ankal captain gadna G. habash na mdau Hartmann kwenye retreat ya Kili Tanzania Music Awards Academy leo hoteli ya Kunduchi Beach
ankal akiwa na mbonie masimba wakiwa katika retreat ya Kilimanjaro Tanzania music Awards Academy 2010 katika hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar leo Mkurugenzi wa masoko wa TBL David Minja (shoto) akipiga stori na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephrahim Mafuru



baadhi ya washiriki katika retreat hiyo

washiriki wakielekea eneo la tukio

Dina Marios (shoto) wakiwa na wadau wa TBC-1

Mussa Kipanya (Kulia) na anti nanihi

wote tuko Pamo Jah!

wadau wakiripoti hotelini

DJ Choka akiendeleza libeneke na wadau kwenye Academy hiyo

Toka shoto ni Saidi Tuli, Frank Kassanga Bwalya,

Mkalla Fundikira na Mahmoud Zubeiry











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. du huyu frank machozi kwa kujirusha ka amezidi yaani jamaa anasafiri kula raha alikuwa london mwezi huu kwenye traffic light party,hivi shughuli zake ni nini hasa?michuzi usinibanie na wewe ndio hao hao

    ReplyDelete
  2. Ankal na Wadau wengine mbona ni kitambo kirefu mkmusicgalaxy.com ina kwikwi? au wamebadilisha link zao?
    Kwa mdau yeyote anayejua website ya miziki ya ki-bongo(bongo flavour,zilipendwa n.k) anirushie link.

    Mdau Zurich

    ReplyDelete
  3. Wanadamu ni wanyama ambao huishi kimakundi makundi kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, nyumbu, nyati, swala, paa, pundamilia, twiga, tembo, na kadhalika.

    Katika makundi makundi ya binadamu kuna yale ya maamuma na viongozi mathalani wanasiasa, waumini waswahalina na walokole, mashabiki na wanazi wa michezo na kadhalika.

    Huku kwetu Tanzania miaka ya karibuni tunaweza kusema kuanzia mwaka 2005 na kuendelea limechipukia hili kundi ambalo kila kukicha wamo maradioni, televisheni, magazetini, mabloguni, na kwenye tovuti mbali mbali. Shughuli yao kubwa ulimbwende, muziki au ubibi uzuri.

    Kundi hili limebarikiwa kupata wahisani na wafadhili ambao huwaandalia mafunzo, hafla na tafrija kubwa kubwa kwenye kumbi na mahoteli makubwa ya kifahari ambapo wengi wa washiriki wasingeliweza kufika kupitia vipato na wasifu wao binafsi. Makampuni ya vinywaji na mawasiliano hususani pombe na simu za mkononi ndiyo wafadhili na wahisani wakuu wa shughuli za kundi hili.

    Sijui asilimia ngapi ya wanakundi hili ambao wanajua kiukweli kweli wanachofanya aidha iwe muziki kama ni wapiga ala au waimbaji stadi. Kama ni walimbwende kama ni wabunifu kweli na wanaoweza kutofautisha kanga na kitenge, au kitambaa cha pamba na hariri, kutia rangi nguo, au kushona. Au kutofautisha kiatu cha kokoko na makubazi. Kujua tofauti kati ya utuli na utuli, au mafuta ya nywele na ya mwili, au krimu ya uso na ya mwili, au wanja na mdaa.

    Inawezekana kuwa wanakundi hili wengi ni wajuzi katika fani zao pia inawezekana kuwa wengi hawajui wanafanya nini haswa.

    Bahati mbaya kwa sababu "zilizo juu ya uwezo wetu" wanazuoni wetu hawafanyi tafiti nyingi za kina kwenye social psychology au sociology. Kundi hili linaweza kuwa na athari chanya au hasi kwenye jamii yetu.

    ReplyDelete
  4. JOHN MASHAKA, EMBU ANDIKA AYTIKO KUHUSU HAWA WAPENDA STAREHE NA MARAHA NDANI YA ROHO. KILA KUKICHA SIJUI MI AWADI GANI. ELIMU HAWANA, KAZI ZA MAANA ZIIII, KAAZI KUUZA SULA TU, WABONGO BANA

    ReplyDelete
  5. ...mdau wa Sat Mar 20, 06:54:00 PM acha kuzunguka mbuyu....lete conclusion !!!

    ReplyDelete
  6. jamani si muende huko moshi mukasiadie hata kujenga shule na misaada mengine kwa jamii, starehe tuuuuuuuu na wakati wenginee wanaesabu tu siku

    ReplyDelete
  7. swali la kizushi, kondomu ziligawiwa huko??

    ReplyDelete
  8. uwiiiii nini hiki tena???

    heeeeee

    wee mdau 3:39pm mbavu zangu kwi kwi
    una visa?!!

    ReplyDelete
  9. Uncle Nanihii = X
    Shangazi Nanihii = y

    If x ni shangazi wa Z
    Na y ni uncle wa Z

    Na wote x & y wana-surname ya Nanihii;

    But X = Ankal Michu,

    Je Y ni nani?

    ReplyDelete
  10. kwani Mussa wa TBC1 na Masoud Kipanya ni ndugu? nisaidieni jamani

    ReplyDelete
  11. aliyeuliza kuhusu Condom ana akili sana, maana waliokusanyika hapo mostly clouds ambao kila mtu anatembea na kila mtu na akili za most of them ni ktk chupi.... msonyo!!

    ReplyDelete
  12. dunia hiiiiiiiiiiiiii God help them wamemaliza mamisssss sasa ni zamu ya wasiniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...