ngoma imedata katikati ya barabara sehemu za mikocheni TMJ jijini dar
kila juhudi za kuiwasha inashindikana
ah... isiwe taabu.
haya ndo mambo mvua inaponyesha jijini dar ambako sio tu mitaro ya maji haitoshi, bali pia aidha imeziba kwa kutosafishwa mara kwa mara ama kuzibwa na ujenzi holela. hapo hatujazungumzia haja ya kuboresha miundombinu kwa kadri ya jiji linavyopanuka...




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Sorry, Bro Michuzi,

    I think it will pass our life time and probably the next generation to see the end game of these.

    But for the time being, we probably need to braced with the ultimate SURVIVAL KIT.

    1. Get yourself a wellington boot and full body waterproof Cloth, make as space for them on your car boot. You need to enjoy this experience get them in different colour of your choice, for those who are well loaded get a branded one, or oh well we are living in a city, the presumtious is we are good at spending.

    2. For the cyclist and motocylist, you dont have much of a choice but getting a public transport, if there is any.

    3. the Advice, put your holiday bookings off work during rainy seasons, you get away from it all and go back to country side with Grannys, no MORE X MASS holiday, or EID Holiday long vacation plans, it wont suit us, we need to adjust for ENVIROMENTAL HOLIDAY INSTEAD. what a sad situation.

    but seriously, this is the very very serious issue, and I know the problem. RUSHWA, kutowajibika on CIVIL Service ENGINEERS, or purely lack of professionalism on MIPANGO MIJI and BUDGETING.

    I am sure the problem can systematically resolved on a phase by phase basis, concentrate on hot spots and most viable economic areas such as city centres, which in fact we are blessed with the OFFSHORE(by the SEA), it is therefore become significantly easier for the ENGINEERS TO GET ON BOARD, AND START DRAWING THE TUNNELS AND CHANNELS AND DUMP THE FLOODING WATER ONTO THE SEA. THE QUESTION IS DO THEY ASK THEMSELVES THOSE QUESTIONS, DO THEY HAVE THE BELIEF TO PUT A FULL COSTED PROPASAL TO A MAYOR, DO THEY WORK ON CO HABBIT ON THE MAYOR WITH COORDINATION ON CITY BUDGETING, AND RESPONSIBLE GOVERNMENT OFFICE IN PROVIDING THAT ASSISTANCE IN A TIMELY AND SET TARGETS TO ACHIEVE THOSE GOALS. MY ANSWER TO THESE QUESTION PROBABLY YES, BUT LUCK CONVICTIONS, OR THEY JUST SIT THERE WITHOUT UNDERSTANDING WHAT THEY ARE SUPPOSED TO BE DOING, AND THE LATTER WILL BE A DANGEROUS CONCLUSION ON ALL OF THIS. BECAUSE THEY DONT DESERVE TO BE THERE AT THE FIRST PLACE.

    AND THEN I WILL GO BACK TO MY SURVIVAL KIT GUIDE ABOVE, AND SIT AND WATCH.

    IT IS LIKE A MOVE, BUT WITH NO GOOD ENDINGS.!

    ReplyDelete
  2. bora box kuliko hii hali hapo umetoka job umechokaa kufika home kitimtim manake mvua za bongo foleni hadi saa tano za usiku mbezi hakuendeki hilo halina ubishi utamm kolea umeme wa mgao jesus... !! acheni tu tuloee huku kweli kabisa

    ReplyDelete
  3. Mkiambiwa msinunue pikipiki za machina hamsikii ... haya sasa piki piki inaumwa ngiri! umeona wapi hiyo?

    Kazi kwa Kikwete na mapikipiki yake 50 ya msaada toka China.

    ReplyDelete
  4. Jamani hivi hakuna sehemu nyingine zinazojaa maji zaidi ya TMJ? Mbona kila siku ni TMJ tu?

    ReplyDelete
  5. ANONY WA APRIL 30 11:28 wanaotembea na camera na wenye muda wa kupiga picha wanakaa maeneo hayo. Wewe mimi natoka Mbagala alfajiri napanda daladala nimesimama katikati miguu haiugusi chini nitapiga picha saa ngapi? kwanza nani ataniruhusu nimtoe dirishani ili niweze kupiga picha. Simu yenyewe ninayomiliki ni za promoshen shs 20,000 sasa uliona wapi simu ya promosheni ikawa na camera?

