sehemu ya waombolezaji kwenye hafla hiyo
Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro akitoa neno. Kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Dk. Augustine Mahiga na shoto ni Mchungaji Butiku Pelocy
Kwa upande wake Father Petro kutoka Shirika la Maryknoll na rafiki wa karibu sana wa Marehemu Balozi Mwakawago, akizungumza kwa Kiswahili kilichonyooka.

Anasema kama si mchango na ushirikiano mkubwa alioutoa Marehemu, basi Shirika hilo lisingeweza kujenga Chuo Kikuu cha Udaktari cha Bungando, ambapo Madaktari 34 wameshahitimu kozi ya udaktari na ambao karibu na wote wanafanya kazi katika hospitali hiyo.

“Tulifanya kazi naye kwa karibu sana, aliweze kuwaunganisha wamarekani na watanzania hadi tukaweza kujenga Chuo hicho, alikuwa ni mtu mwenye mawazo na mchango mkubwa, tutamkumbuka sana” akasema Padre Petro.

Akiunga mkono hoja ya kuwa marehemu alikuwa mtu wa watu na aliyejishusha, Padre Petro ambaye alifuatana na Bi Sally kutoka Touch Foundation na mpwa yake ambaye pia anaitwa Petro anaeleza. “ nilipokuwa nikimwita Mhe.Balozi, yeye daima alikuwa akisema niite Daudi tu inatosha, huyu ndiye Mwakawago aliyekuwa na uwezo na mawazo ya kuzilainisha nyonyo za wamarekani hadi wakajenga urafiki mkubwa na watanzania”.
Mchungaji Pelocy Butiku akiongoza sala
Familia ya Marehemu Balozi Mwakawago
Balozi Dk. Mahiga akimpa pole binti wa Marehemu
Na Mwandishi Maalum
NEW YORK- Watanzania wanaoishi jijijni New York na vitongoji vyake, wamemwelezea Marehemu Balozi Daudi Ngaleutwa Mwakawago kwamba kwao alikuwa zaidi ya Balozi.

“Kwetu sisi alikuwa sawa na Baba, alikuwa mlezi wetu, alitujua kwa majina mpaka ya watoto wetu. Alijua tunakoishi hataka kama ni ‘uswahili’, hakujali alifika. Alikuwa rafiki na mwalimu aliyetufundisha kuhusu thamani ya utanzania wetu na umuhimu wa kuuenzi”.

Wameyasema hayo kupitia mwakilishi wao Dkt. Benson Mwakalinga Mwenyekiti wa Kamati iliyoandaa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania halfa maalum ya kumkumbuka na kumwombea Dua Marehemu Balozi Daudi Mwakawago.

Hafla hiyo imefanyika siku ya jumamosi katika Makazi ya Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dkt. Augustine Mahiga. Na kuhudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, watoto wa marehemu na marafiki wa karibu wa Marehemu Balozi Mwakago.

Na ilianza kwa Dua iliyosomwa na Prof. Alhaji Abbas Byabusha akishirikiana na Sheikh Hassan Maftaha kwa upande wa madhebu ya Kiislamu . Wakati upande wa Madhehebu ya Kikrsto Sala iliongozwa na Mchungaji (Rev) Perucy Butiku.

Watanzania hao ambao walionyesha waziwasi huzuni na hisia zao kwa kuondokewa ghafla na aliyekuwa kiongozi wao kwa miaka tisa. Wanasema Marehemu daima alitanguliza mbele utanzania na maslahi ya watanzania kuliko kitu kingine chochote.

“Alitujali sote, bila ya kujali dini zetu, jinsia zetu , unawadhifa gani au ulikuwa unatoka wapi. Alikuwa na moyo wakushirikiana na kila mtu , makazi yake yalikuwa makazi yetu.Alitupatia elimu na maarifa mbalimbali, alitufunza jeuri ya kuwa mtanzania. Na daima alituhimiza watanzania wa New York kupendana na kushirikiana” anasema Mwakalinga

Na Kuongeza. “ Pamoja na kwamba alifahamiana na watu wengi na wa kila hadhi,mamlaka na utajiri lakini kamwe hakuitumia fursa hiyo kujilimbikiza utajiri, daima alitanguliza maslahi ya nchi na watanzania. Hakuwa mtu wa makuu, hakuwa mtu wa kuthamini ufahari.

Kwa upande wake, Balozi Augustine Mahiga, yeye amemuelezea Balozi Mwakawago kama kiongozi ambaye ni kielelezo cha uadilifu, uaminifu na aliyefanya vizuri kazi yoyote aliyopewa.

“ Tulifahamiana na marehemu tangu tukiwa wadogo, alikuwa ni mtu asiye kata tama, aliyejituma sana katika kuifafuta elimu. Alikuwa kati ya watanzania wachache waliopata shahada wakati wa ukoloni. Hakuwa mtu wa mali, mali yake ilikuwa ni heshima anayopata kutoka kwa watu anaowaongoza na kwa kweli hakuna mtu anayeweza kumnyooshea kidole kwamba alijilimbikiziza mali” anasema Balozi Mahiga.

Balozi Mahiga anasema sifa za mwanadamu ni chache na hakuna sifa ambazo marehemu hakuwa nazo, alikuwa mtu wa dini, aliyetoa mchang wake mkubwa kwa taifa tangu wakati wa TANU. Alikuwa mtu wa kawaida kabisa, hakuwa na mbwembwe na kwa lugha nyingine tunaweza kusema alikuwa mtu ‘modest’ na mfano wa kuigwa na kila mtu na hasa vijana.

