Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Je suala la neno matakwa nalo ni kosa?Mzizi wa neno ni taka au tako kutaka...je yaweza ikawa matako yangu au mataka yangu?yaani mahitajio yangu?

    ReplyDelete
  2. Michuzi,

    Mtaalamu wako ana matatizo mawili.
    Kwanza Kiswahili kama ulivyo wewe sio lugha ya kwanza kwahiyo ana matatizo ya kupata matamshi ya "la".

    Pili mtaalamu wako anataka watu wazungumze Kiswahili cha vitabuni. Ni sawasawa na mimi nisome Kizaramu kisha niende nikawaambie wazaramu kuwa Kizaramu chenukina matatizo kwasababu hakiendani na utaratibu wa Kisarufi ya Kibantu. Nafikiri lugha ni suala la mawasiliano.Hakuna polisi ambae hataelewa ukimwambia kuwa Mimi nimeibiwa gari langu. Hii ni njia ya watu wanaojifanya kuwa ni wataalamu wa Kiswahili kupata ulaji kwa kutaka kutengeneza ugumu ili wasemaje wa Kiswahili wa awali kwa mfano Zanzibar waonekane kuwa hawasemi Kiswahili safi. Hii ni sawa na watu wa Rwanda wakataka kuwakosoa wafaransa kwenye kifaransa chao.
    Naona wataalamu wanatupotezea muda kwa kutafuta umaarufu na ulaji.

    ReplyDelete
  3. Huyu mtaalamu anatumia nadharia za kimapokeo za uchambuzi wa sarufi, isimu kwa jumla, na hata semantikia. Nadharia ya matumizi ya lugha itakupatia majibu tofauti, na kwa hakika itakwambia kuwa "nimeibiwa" gari ni sahihi kabisa (hilo neno limezidi mipaka ya sarufi anayoongelea) na 'mgombea mwenza' ni sahihi kabisa (na hilo limevuka mipaka "mke mwenza", dhana ambayo ninafikiri ndio imemwongoza kuona 'mwenza' ni sawa na 'mshindani'. Kwa hakika 'uke wenza' huwa sio ushindani bali ni 'ukamilishani'.

    ReplyDelete
  4. Katumia neno wamechukuwa kuchukuwa si kuiba sindio? kwahiyo hawajaiba wamechukuwa mtaalamu hajaongea sahihi.

    ReplyDelete
  5. Nikikuambia "inaonekana unamtako wa ufuzi" utanipa za uso au utanielewa, yaani "inaonekana unataka kufua"? Giswahili zidum! JIBU: zidum...!

    Unajua ubora wa lugha yetu ni kwamba kila unachoongea unaeleweka tu, ila inategemea unaelewekaje...hivyo cha msingi ni kutoa madokezo kuhusu upotoshwaji wa maana. Ndugu yangu mmoja kutoka Shinyanga alishawahi kula za uso hapo kwa Likuvi kwa kutoeleweka tu, ila alikuwa na maana nzuri kabisa. Niliingilia kati na kumuuliza aliyetembeza kichapo kuwa "ningekuambia maneno hayo hayo miaka ya 80 au mwanzoni mwa 90 ungenielewaje?" Ndipo jamaa akaomba msamaa kwa kusema kuwa yeye alielewa vingine.

    Hivi Kiswahili kina tabia gani hiki lakini, au ni sisi watumiaji ndio tuna vitabia na vijitabia???

    Mdau wa Canada.

    ReplyDelete
  6. Kuhusu mgombea mwenza kachemka. Wanamwita mgombeamwenza kwa sababu kama jambo lolote likitokea basi mgombeamwenza anachukua madaraka.

    ReplyDelete
  7. Huyu anonimas ni jinias kama mimi. Amefumua bonge la pwenti. yaan wa2 wanataka kujizolea umaarufu na kaulaji2 wala c ki2 kingine.

    ilo jamaa taalamu linashupaa, yaan na misuli yote nje eti m2 akisema kaibiwa gari angemkamata na kuweka ndani iwapo angekuwa polisi. Basi ndio mana Mungu kakuepusha na kibarua hicho, yaan ungekuwa hivyo hiyo. na unataka ku2mia udikteta wako huo kuwalazimisha wa2 waseme unavyotaka weye, alaaa! Cjui utavuna wangapi.

    hii luga sote twaijua, ha2hitaji wataalamu wala nini. kazi zinaenda, na siku pia zinaenda bila ya kuwepo wewe ndugu mtaalamu. Unataka kupotezea wa2 muda wao bure tu kwa kuwakomfyuzi.

    sana sana nakushauri uanzishe lugha yako, afu uwaadhibu watakaokiuka amri za matumizi ya lugha yako. vinginevyo, anzisha biashara nyingine ya kukuwezesha kupata kipato

    ReplyDelete
  8. The mtaalam is right. Nimependa tafsiri zake ni za kitaalam zaidi. Tunalazimisha kiswahili.

    Its ok tunavyoongea kwa maana ya mawasiliano but ukifikilia outside the box ninaungana na huyo mtaalam.

    ReplyDelete
  9. michu mnaongelea aya mahojiano na mnajiweka YUTUBE breakpoint BAR??au bar gani ilo

    kazzz kweli

    ReplyDelete
  10. Mimi nadhani mtaalamu yuko sahihi kabisa sambamba na mifano aliyotoa. Labdal la msingi hapa, ni kuangalia maneno haya yanatumika katika kusudio lipo. Yaani tafsiri sahihi itatokana na kiini cha hoja yenyewe inazungumzia nini. Kwa mfano wa gari, katika uhalisia wa maana ya matumizi katika hoja nzima ya gari, yuko sahihi ukipeleka katika hali ya kuripoti au kutoa taarifa. Ukirudi katika hali ya kutendewa, ilipaswa kusema gari langu limeibwa.

