Ankal Michu kwanza pole sana kwa kazi ngumu nay a uvumilivu unayotufanyia..mie naomba unisaidie pamoja na wadau wote nina utata.
Kuna eneo liko maeneo ya Tangasisi kata ya Mwambani-Tanga kuna viwanja vilikatwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tanga, vikauzwa na watu wakapewa hati zao na zina Namba za viwanja.
Watu wakaanda ramani za ujenzi na zikapitishwa na Manispaa hiyo hiyo na watu wakaanza kujenga ….Leo hii Wakurugenzi hao hao wa Manispaa wamekongea na watu wa eneo hilo na kusema kuwa eneo lile liko karibu na Bandari (Bandari mpya ya tanga).
Kwahiyo nyumba pamoja na viwanja ambavyo vipo Eneo hilo vinaweza vikachukulwia na bandari kwa vile havipo kwenye Ramani ya mji…Kwahiyo kila mtu anapaswa atoe 100,000/= ili nyumba au kiwanja chake kitiwe ndani ya ramani.
Swali langu ni hili…JE?? Gharama za kutia kiwanja kwenye ramani ya mji ni gharama za Manispaa/Ardhi au za mwenye kiwanja, je zile pesa tunazolipia kiwanja kila mwaka ni kwa ajli ya shughuli gani???? Na Je? Utagawaje kiwanja na kukipa Namba wakati hakipo kwenye ramani ya mji???? Je kama hakipo kwenye ramani ya mji hizo kodi za kila mwaka za kiwanja kile wanarecord vipi SHAMBA??? Na kama watalipa hizo gharama Je hao bandari ndo watakuja kusema kuwa Si eneo Lao????...

Maana sisi wengine tunamalizia malizia karibu tutahamia kwenye nyumba zetu sasa Pressure zimeshaanza kupanda na kushuka kiukweli…sasa nimegundua kwanini watu wanakufa kabla siku zao…
NAOMBA MNISAIDIE HII ISSUE IPO MIKOANI KOTE AU WAO WAKO SAWA…SIJAELEWA LABDA KWA KUCHANGANYIKIWA...
Mdau Kwa Minchi
UMOJA NI NI NGUVU JIKUSANYANYENI WAHUSIKA WOTE,KILA MTU AJE NA SILA YAKE YA JADI MSUBIRINI MUHUSIKA OFISINI IWE HASUBUHI NA MAPEMA KABLA AJAINGIA OFISINI KISHA MTANDIKETENI KWA KILA KILICHO KARIBU KAMA TUNAVYO JIPANGA SISI WAKAZI WA KIGAMBONI DAR,NA HII NDIO DAWA PEKEE AMINI NAWAMBIA.
ReplyDeletetafuta wakili ili afahamishe sheria inaendaje hapo..
ReplyDeleteUkitafuta wakili itakucost mora than tha...cha muhimu jiungeni wote mumfate huyo mkuu wa mji au sijui majoy wa mji awaeleze kulikoni....asipojibu mumwendee kwa bibi hapo tanga mjini majipu ya mtoke...umoja ni nguvu mkisimama wote kidedea kitaeleweka kitu lakini uoga wa watu wa bongo wanalipa kimya kimya na kutoa rushwa juu....wake up guys
ReplyDeleteby the way hivyo viwabja bado vipo?
Nilikua naangalia olympic canada wakasema nchi yao inawatu million 35 nikajiuliza sisi ilikuaje tuko wengi hivyo na kanchi jet hako kadogo hivyo?