Katibu Mkuu wa Umoja wa Madreva wa Mabasi ya Abiria Tanzania (UWATA) Salum Abdallah (kulia) akitoa tamko jana jijini Dar es salaam la kuwadhibiti madreva wote wenye tabia za kuendesha mabasi kwa mwendo kasi na hivyo kusababisha ajali. Kushoto ni mjumbe wa Kamati Kuu ya UWAMATA Yusuph Mgumba. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Is that a pyramid sign over there ?
    Illuminati drivers?, cummon dont make me chuck !
    no wonder they are killing us more than Americans in Kandahar .
    Drivers be careful please!
    Dont drink and drive , you will spill the drink !
    If you can afford a drink, why cant you afford the tax too !
    Kaima (UK)

    ReplyDelete
  2. SAWA; NI WAZO ZURI LAKINI
    AJALI SIYO MADEREVA TU;
    VIPI UBORA WA MABASI NA BARABARA???
    ALAMA ZA BARABARANI NA MATAA NAYO YANA TILIWA MAANANI??????

    ReplyDelete
  3. Hamna kitu bla bla tu hizo, hivi kwanini madereva wa magari ya abiria hapa bongo (sijui nchi zingine) huwa ni kama hawana akili? Wanapenda sana kwenda mwendo kasi hata pale ambapo hapastahili. Daladala anajua anasimama vituoni lakini hata mita 100 kabla ya kituo anataka a-overtake gari ya mbele. Mabasi ya mikoani sheria ya kuto-overtake kwenye kona, mwinuko au anapoona gari inakuja upande wa pili ni kama hawaijui na hawaoni umuhimu wake kabisa. Ajali nyingi zinatokana na overtaking. Imagine kwenye kona kama za Mikumi mpaka Kitonga kwa waliokwenda nyanda za juu kusini dereva wa basi ana-overtake kama anaendesha gari ya mashindano, wakati upande wa pili wa kona hauonekani. Wenyewe kwa wenyewe wanapenda sana kushindana, hawezi kukubali basi jingine au gari yoyote iwe mbele yake. Kwa daladala kusimama ni popote na wakati wowote mradi kuna abiria, hata hawajali watumiaji wengine wa barabara, wanapo'tanua' pembezoni mwa barabara wanakwenda speed kama ya mwizi bila kujali kwamba mtu anaweza kutokea ghafla. Kwao kukaa foleni ni mwiko. Madereva wa magari ya abiria wana matatizo gani? Kwanini wanapuuza sana sheria za usalama barabarani? Maswali kama haya yakijibiwa na hawa madereva wakapelekwa rehabilitation kutibiwa matatizo yao ndipo ajali zitakwisha.

    ReplyDelete
  4. JAMANI TUACHE MZAHA , HIVI TUNAWEZA DHIBITI MADEREVA KWA TAMKO? HIKI NI KICHEKESHO.. KAMA INGEKUWA INAWEZEKANA KAUWADHIBITI KWA MATAMKO BASI POLISI WANGEKUWA WAMEWEZA KWANI KILA SIKU NDIO KITU WANACHOFANYA AKINA KOMBE NA MPINGA. THESE GUYS ARE NOT SERIOUS. WEKENI GAVANA TUU NDIO SULUHISHO. ACHENI LONGOLONGO HAPA..

    Mzozaji

    ReplyDelete
  5. MIMI BINAFSI SIWEZI KULAUMU TRAFIK POLISI, KWANZA WANAKAMSHAHARA KADO... PIA HATA UNGEKUWA WEWE NI TRAFIK PIGA UA UNGECHUKUA KITU NDOGO TU HIYO NI, MIMI NALAUMU ABIRIA MAANA KUNA WANAOCHOCHEA MADEREVA WAENDE KASI ILI WAWAHI, NA WAPO WANANYUTI TU, LAKINI KAMA ABIRIA WAKIWA WANAWAPA KICHAPO MADEREVA KIMEO HIZI AJALI USINGE ZISIKIA KABSAA
    AU SERIKALI IONGEZE MATUTA NDO SURUHISHO KILA MMOJA ACHELEWE

    ReplyDelete
  6. Anony wa Wed Mar 17, 04:50:00 PM,
    hawa madereva akili zao ni sawa akili za NGUCHURO tu hamna la maana wanalolijua, siku wakisamama kwa mbele kupakia wewe overtake na usimame kama yeye, alafu wakilisha riport ndani ya blog.

    ReplyDelete
  7. Mimi bado nawalaumu polisi usalama wa barabari hata wale wapima uzito, kwasababu mara nyingi wakipigwa mkono njiani dereva anatoka kwenda kwa polisi au hata kama polisi akimfuata dereva anaongea naye dirishani kwanini polisi wasiingie ndani ya gari kuona je huyu jamaa amezidisha abiria je ubora basi hili ni vipi? Halafu watu wa mizani wanatakiwa kujua basi linatakiwa kufika eneo fulani saa ngapi na kama limewahi linapigwa stop kukaa kufidia muda wake na abiria wafundishwe hili kuanzia kukata tiketi maana unaingia mkataba na mwenye gari na abiria waweze kutafutiwa usafiri mwingine wakuwafikisha kule waendako. Tukiweza kufanya hivi hawa matajiri wa basi watakuwa wakali kwa madereva maana kama atarudisha nauli mara tatu kwa abiria na fine juu sijui kama watafurahia

    ReplyDelete
  8. Hili ni suala la wizara ya mambo ya ndani. Kama hatuna sheria madhubuti Wizara ya mambo ya ndani inabidi itunge sheria ngumu, polisi waache kula rushwa na wa enforce hizo sheria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...