JK akitoka katika nyumba ya familia ya Marehemu Evaristi Semeni(11) mmoja kati ya watoto watatu walifariki kwa ajali ya kugongwa na lori katika kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo,juzi jioni. JK alizitembelea familia za marehemu na kuwafariji.
Semeni pamoja na wenzake Ezekiel George Setumbi(13) mwanafunzi katika shule ya msingi Mboga wilayani Bagamoyo na Omari Mrisho aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Msoga walifariki dunia baada ya kugongwa jana saa moja na nusu jioni na lori aina ya Isuzu Tiper lenye usajili wa namba SM 2514 mali ya Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo lililokuwa likitoka Chalinze Kuelekea Msata.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Bwana Mohamed Mbwana amesema kuwa wakati wa ajali hiyo mtoto Ezekiel Setumbi alifariki papo hapo ambapo wenzake Evarist Semeni(11) na Omari Mrisho(13) walifariki wakati wakipata matibabu katika kituo cha afya Chalinze.
Kwa Mujibu wa Kamanda Mbwana Dereva wa lori hilo Lukino Kayela(40) mkazi wa Mji Mwema Bagamoyo amekamatwa na alitarajia kufikishwa mahakamani leo.Wanafunzi hao walifariki kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata kichwani.
JK akiifariji familia ya Marehemu Evaristi Semeni mtoto mwenye umri wa miaka 11 kumi na moja aliyefariki katika ajali ya kugongwa na gari juzi jioni katika kijiji cha Msoga ambapo yeye pamoja na watoto wengine wawili walifariki dunia.Semeni alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi Msoga.
JK akifika kutoa heshima za mwisho na kuifariji familia ya marehemu Omari Mrisho(13) aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Msoga ambaye yeye na wanafunzi wenzake wawili walifariki katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msoga jana.
JK akimfariji mzee Mrisho Omari mzazi wa Marehemu Omari Mrisho(13) katika kijiji cha Msoga jana.Omari(13) na wenzake wawili walifariki katika ajali ya gari jana jioni.
JK akiwafariji baadhi ya wakazi wa vijiji vya Msoga na Mboga wilayani Bagamoyo jana wakati wa mazishi ya wanafunzi watatu wa Shule za msingi Mboga na Msoga waliofariki kwa ajali ya gari juzi kijijini hapo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. KWELI JK MTU WA WATU.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi nawapa pole sana wafiwa wote kwani hiyo ni kazi ya Mungu!Naomba nieleze hisia zangu kwamba mara kwa mara namuona Mh.Rais akiwatembelea watu mbalimbali tena wanyonge na kuwapa pole kwa matatizo kama haya......binafsi sijawahi kuona Rais mwenye mapenzi na watu wake kama Mh.Kikwete ukiondoa hayati baba wa Taifa mwalimu Nyerere!Nampongeza sana Mh. Rais na naomba aendelee kutambua kwamba hiyo ndiyo maana halisi ya kuwa kiongozi wa watu bila kujali kipato cha watu husika.Nikiwa mtoto kutoka familia ya mkulima najisikia furaha sana kwa Mh.Rais wangu na namtakia kila la heri katika uchaguzi mkuu ujao!(Richard M.Mizambwa,masomoni Uholanzi(Masters Program),mizambwar@yahoo.com/Mizambwa.MBA26@msm.nl.).

    ReplyDelete
  3. poleni sana wafiwa inamaana aliwagonga bahati mbaya au? inabidi ashikishwe adabu huyo dereva.Hata ivyo kaka michu hukustahili kuweka hiyo picha waliokaa ndani inazidi kutudhalilisha tulivyo maskiniiiiiiii!!!!!!!!Otherwise jina la bwana lihimidiwe!

    ReplyDelete
  4. ANKAL ASANTE SANA KWA HIZI PICHA.

    LAKINI NAOMBA COMMENTS ZA WATU KUHUSU HIZI HABARI NA PICHA ZAKE USIWEKE KAPUNI TAFADHALI

    ReplyDelete
  5. Hapo ndio JK anapowapiga bao Maraisi waliomtangulia!!

    Keep it up Mr. President!!

    ReplyDelete
  6. HIVI RAIS WETU PAMOJA NA VIONGOZI WOTE ALIOAMBATANA NAO WANAFIKIRIA NINI KUHUSU MAISHA YA HAWA WATANZANIA?

