Juu na chini ni Mzee SIKAUKA MWACHANGU (shoto) na Mzee RAFAEL NGOGO (kuume) ambao ni kati ya Viongozi wa Kabila la Kihehe katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wakimvalisha mgolole, Vazi rasmi la Utawala wa kabila la Kihehe na kumkabidhi Utawala wa Kabila hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN alipowasili katika uwanja wa Mashujaa Mufindi kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara. Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. MOHAMED ABDULAZIZI.
Wazee wakimvisha Dk. Shein Mgolole
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN, akiwa amekalia Kigoda huku akishikilia Mkuki mara baada ya kuvalishwa Vazi la Utawala wa Kabila la Kihehe na Wazee wa kabila hilo. .
Kiongozi wa Kabila la Kihehe katika kijiji cha Mafinga Wilayani Mufindi Mzee SIKAUKA MWACHANGU, akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN baada ya kumvalisha Vazi la Utawala wa Kabila la Kihehe na kumkabidhi Utawala wa Kabila hilo katika Uwanja wa Mashujaa Mafinga Wilayani Mufindi kwa ajili ya kuhutubia Wananchi Mkutano wa Hadhara. Picha na mdau Amour Nassor

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Chifu Mkwawa alikuwa akivaa hivyo...I mean the main man aliyewafanyia waherumani.

    Ila nina swali...kwa wafahamu wa history, Hivi Chifu Mkwawa alikuwa ni Muislam, Mkristo au hakuwa na dini?

    Hayo mavazi ni kama waislam machief wengi wa Afrika walikuwa wakivaa enzi hizo, lakini hawa kina-Mkwawa waliofuatia baada yake wengi wamechanganyika, wapo Wakristo na Waislam.

    Just curious, does anybody have any explanation?

    Shukran.

    ReplyDelete
  2. Dini zote,Ila mi swali langu ni kuwa mbona HUYU DR.SHEIN yeye NI MIKOANI TU,HAENDI ULAYA? WAKATI MZEE MZIMA JK KILA SIKU WASHINGTON-CARLIFORNIA-UK-AUSTRALIA! AU NDIO INAVYOKUA UKIWA RAISI USAFIRI NJE YA NCHI TU? BASI HATA KUONDOLEWA VISA YA NCHI MOJA TRIP ZOTE JAMANI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...