FFU wa ughaibuni a.k.a Ngoma Africa band watapiga kwata katika sherehe za washabiki wa Wold Cup 2010,huko Munchen aka Bayern,Munich May 8, 2010!
Onyesho litafanyika eneo la
Pfarrheim.St.Joseph,
Joseph Platz 1.
München
Wazee hawa wa kukaanga mbuyu wenye maskani yao huko Ujerumani wanatarajiwa kuwasili mjini Munich aka Muchen siku ya jumamosi ya 8 May 2010 kwa ajili ya kufanya onesho la shamra shamra ya Sherehe za kombe la kandanda la Dunia,ambalo kwa mara ya kwanza litafanyikia nchini Afrika Kusini aka Azania.
Wazee hawa wa kukaanga mbuyu wenye maskani yao huko Ujerumani wanatarajiwa kuwasili mjini Munich aka Muchen siku ya jumamosi ya 8 May 2010 kwa ajili ya kufanya onesho la shamra shamra ya Sherehe za kombe la kandanda la Dunia,ambalo kwa mara ya kwanza litafanyikia nchini Afrika Kusini aka Azania.
Shamra shamra hizo zimeandaliwa na jumuiya za Wafrika Mashirika yasio ya kiserekali pamoja na Chama cha urafiki kati ya Tanzania na Ujerumani.Sherehe hizo inasemekana zitaudhuriwa na mabalozi wa nchi mbali mbali.
Wakazi na washabiki wa mji wa Munich,ambako ndipo makao makuu ya klabu ya mashuhuri ya kandanda "Bayern,Munich" ,watapata bahati ya kusakata mziki wa dansi kutoka kwa mzimu wa dansi "The Ngoma Africa Band".
Bendi ambayo inasifa za tabia ya kupelekana mchaka mchaka na washabiki wake kwa kutumia mdundo wake wa dansi. Hebu cheki mwenyewe:
Bendi hiyo ni juzi tu waliachia singo CD yao iliyobeba jina la "Jakaya Kikwete 2010" na kufanikiwa kuteka washabiki lukuki katika youtube!
Karandinga la FFU wa Ngoma Africa band litahakikisha limewasili mapema mjini Munich aka Munchen ,huku likiwa na mabox ya kutosha yaliojaa virungu vya mziki, na magitaa kwa ajili ya ligwaride hilo.
Wadau wa Bayern kaeni tayari tayari kwa kusakata magoma mpaka asubuhi lakini hamna kukesha! Shotooooozzzzzzz GEUKA! Whaaaaam!
kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Temu
ambaye ndie mratibu wa tamasha hilo kwa
simu +49(0)179 6661748
simu +49(0)179 6661748
karibuni nyote!
Party ya kitoto hiyo mwisho ni saa 6 usiku tangu lini party ya ukweli ikafanyika ktk ukumbi wa kanisa wacheni kupenda dezo watu wa München
ReplyDeletenimecheka,,,
ReplyDeletesizani kama kuna paty ya kitoto Munchen,mpaka wamehamua kuwapa uwanja ffu!
ReplyDeletendio kusema kikisi cha FFU aka watoto wa mbwa kupiga ligwaride ndani ya Munich!kweli sasa wazee munich mmehamua!!!!!!!
ReplyDelete