Hivi ndivyo hali ilivyo leo ya kiplefti chetu mtaa wa azikiwe street jijini dar. Tumesimamisha ujenzi kwa muda kwa sababu injinia kaitwa mwenge kuangalia mambo yanavyokwenda, na mashine ya kupikia lami haijarudi toka kibiti. Tutamalizia kazi ijumaa ijayo hivyo tunamwomba JK na Pindwa wafanye subira. Tukimaliza tutawaita waje kuzindua kiplefti hii ambayo ujenzi wake umeanza Macho mosi mwaka huu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Msaada ndani ya TuuTaaa!,

    Hivii, chaitwa kiplefti kwa kuwa ni kidogo? Je likiwa BONGE, yaani kubwaaaa laitwaje?

    Mdau, ALGERIE

    ReplyDelete
  2. NJIA PANDA YA HAILE SELASIE NA CHOLE WALILETWA WAFANYAKAZI KUMI NA TANO KUZIBA MASHIMO MANNE YENYE ENEO LA MITA SITA ZA MRABA NA WALILETA TANI KUMI NA TANO ZA UDONGO KISHA WAKAFUKIA MITA MBILI NA NUSU ZA MRABA KWAZI ILIYOFANYIKA SIKU MBILI SIKU YA NNE UDONGO ULIOBAKI UKAYEYUKA HUENDA KWA UPEPO TOKA BAHARINI. SASA HIVI KAZI IMEKAMILIKA JAPOKUWA MASHIMO BADO YAPO LAKINI BAADA YA SIKU KWENDA TUNATEGEMEA YATAPONA.

    ReplyDelete
  3. Michuzi hao watu bado hawajakuelewa kabisaaa .... hapo unaona jinsi tunavyoenda kiolela olela ...Na sisi jangwani beach shule mfareji mpaka leo bado hauja shughulikiwa! mvua zikinyesha ni mafuriko...

    ReplyDelete
  4. Mdau Algerie, wanaita kiplefti kutokana na maneno 'keep left' ya Kiingereza. Mtumia barabara hupaswa kuzunguka hivi visiwa barabarani kwa kupitia kushoto.

    ReplyDelete
  5. Mdau Algerie keepleft kikiwa kikubwa kinaitwa `LIPLEFT` tia akili!...nchi hii!Michuzi nafikiri wakati umefika sasa matatizo kama haya mwendelezo wake uwe unawekewa na muda,kwa maana ipi,nimeshuhudia mashimo ya barabarani mitaa ya nyumbani inakua pamoja nawe! unamaliza shule ya msingi shimo liko pale pale na watu wanalizunguka kila siku,unaingia sekondari,una bahatika elimu ya chuo kikuu,umeweza kufanya shahada ya uzamili na sasa una kazi nawe unaendesha gari na unalizunguka shimo lile lile wazazi wako walikuwa wanalizunguka!naamini sana juu ya takwimu,tukiweza kutathimini shimo kama hilo limekaa bila kushughulikiwa kwa idadi ya siku,masaa,au dakika utweza kuona mipango yetu haiendi kwa wakati kiasi gani,napendekeza mitaro,mifereji,mashimo na madaraja yawekwe katika blog yako kwa mtiririko wa takwimu,mfano yana `square metre` ngapi inaweza gharama yake ikawa kiasi gani?imechukua muda kiasi gani wahusika kulishughulikia tatizo,naamin itatusaidia kujiangalia upya na kutenda mambo yetu kwa wakati..Dar ni miongoni mwa majiji machafu ulimwenguni na uchafu mmojawapo ni mashimo kama hayo katikati ya jiji.Ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...