    KARNE HII YA 21 KWELI WATANZANIA WANATAKIWA KUISHI KWENYE NYUMBA KAMA HIZI?

    ReplyDelete
  7. Kwa kweli sina mengi ya kusema, picha hizi zinaeleza mengi,lakini moja tuu Kikwete ni mtu wa watu...kataa usiakatae huu ndiyo ukweli....

    ReplyDelete
  8. HONGERA KIKWETE KWA KUWAPA POLE HAWA WATANZANIA MASKINI WA MUNGU.

    LAKINI NI VYEMA PIA KURUDI NYUMA NA KUTAFAKARI KWA MAKINI HALI HALISI YA MAISHA YAO NA JINSI GANI UFANYE KUWAONDOA KWENYE HIYO HALI.

    WATANZANIA HAWA NDIYO WALIKUWA NA MATUMANI YA MAISHA WAKATI WA UHURU, LAKINI SASA NI KARIBU MIAKA 50 IMEPITA. JE MATUMAINI YAO VIPI?

    HAWA NDIYO WANAOISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU. HIYO NYUMBA YAO NA WANAVYOONEKANA NI USHAHIDI.

    ReplyDelete
  9. Hivi hawa waheshimiwa wangepewa maji ya kunywa kwenye hii nyumba wangekunywa?

    ReplyDelete
  10. Tuachi siasa jamani. Wananchi wanaishi maisha ya hali ya chini sana.

    ReplyDelete
  11. 1.Jk,nampongeza kwa kushiriki mojakwa moja kwenye mambo ya jamii,hasa anapopata nafasi ya kufanya hivyo,hasa tukizingatia nafasi yake.Ni maraisi wachache walioweza kujichanganya kama yeye.
    2.Kale kawimbo kake ka ''MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA''nafikri amejionea mwenyewe,sijui mwaka huu atakaimba tena au Komba atamtungia kawimbo kengine,mmmmmmh yetu macho ngoja tusubiri.

    ReplyDelete
  12. Tanzania kila leo watu wanakufa kwenye ajali za barabarani. Hivi kuna magari mengi sana, kuna watu wengi sana, barabara ni mbovu, magari mabovu, wadereva wazembe, wananchi hawajui kutumia barabara, sheria hakuna au nini jamani)

    ReplyDelete
  13. Wafiwa na wote walioguswa na msiba huu, poleni sana. Mungu azilaze roho za marehemu wote watatu mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  14. Huyu President ni kiboko. Simply, A MAN OF THE PEOPLE. Nafikiri Kikwete urais unambana sana ili asichanganyike na watu.

    ReplyDelete
  15. Thanks Mr Michuzi for capturing this Emotional and yet a sad scene. But i am also so glad in the midst of this tragedy to see that we have a kind of a president who is so compassionate as take some time out of his obviously busy schedule to pay a visit to the bereaved families. Asante Sana Mh. Rais and God bless you!

    www.hacksglory.blogspot.com

    ReplyDelete
  16. Mh! haya mapya. Sikumbuki kuona tawira za aina hii, labda wakati wa nyerere. Hongera Kikwete kwa kufika mpaka Tanzania. Hii itakuwa changamoto kwako kushughulikia umaskini bila shaka. Utaweza kujionea kwamba nyumba ya nanihii kujengwa kwa Bil 1.2 ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi!!

    ReplyDelete
  17. JK: HIZO NYUMBA ZA HAO WATU UMEZIONA? Maisha yao umeyaona? Je First Lady wetu amewatembelea hao watu Tangu WAMA imeanzishwa? Je ufisadi unaonyamaziwa nchini hauwezi kuboresha maisha ya watu hawa japo kwa theluthi moja? TAFAKARI.
    Pole haisaidii chochote, yaweza kuwa kampeni tu. Ombi ni kukuona ukibadilika na kujaribu kuja na mikakati ya kuwakomboa waTanzania katika hali ngumu ya maisha. Pesa mtakusanya, lakini maisha mafupi. You better leave a GOOD LEGACY behind you, than amsaa welth that you can hardly go with in death. Please, please kumbuka tulikotoka!
    Yote tis, kumi, asante japo kwa kuwafariji
    Mungu azilaze mahali pema peponi roho zao, Ameni.