    ReplyDelete
  6. Wanaotamba barabarani na pikipiki za Mchina inabidi wazifungie ndani mpaka mvua zimalizike maana hazipatani kabisa na maji. Pikipiki mpya inapouzwa Sh500,000 tu inabidi ujiulize mara mbili kama ina ubora unaokubalika, sio kuvamia tu kwa sababu bei ni chee.

    ReplyDelete
  7. kwa ujengaji wa majumba mengi katikati ya jiji sio kupanuka,hili jiji lina condensed/shrink. Kupanuka maana yake ni kutoka ktk kitovu cha jiji kwenda nje ya jiji.Endeleeni kuishi vumbini.

    ReplyDelete
  8. Mfichaficha maradhi kifo humuumbua! Hali kama hii inathibitisha jinsi wabongo tunavyofikiri na kutenda. Tu wajuzi wa mashairi na ngonjera huku ndani tukiwa tumejaa uonzo! Tunapenda sana kuonekana watanashati (tunavaa suti na tai - vazi linasisitizwa na utawala wa sasa)huku vichwani mwetu tunafikiri kiujimaujima!!!

    ReplyDelete
  9. Neema raymondApril 30, 2010

    Miaka nenda rudi hii barabara ya mikocheni inajaa maji. Ina maana maplanner wa jiji na engineers hawaioni au inakuwaje? Serikali yetu inaenda wapi? Hata mwaka wa uchaguzi basi wafanye walau kitu kidogo....Tanzania inatia aibu kwa kweli.....shame on you viongozi, mmejaa ubinafsi na ufisadi, hamfikirii wananchi wa kawaida hata siku moja!

    ReplyDelete
  10. Huu ni ukengewehu. Yaani jiji ambalo viongozi wote wa serikali wanaishi, linashindwa kukarabatiwa na kuhakikisha mitaro ipo na haijaziba na kwamba hali kama hii haitokea tena? Kweli CCM mmeshika PATAMU, hata hamkumbuki adha zinazowakumba walalahoi?

    ReplyDelete
  11. Mchangiaji wa kwanza, Kiingereza kibovu, sarufi ya kiingereza mbovu; kwani lazima uandike kiingereza kwenye blogu ya Kiswahili? Hujamsikia Waziri hapo juzi akisisitiza matumizi ya Kiswahili?

    Agh, umenichefua!

    ReplyDelete
  12. Watanzania inabidi tuelimike zaidi kwani maendeleo ya nchi sio mji kuwa na majumba mazuri tu au mtu kuwa na kazi nzuri tu.Miundombinu ndio nyenzo muhimu kama mtu utashindwa kufika kazini kwaajili ya mafuriko barabarani sioni ni jinsi gani tunaweza kuwa namaendeleo, au wakulima wakashindwa kusafirisha mazao yao.Serikali ya tanzania iko wapi? Watanzania amkeni uchaguzi unakuja fanyeni maamuzi yenye busara ili muweze kuondokewa na kero.

    ReplyDelete
  13. Hii ni hali ya kawaida popote duniani..mimi niko toronto..mvua ikinyesha mafuriko kila sehemu..na hivi sasa mwezi mzima kuna mgao wa umeme huku canada..bora huko bongo ndugu zangu..mliokuwepo huko bakini hukohuko maana hata mimi nina mpango wa kurudi nyumbani..nimechoka na haya mafuriko na mgao wa umeme wa huku..

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2010

    Wewe anony wa 8.20pm acha uwongo, Toronto ipi unayoishi wewe ambayo ina mgao wa umeme? Hebu weka basi hata article ya gazeti inayoonyesha mgao huo wa umeme maana kitu kama hiki ni big news kwa mji kama Toronto. Naishi Toronto pia sijasikia wala kuona mgao wowote wa umeme.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2010

    mmh! huo mgao wa umeme canada uko kipande ipi? makubwa leo duu jamaa anaota huyu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...