Naye Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro, yeye anasema. Balozi Daudi Mwakawago anakumbukuwa sana kwa mchango wake katika Umoja wa Mataifa. Na kwamba alikuwa ni mwalimu aliyefundisha kwa maneno na matendo.

“ Nakumbuka nilipoteuliwa kushika wadhifa huu nilionao sasa, hakusita kunitafuta na kunipatia ushauri na wosia, na hata nilipokwenda Tanzania mwaka jana na aliposikia nipo alinipigia simu na kunisalimu, ndivyo alivyokuwa Marehemu,alikuwa mnyoofu, mwadilifu na aliyejitoa” anasema Migiro

Kwa upande wake Father Petro kutoka Shirika la Watawa wa Menonite na rafiki wa karibu sana wa Marehemu Balozi Mwakawago, akizungumza kwa Kiswahili kilichonyooka.

Anasema Kama si mchango na ushirikiano mkubwa alioutoa Marehemu, basi Shirika hilo lisingeweza kujenga Hospitali kubwa ya Rufaa ya Bungado, pamoja na kusomesha Madaktari 34 ambao wote wanafanya kazi katika hospitali hiyo.

“Tulifanya kazi naye kwa karibu sana, aliweze kuwaunganisha wamarekani na watanzania hadi tukaweza kujenga hospitali ile, alikuwa ni mtu mwenye mawazo na mchango mkubwa, tutamkumbuka sana” akasema Padre Petro.

Akiunga mkono hoja ya kuwa marehemu alikuwa mtu wa watu na aliyejishusha, Padre Petro ambaye alifuatana na Bi Sally kutoka Touch Foundation na Binamu yake ambaye pia anaitwa Petro anaeleza. “ nilipokuwa nikimwita Mhe.Balozi, yeye daima alikuwa akisema niite Daudi tu inatosha, huyu ndiye Mwakawago aliyekuwa na uwezo na mawazo ya kuzilainisha nyonyo za wamarekani hadi wakajenga urafiki mkubwa na watanzania”.

Katika Hafla hiyo pia ziliwasilishwa salamu kutoka kwa Bw. Eddie Begum wa Miracle Corner of the World, taasisi ambayo ilikuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na marehemu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali hasa ile inayolenga katika uwezeshaji wa vijana. Akasema wamempoteza Mshauri wao, rafiki na Kaka.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Bi. Jenista Mhagama (MB) na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Asha Abdulla Juma, Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, wanawake na watoto kutoka serikali ya Mapinfuzi Zanzibar, Msajili wa Mahakama ya Rufaa Bw. Francis Mutungi, Kanali Maganga na Bw.Abbass Missana Kutoka Ubalozi wa Tanzania –Washington..











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni na Msiba wa Mzee wetu mwakawango. Sahihisho kidogo. Huyo hapo ni Padre Dr. Petro Lejacq, MM padri wa Mashirika la Maryknoll na si Mennonite kama ilivyotajwa. Ninakumbuka sana jinsi Balozi Mwakawago alivyoshiriki fika katika kufaniksiha ukarabati wa hosptali ya Rufaa ya Bugando akishirikiana na Padre Peter na Watanzania wengi hapa NYC.

    ReplyDelete
  2. Sahihisho kidogo siyo Prof. Alhaji Abbas Byabusha ni Dr. Alhaji Abbas Byabusha

    ReplyDelete
  3. poleni wana familia wote,ndugu na marafiki na watanzania wote kwa kifo cha mzee wetu,rafiki yetu,ndugu yetu mpendwa balozi mwakawago,INNA LILLAHI WAINA ILLAHI RAJIUN.

    Lakini nina swali hili mmoja mbona anapokuwa kabwera watanzania we New York hawakusanyiki na kungana na wafiwa,kama ilivyo kwa watanzania wa D.C wenye ushirikiano wa hali ya juu kwa kila kitu.Meaning furaha kwenye harusi na msiba kwenye vifo wote watanzania wa D.c huwa kitu kimoja na kushirikiana.

    Nimetoa duku duku langu hili kwa sababu wakati kunapotokea mambo kama haya watanzania wengi wa New York huwa hawaabiwi na balozi yetu,meaning hawapigiwi hata simu isipokuwa wale wanaojulika(famous) ndo hupigiwa visimu vyao na kuwaarifu leo kuna hivi na vile balozini au kwa mama balozi,ina ni kera sana hiii na sio leo ni long time mambo haya hufanyika ukija kusikia unashanga duu yani mimi si mtanzania mbona sijapigiwa simu au kutaarifiwa.

    michuzi mkuu usiibaniye comment yangu ukiibania nitaweka kwenye blog zote za kiswahili sina wasi wasi sawa mkuu.kwa sababu nataka wajue wanavyofanya wafanyakazi wa ubalozi wa tanzania si sawa kabisa, wana ubinafsi kutoa taarifa kwa watu wanao wataka wao na walio karibu yao.

    ReplyDelete
  4. watu waadilifu manbo makubwa waliyofanya yawe yanawekwa magazetini, tusisubiri mpaka wafe kutoa sifa zao.wapo wengi wanawake kwa waume. kuwe na kipindi cha kuwaenzi watu namna hii

    ReplyDelete
  5. sasa mbona umu mmekazana kusema uyo ni padre ni mennonite?
    poleni wafiwa wote mtiwe nguvu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...