    ReplyDelete
  18. TUNASHUKURU MZEE UNASHUHUDIA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA NAFIKIRIA HIYO MIAKA 5 ULIYOBAKIZA YATAKUWA BORA MARADUFU

    ReplyDelete
  19. JK AMEJITAHIDI SANA, sasa nyie mnaosema hajatekeleza maisha bora kwa kila mtanzania, mlikuwa mnataka akawagawie watu pesa majumbani au. JK ameweka oportunities sasa niwatu kuzitumia. hebu jaribuni kuangalia na takwimu jinsi mambo yalivyo badilika tangu aingie madarakani.
    Kusema kweli amefanya jambo anahitaji pongezi atleast.

    ReplyDelete
  20. KWANZWA NINATOA POLE NYINGI KWA FAMILIA ILIYOPOTEZA WAPENDWA WAO MWENYEZI MUNGU AWAPE FARAJA NA MATUMAINI. PILI WAKATI WA UCHAGUZI UNAPOKARIBIA VIONGOZI WETU HUWA WANAFIKA UNREACHABLE PLACES NA KUJIONYESHA KWA WANANCHI KWAMBA WANAJALI NA WAPO PAMOJA NAO HASA KATIKA KIPINDI KIGUMU, LAKINI BAADA YA UCHAGUZI HAWAKANYAGI TENA MAENEO YA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA HALI NGUMU YA MAISHA! WANAISHIA MIJINI TU. HAPO NI WAZI KWAMBA KURA INATAFUTWA KWA UDI NA UVUMBA! ANKAL KWA VILE HII NI SEHEMU YA MAONI PLEASE USIITUPE KAPUNI HUU UJUMBE. I WILL KNOW HOW BIAS ARE YOU!

    ReplyDelete
  21. Mheshimiwa JK, kuna ajali ya pikipiki imetokea hapa kijiji cha Mtopwa, Mtwara mtoto mmoja kafariki, unasubiriwa uje ufariji wafiwa! Wewe ni raisi wetu wote, sio wa Bagamoyo na vijiji vyake.

    ReplyDelete
  22. HIVI JK KAMA KWELI UNAPENDA WATANZANIA NA KAMA UNATAKA WATANZANIA WAKUKUMBUKE KWANI NINI USIFANYA MAMBO YA MSINGI AMBAYO YANAWEZE KULETE CHACHU YA KUBADILISHA MAISHA YA WATANZANIA HAWA MASIKINI KABISA.

    KITU MUHIMU MH JK NI UONGOZI WA NCHI YETU. KWA MFUMO WETU WA UONGOZI WA SASA NI VIGUMU SANA KWA VIONGOZI WA KWELI KULETA MAENDELEO.

    ITISHA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU KATIBA NA MFUMO MZIMA WA UONGOZI WA NCHI ILI WANANCHI WATOE MAONI KUHUSU MSITAKABALI WA NCHI YAO. KATIBA NA MFUMO WA UONGOZI UNATAKIWA KUFANYIWA MABADILIKO MAKUBWA.

    ReplyDelete
  23. YOTE TISA LAKINI JAMANI, KUNA WATU MASKINI JAMANI, HEBU ONEN WALIVYOPAUKA HAO KINA MAMA HUMO NDANI. HIVI KWELI NI TANZANIA HAPO, PANATIA UCHUNGU HALAFU NDIO TENA WAMEMPOTEZA MTOT WAO AMBAE LABDANDIE ANGEKUJA KUWAJENGEA NYUMBA BOR. MMHH WADAU HEBU TUANZISHENI KAMCHANGO KA KUWAJENGEA HATA POLISI POSTI TU JAMANI. ROHO INANIUMA WAKATI WENGINE WANA MAGOROFA YA KUFA MTU HUKO MBEZI

