Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh. Said Mwambungu ( mbele kulia) akikagua timu ya soka ya Mazimbu Market , akiambatana na Mdhamini wa Mashindano ya ABOOD Cup , Aziz Abood ( wa pili nyumba ) kabla ya mchezo wa fainali dhidi ya timu ya Moro Kids kwenye Uwanja wa Jamhuri wa Morogoro ambapo katika mchezo huo uliofanyika wikiendi hii Moro Kids ilishinda kwa mabao 5-1. Mchezaji wa timu ya soka ya Moro Kids, Godfery Methord akinyayua juu zawadi ya mpira na fedha tasilimu sh: 300,000 kwenye bahasha baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ( watatu kushoto) na wa pili kutoka kushoto ni mfadhili wa mashindo ya Abood Cup, Aziz Abood , ambapo katika mchezo huo Moro Kids iliishinda mabao 5-1 dhidi ya timu ya Mazimbu Market kwenye fainali iliyofanyika wikiendi hii
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Queens kutoka Kata ya Kingolwira, Tatu Ramadhani ( mwenye mpira) akijiandaa kutoa pasi kwa mchezaji mwenzake wakati wa mchezo wa kuhitimisha fainali ya mashindano ya Abood Cup dhidi ya Mji Mpya ambao ni mabingwa wa mashindano hayo , katika mchezo huo, Mji Mpya ilishinda mabao 35 dhidi ya 11 ya Queens.
Picha zote na mdau John Nditi wa Globu ya Jamii.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...