Kutoka kulia ni Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Dr Kafumu,Muongozaji wa Kipindi Sebastian Maganga,Barbra Hassan,Paul James pamoja na Gerald Hando wakiwa Live asubuhi ndani ya hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk. Clouds Fm 88.4 kupitia kipindi chake cha Power Breakfast wakizungumza Live sasa hivi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk (Frame tree Lounge) na Kamishna wa madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Dr.D.P Kafumu ,kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya madini ikiwemo na sheria yetu mpya ya madini ambayo baadhi ya watu wamekuwa na walakini nayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Interview ilikuwa nzuri sana. Kamishna amefanya kazi nzuri sana kuelimisha watu wasiokuwa na uelewa na suala la madini - yaani watu wanachukulia sekta ya madini ki siasa zaidi.

    ReplyDelete
  2. na kamishna uwe unasema iyo risechi ya watu mlioongea nao ni wapi!!maana nikinukuu statement yako leo asubuhi POWER BREKFAST umesema kila mtanzania alipitiwa kuulizwa hii ishi ya madini!!si kweli na maofisi mengi na vyuo vingi tu havijapitiwa...

    sorry to say hapa tulipo hatujawai ona hao watu na tumefanya kusikia hii bill bungeni,upo hapo??

    2.naamini hiyo sheria tutaipata ili kusoma katika website za serikali ili tujue kilichomo umo

    3.tafadhali michuzi ebu tuwekee kwa dondoo point zilizomo umo ktk sheria hii mpya

    hope hii sheria imetulia/itusaidie angalau

    ReplyDelete
  3. Naomba kujua, sababu ya interview hiyo kufanyikia kempinski na sio clouds au wizarani.

    ReplyDelete
  4. Sali zuri anon wa Fri Apr 30, 10:01:00 AM

    Huu ndio ufahari ambao Raisi Kagame anaupiga vita kule Rwanda.

    ReplyDelete
  5. Ankal, hii Radio station ilianza kihuni tu but ina viongozi makini sana. pamoja na kwamba wako kisocial zaidi lakini wana habari muhimu mno na ni wabunifu sana katika kufikisha ujumbe. kwenda Kempinky au popote sio hoja ya msingi, hawa hawtumii hela ya serikali, ya wizara au ya kwako. watu wajue kuwa kamishna kaalikwa tu kuongea kwenye kipindi na sio kamishna ndio kawaalika Clouds hotelini. ingekuwa hivyo angewaita waandishi wote.

    wewe Anony wa 10:01:00 AM ni nani kuhoji Clouds wanatumiaje hela zao.ndio nyie kama wangefanyia kipindi Tandale uwanja wa fisi mnadanganyika kilaini kwamba wanawajali watu wa chini.

    ReplyDelete
  6. naomba nifahamishwe why kempensiki, mantiki ninijamani watanzania tu walimbukeni. laura

    ReplyDelete
  7. Ankal
    Mimi najali mantiki ya kipindi yaani kutoa elimu kwa jamii, popote pangefaa ili mradi azma imetimia, mimi ningependa kujua pamoja na maelezo ya Kamishna Dr. Kafumu je nini kimesababisha muswada upelekwe Bungeni kwa HATI YA DHARURA? Kuna dharura gani hapa?????Dr. Kafumu atusaidie kidogo hapa!!!!!!!!!!
    Asante sana

    ReplyDelete
  8. Hivi mmeshasikiliza Morning Magic ya Magic FM...92.9? Wale jamaa wako njema na serious in issues discussion/analysis/follow up kuzidi Clouds FM. Big up Morning Magic...Mr Orest Kawau, Abdallah Ramadhani na Mishi.

    ReplyDelete
  9. Mama Makani (Bite)April 30, 2010

    Big ups Clouds ... huo ni ubunifu wa hali ya juu. Muendelee na watu wengine katika maswala ambayo watu yanatuchanganya kama vile DAWASCO TANESCO na Halmashuri za jiji la DSM. Jamani tuliomba calendar hali leo hatujaletewa licha ya kuandika msg kwa bonge. Mimi ni mama ushauri DSM

    ReplyDelete
  10. WADAU,

    HII SHERIA MPYA YA MADINI HAITAKUWA NA MAANA SANA KWA WANANCHI KAMA HOJA ALIYOITOA MHESHIMIWA SITA, SPIKA WA BUNGE, HAITAJUMUISHWA NA KUWA SEHEMU YA SHERIA.

    HOJA YA SITA INAHUSU FIDIA. LIPO TATIZO KUBWA SANA KUHUSU FIDIA KWA MWANANCHIU ANAYEONDOLEWA ENEO LENYE MADINI. SERIKALI AMA KUTOKUJUA AU SIJUI NAMNA GANI VILE WANARIDHIKA KABISA NA FIDIA DHALIMU WANAYOPEWA WENYEJI.

    ANGALIA, UNAISHI KWENYE ENEO LA MADINI AMBALO THAMANI YAKE NI KARIBIA, KWA MFANO, DOLA MILIONI 300 AMBAZO ZINAWEZA KUPATIKANA KWA UCHIMBAJI WA MIAKA 3. UNAPOHAMISHWA FIDIA YAKO INAKUWA NI THAMANI YA MIPAPAI, MAEMBE, MAPERA, VINYUMBA NA MAKABURI YAANI MAENDELEZO JUU YA ARDHI KWA THAMANI AMBAYO MARA NYINGI HAIFIKII HATA 0.001% YA THAMANI YA ENEO.

    MAISHA BORA WANAYOANDALIWA WANANCHI NI YEPI??

    SASA CHA AJABU, SERIKALI WANAMUUZIA MUWEKEZAJI 100% BILA WAO KUCHUKUA SEHEMU YOYOTE YA THAMANI YA HAYO MADINI KWA KUTEGEMEA KUPATA KODI PEKEE.

    TUNAENDA KWELI?, TUTAFIKA??

    ReplyDelete
  11. Kuhusu hilo suala la wanaohamishwa kulipwa fidia ya mipapai na majengo etc, nadhani ni kwa vile madini yaliyoko chini ya ardhi ni mali ya Serikali, ama? Mmiliki wa ardhi yeye ana haki ya makazi na vyote vilivyopo juu ya ardhi, vilivyopo chini ya ardhi ni mali ya Serikali, ama? Occupants have surface rights only, everything of value beneath belong to the State. The State has sub-surface rights, ama? Hivyo serikali ina haki ya kukuhamisha pindi watafiti waki-strike gold na madini mengine, hata kama una hati halali. Same applies kama wataalam wakigundua mafuta au gesi. Wataalam tusaidieni hapo.

    ReplyDelete
  12. Jamani mliouliza why Kempinski hapo juu inawezekana Clouds wanafanya deal yakuitangaza Kempinski pia na hiyo ni makubaliana yao na Kempinski kwahiyo mi sioni ni tatizo kwani sio government/kodi zinagharamikia. Wakati muingine ukitaka kudhamini kitu au kufanya promo ya mahali inabidi uwe mbunifu. I think that is part of marketing strategies za pande zote mbili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...