani, Uingereza n.k) unaweza kutuma rambirambi zako kwenye
accnt # 1259458568,
routing #221172610.
Au
kwenye anwani ifuatayo:
Vincent Mughwai
370 Huntington Road
2F Bridgeport
CT 06608

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni kaka na dada zangu. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.Alex na Familia, Maryland, USA

    ReplyDelete
  2. Lissu Mghwai poleni kwa msiba mlioupata, mlimpenda mama sana lakini mungu amempenda zaidi, BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMEN. Alcard Mumwi& Family, Dar, Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Poleni,kwani Bwana ametoa na ametwaa. Ila rambi rambi lazima tuweke kwa hizo akaunti??

    ReplyDelete
  4. Mungu awasaidie sana katika kipindi hiki kigumu cha msiba,poleni sana kwa msiba,D.Mwashumbe

    ReplyDelete
  5. Patrick TsereApril 02, 2010

    Ndugu ALUTE na TUNDU namuomba Mungu awatie nguvu na moyo wa subira wakati huu ambapo mumefikwa na msiba wa kufiwa na mama yenu. Poleni sana. May Her Soul Rest in Eternal Peace. Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...