Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeifunga timu ya taifa ya Ethiopia kwa mabao 3-1.

Mchezo huo umefanyika mjini Addis Ababa. Mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake nchini Tanzania, Lina Mhando, amekiambia kipindi cha Michezo na Wachezaji cha BBC kuwa goli la kwanza limefungwa na Esther Chamburuma.
Amesema bao la pili limefungwa na Mwanahamisi Omari la tatu kufungwa na Asha Rashid.

Timu hizo zitakutana tena wiki mbili zijazo, katika mechi itakayochezwa mjini Dar es Salaam. Atakayeibuka mshindi baada ya mechi hizo mbili atacheza na Eritrea, kufuatia timu ya Kenya kuamua kujiondoa katika mechi hizo za kufuzu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hiyo mashine Ester Chabruma noma! Wadau tujitokeze kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti Twiga Stars.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana dada zetu, mwanzo mzuri. Tunawatikia kila la kheri katika safari yenu hii ngumu. Wakija na kwetu wembe ule ule mpaka JK awaite Mjengoni mle nae dina na mazawadi bwerere. Msikubali tuamini kuwa watanzania tunabweteka haraka tunapofanikiwa kidogo.Kazeni buti mwendo mdundo.

    Mdau wa Mbezi
    (Ni mdau wa Cardiff nierejea Nyumbani)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...