    ReplyDelete
  24. JK, misiba ya/kwa Watanzania ipo kila sehemu na katika mazingira tofauti e.g. uporwaji wa mali za wananchi kupitia uchimbaji "haramu" wa madini, wizi wa kalamu na wezi wanaofahamika, kusota kwa wanafunzi (hasa watoto wadogo) katika kugombania usafiri na wakubwa ili wahudhurie masomo, utolewaji wa elimu isiyo na tija na fanaka kwa taifa (ikiambatana na kufeli kwingi), mifumo isiyofaa ya udhibiti mwendo na ulegevu wa mamlaka husika katika ufuatiliaji wa uvunjwaji wa sheria za barabarani, unyanyasaji wa kijinsia, matatizo ya kiafya na ugumu wa upatikanaji wa huduma stahili, shida za maji hasa vijijini, uwindwaji wa albino etc. Mtu akiaga dunia inakuwa ni matokeo tu ya mambo haya. Ukiwa kama msimamizi mkuu wa masuala yote haya na mengineyo, unajisikiaje? Mi nadhani una masuala mengi mazito ya kufanya katika kuimarisha mifumo mbali mbali ya maendeleo kwa ajili ya nchi na wananchi waliokutuma ili kuboresha na kuokoa maisha yao, tumia muda mwingi na nguvu nyingi katika hayo na sio katika matokeo. Ni vema na haki kuwafariji wafiwa, na Mungu akubariki kwa moyo ulionao, ila pengine ungemtuma mtu tu na wewe ungekuwa Shinyanga au Kilosa wakati huo. Misiba ni mingi nchini na dunia nzima, lakini kazi yako ni kubwa sana na ya kipekee, hivyo uwepo wako katika masuala nyeti ya kitaifa kwa ajili ya Watanzania ni muhimu zaidi.

    Naomba nisieleweke vibaya na wanafamilia waliofiwa na uma wa Watanzania kwa ujumla, ila najaribu tu kukumbusha (au pengine kuelewa) uzito wa majukumu ya Rais na vipaumbele kwa manufaa ya Watanzania na maisha yao.

    Samahani sana kama nimekukera Mheshimiwa Rais na Watanzania wenzangu, ila naguswa sana na sababu za vifo na uwezo wa Rais katika kudhibiti vifo visivyo vya lazima nchini (viwe vya ghafla au vya muda mrefu).

    Poleni sana ndugu wafiwa na Watanzania kwa ujumla katika matatizo yote magumu myapitiayo kila kukicha. Mungu awabariki, awaongoze na kuwalinda siku zote.

    ReplyDelete
  25. Mr President,

    Kuhani tu hakutoshi. Please, do something. Watu tunateketea.

    Kalikali

    ReplyDelete
  26. Afadhali Mr President ana GUM BOOT.

    ReplyDelete
  27. Hiyo ni kampeni hamna lolote mbona hapa DAR waliolaliwa na trellar hatukumuona Rais wala diwani changa la macho!Kampani zimeanza tutaona mengi....!

    ReplyDelete
  28. Poleni sana wafiwa inasikitisha sana.Jamani kikwete nimekukubali siio siri unaimani kwa watu hasa wenye shida naamini ungekuwa na uwezo wa kuboresha maisha ya watu wote kwa haraka ungefanya hivyo,lakini nakuombea tu na utazidi kupata dhawabu kwa imani yako.
    nakupenda sana raisi wangu.
    zamda

    ReplyDelete
  29. Kwanza kabisa ninatoa pole kwa wafiwa kutokana na msiba wa watoto waliopoteza maisha kwa ajali ya kugongwa na gari.

    Pili, sina budi kumpongeza Mh. Rais kwa kuweza kufika msibani na kuwafariji wafiwa. Ninatambua kuwa Rais ana kazi nyingi lakini leo hii hizi picha zinaonesha kuwa pamoja na ratiba ngumu ya kazi ya urais lakini hili jambo la kuwafariji wananchi limepewa kipaumbele katika majukumu ya kazi zake.

