Bondi mkongwe Iraki Hudu (kushoto) akiwaelekeza mabondia wa Klabu ya Ashanti ya Ilala Dar es salaa wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano ya kirafiki yatakayofanyika siku ya 30/4/2010 katika ukumbi wa Max bungoni kulia ni Katibu wa Ashanti FC, Haji Bechina
Juu na chini mabondia wa Ashanti wakila mazoezini kabla ya mpambano wao utakaofanyika ijumaa ijayo ya tarehe 30 Aprili, 2010


Na mwandishi wetu
KLABU mpya ya Mchezo wa Ngumi ya Ashanti inayokuja kwa kasi kuleta mabadiliko ya mchezo uho watacheza mchezo wa kujipima nguvu na zingine za mchezo huo Ijumaa katika ukumbi wa Max Ilala Bungoni Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema Dar es Salaam jana kuwa klabu hiyo yenye mabondia 16 itapigana na klabu zingine itambulike kuwa ni miongoni mwa klabu zinazoendeleza mchezo wa ngumi Tanzania.
Alisema kabla ya kushiriki michezo ya klabu bigwa yanayotarajia kufanyika mapema mwaka uhu ambapo klabu zote zipo katika maandalizi ya kushiliki mashindano hayo,
Super D alisema katika kujipima huko kutakuwa na Klabu za Ashanti ya Ilala, Mtakuja ya Vingunguti, Sifa ya Manzese na Mkumwena ya Buguruni, na wenyeji Ashanti ambapo kila klabu aliwataja mambondia watakaopanda na klabu wanazotoka


KGS (LIGHT FLY WEIGHT)
1. RAJABU HAMISI ‘ROJA MJESHI’ (ASHANTI) Vs HUSSEIN SAID (SIFA)
2. BADRU HASSAN ‘MUHINDI MWEUSI’ (ASHANTI) Vs SALUMU IDDI (MTAKUJA)
3. SHABAN MADILU ‘TYSON’ (ASHANTI) Vs ASHRAF JUMA (MTAKUJA)
4. HASSAN SAID (ASHANTI) Vs SAID ALLY (MTAKUJA)

54 KGS (BANTAM WEIGHT)
1. JOSEPH RICHARD ‘MNYAMA’ (ASHANTI) Vs HUSSEIN KASSIM (SIFA)
2. HUSSEIN ABDALLAH (MTAKUJA) Vs HASSAN SHARI (SIFA)
3. MATIKU MAGESA (ASHANTI) Vs OMAR ABDALLAH (SIFA)
4. HASEN SAID ‘MNGONI’ (ASHANTI) Vs RASHID ABDALLAH (MTAKUJA)
5. IDDI RAMADHAN (ASHANTI) Vs KULWA KILIANI (MTAKUJA)

64 KGS (LIGHT WEIGHT)
1.MOHAMMED RAJAB ‘BONGE’ (ASHANTI) Vs IDDI PIALALI (MTAKUJA)
2. ABJERINA KADRI (ASHANTI) Vs HAMISI ABDI (ASHANTI)
3. JUMA CHAMBALA (ASHANTI) Vs ABDALLAH MSHINDO (MTAKUJA)
4. OMAR KANESA (MTAKUJA) Vs KOBA KITEA (MTAKUJA)5. SAKO MWAISEJE (ASHANTI) Vs SHARIF MZEZELE (SIFA)
6. HANS JOHN (SIFA) Vs MOHAMMED MUSSA (MTAKUJA)

RAJABU MHAMILA “Super D” TEAM COACH
ASHANTI BOXING CLUB
Mobile Numbers:- 0713/0754/0787/0774-406938
WE ARE HERE TO SUPPORT THE GROWTH OF BOXING TALENT




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mkuu wetu naomba mpe ma wasiliano yangu bechina ili tuangalie jinsi gani tunaweza kuisaidia timu yake.

    ReplyDelete
  2. NI wakati wa Juma Nyoso kurudi Ashanti

    ReplyDelete
  3. Nikiwa rais ngumi basi, hakuna mchezo ukaitwa mchezo wa kupigana

    ReplyDelete
  4. na ndo maaana hutakuwa raisi. Kila kiumbe duniani kinajua science ya kupigana. Ni mchezo natural unaotokana na maungo yetu wenyewe. Hakuna kitu kama mpira cha kuchezea, ni mwili wako mwenye na stamina. Michezo mingine ya aina hii ni kama riadha. Sheria za mchezo zipo kujaribu kulinda wachezaji na kama katika michezo mengine yoyote kuumia kunakuwapo. Unajulikana pia kamasweet science na ukiangalia watu wanaojua kuucheza mfano Ali, Hagler, Sugar Ray, Tyson na wengineo wanafurahisha kwa jinsi walivyo pigana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...