    Tatu, mimi ninaishi hapa US kwa miaka mingi, serikali ya hapa inachokifanya ni kutengeneza nafasi (opportunities) kwa ajili ya wananchi wake wazitumie (utilize). Serikali ya US kwa takriban miongo kadhaa iliweka mazingira hayo ambayo leo wanaofaidika sana ni wale ambao wanazitumia fursa hizo. Kuna baadhi hawakuzitumia fursa zilizopo na wanaishi katika maisha ya umasikini kwa miaka mingi na hata wengine hawana mahali pa kulala. Umasikini wa hapa ni mbaya kuliko umasikini wa nyumbani. Masikini wa nyumbani amezungukwa na ardhi yake mwenyewe.
    Mwisho, ninawasihi watanzania wote kuchukua fursa zilizopo kujiletea maendeleo kwani yale yaliyokuwa yameanzishwa baada ya uhuru kuwa serikali ndiyo mhimili wa rizki ya kila mtanzania leo hii tumeshuhudia si kweli, kwani serikali haiwezi kuwanyia kila kitu, kuwajengea nyumba, kuwalimia mashamba yao, kuwachungia mifugo yao, kuwaletea vyakula hadi majumbani mwao, nk.
    Tuamke tujiletee maisha bora kwa kila mtanzania

    ReplyDelete
  30. Watanzania jukumu la kujenga nchi ni la wananchi wote si JK peke yake. Nimeona maoni huko juu watu wanalaumu hali mbaya ya uchumi na kupeleka lawama kwa JK yeye ni mmoja tu kati ya watanzania zaidi ya milioni 40. Naomba tubadilike na kuangaika kuleta maendeleo ya nchi yetu na si kulaumu viongozi. Wengi wetu tuna roho ya chuki na ubinafsi ingawa machoni tunachekeana, kazi yetu ni kuponda tu serikali. Kiulize ww kama mwananchi umeifanyia nn jamii maskini nchini tunabadilisha magari ya kifahari mjini na kujaza foleni wakati wazazi wetu vijijini hawana pa kulala

    Tuamke tuchangie shule za kata na kusaidia kuinua kilimo ambacho ndicho mkombozi wa wanyonge tununue bidhaa za Tz ili tukuze viwanda vyetu na wabeba boksi mkumbuke nchi yenu kwa kila hali sio kuponda tu

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  31. Poleni wafiwa. ajali hizi zithibitiwe.

    Kwamba JK ni mtu wa Watu hilo halina ubishi na hakuanza leo wala jana na anajali utu wa mtu kama mtu.
    Nimependa rangi ya Gam-buti za Mheshimiwa.

    ReplyDelete
  32. We mdau wa usa usione kama umesha yapatia unataka kuniambia umasiki wa nyumbani tz ni wa kujitakia au mzee wa watu hapo juu akuweza kuyatumia mazingira yalio wekwa na serekari ya tz we usiwatukane watu wewe kwanza utafananishaje usa na tanzania yani unaringanisha usingizi na kifo du we kweli umeondoka tz siku nyingi na si zani kama umesha wai kwenda tz toka uondoke . mazingira gani ulio yaona wewe tz yamewekwa vizuli kwa ajili ya wananchi . usitake kutuingiza kwenye siasa sisi sio wana siasa ila ni utaifa na hari ya wananchi wengi wa tz pamoja na ukiringanisha na ali alisi ya picha apo juu ndio maana watu wengi wameshindwa kuvumilia na kutokwa na maneno mengi . mimi Naamini na si zani kama watu wana mchukia mueshimiwa raisi ila wameona ni mahali pazuli kwa raisi kujalibu kumkumbusha ali nzuli ya maisha kwa kira mtz na maisha yenyewe ndio kama hayo hapo juu kwenye picha au ? au we unataka kwenda tz kugombea nafasi yoyote nini ? du tanzania ni kiboko yani mtu mmoja gavana maisha yake yana samani kuliko mamilion ya watu du ni kiboko .

    ReplyDelete
  33. yaani sina ka kusema , nimefurahi ndani ya moyo wangu kumuona rais akijali wananchi wake , yaani piga ua kikwete unayo kura yangu ....

    ReplyDelete
  34. Ama kweli Afrika watu wanapendana sana hata kama kuna unyonyaji na rushwa na ubadhirifu. Sehemu ingine wangempiga mawe mkuu wao na kumlaumu angalia tunavyoteseka nyie mnatembea na Limo za BMW na kusafiri na First Class na kukaa kwenye mahoteli makubwa mkiwa nje. Shukran mungu ibariki Afrika na watu wake, wabariki pia viongozi dumisha umoja. Tuwe wakweli na tusiwe na unafiki wowote kuhusu umaskini na shida za watu wenye kipato duni mno.Sote ni wamoja na umaskini wao ni wetu wote kama taifa! Inatia uchungu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...