    Lakini tuangalie kwa upande mwingine. Je, utaelewaje mtu akisema kaka yangu amenipigia simu? Ina maana kaka yako amepiga simu kwa niaba yako au amefanya mawasiliano nawe kwa njia ya simu? Mimi nadhni hapa inaeleweka kuwa kaka amefanya mawsiliano kwa njia ya simu. Kwa jinsi hii ndiyo maana nikasema, maneno hueleweka katika dhana hitajika, katika mazungumzo gani.

    Kwa namna hiyo, sipendi kabisa kuleta ubishi wa kumpinga mtaalamu, kwani kwa mifano yote aliyotoa yoko sahihi. Tatizo baadhi yetu watanzania hatutaki kukosolewa wala kuelimishwa.

    Kwa mfano katika dhana ya mgombea, hasa kwa mfano huu wa urais, lazima tuangalie kusudio ni nini? Nini maana ya kile kinachogombewa. Je, kuna kushiriki kwa pamoja katika kumiliki? Jibu hapana. Hivyo lengo pale ni kupata, na watakaji ni wale wanaohitaji tu kuwa katika nafasi ile. Na ukipata hata yule mwambata wako hatakuwa wewe uliyepata, yaani kwa maneno mengine haitwi rais huyu; anaitwa makamu. Kwa hali na jinsi yoyte ile hawi rais kwa kipindi kile chote. Rais atabaki kuwa rais na makamu atabaki kuwa makamu. Kwa jinsi hii wagombea pale ni wale wa pande tofauti, na hawa ndiyo tunawaita wagombea wenza. Wanagombea kitu kila mmoja anachokihitaji. Huyu aliye na mwingine kwa umoja wao hahitaji urais, hivyo hagombei kuwa rais. Wagombea lazima wawe na nia ya kukitaka kile kinachogombewa.

    Mfano mwaka 2005 Kikwete alikuwa na wagombea wenzake akina Lipumba wa CUF, Mbowe wa CHADEMA na wengine wa vyama pinzni kwa majina yao waliosimama kugombea kiti cha urais sambamba na vyama vyao.

    Upo mfano ambao mngeweza kumpinga kama angekataa na kusema ni kosa kusema mke mwenza; maana mke mwenza ni yule anayeshiki pamoja mume mmoja. Hawa wawili ni wenza katika mume mmoja. Kila mmoja anayo amri na mamlaka kwa mume yule. Ukielewa maana ya amri na mamlaka katika mfano huu mke mwenza, basi nadhani utaona tofauti iliko katika mgombea mwenza. Unahitaji kuzama kwa kina katika hili. Lakini tatizo ni lile lie la watu kurahisisha jambo. Ona ananimous mmoja anadiriki kulifikisha jambo hili katika hatua ya kumwona mtoa hoja kuwa mtesaji. amefananisha na mtu ambaye anakwenda kuripoti polisi kuwa amefanya kosa sambamba na maana na tafsiri halisi ya sentensi au maneno.

    Jamani tusipinge tu kwa vile kuna neno kupinga na hivyo kutaka kuhalalisha kutumika hata kama hakuna sababu ya kulitumia. Nomba tupende kujifunza na kufundishika, na siyo kuzoea kushutumu tu!!

    Mpenda kujifunza.

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi, asante maana hakika tnaelimika kupitia katika blogo hii ya jamii, ingawa wengine hawapendi kabisa kufundishwa au kuelimishwa.

    Tukubali kuwa kuna semi rahisi na gumu, na ndiyo maana kukawepo neno kutafsiri yale yanayoonekana kuwa ni magumu kwa wengine. Na huku ndiyo kufundisha na kufundishwa. Lengo ni kutaka watu waache kufanya makosa ya matumizi ya maneno yasiyo sahihi. Sasa inpotokea mtu anachukuwa nafasi ya kutuelimisha, tuwe tayari kujifunza.

    Mimi nakubaliana na mtaalamu kwa neno mgombea mwenza. Kwanza tufahamu kuwa neno kugombea ni kushindania. Hivyo sidhani kama ni kweli kuwa watu wa upande mmoja, wenye nia moja kusudio moja wanaweza kugombea (kushindana)!! Mshindani ni yule wa upande mwingine anayekitaka kukipata kile kitu.

    Hivyo basi, si sahihi kusema Dr. Shein alikuwa mgombea mwenza wa JK katika mwaka 2005. Haya makosa rahisi sana yanayoweza kukubalika na wengi kwa wepesi bila kuzingatia dhana. Najua tulitumia na tunatumia. lakini tujue kuwa tunafanya makosa. Si matumizi sahihi kabisa. Wagombea wenza ni wale waliokuwa wakishindanisha sera zao kukubalika kwa watu ili waweze kukubalika na kuchaguliwa.

    Swali, Dr Shein alikuwa ananadi nini kinyume cha Kikwete? Alikuwa ananadi sera za CCM ili Kikwete akubalike na yeye awe makamu wake, basi na si vinginevyo. Sasa je! utamwita mgombea mwenza au mshirika? Lugha rahisi ni mwambata, Na hivyo anapaswa kuitwa mgombea mwambata. Ukweli ni huu, hata kama tutashupaza shingo, tukubali kuwa tulikuwa tunafanya makosa. Shein ni mwana CCM mwenza wa Kikwete, ni kweli maana hawapingani katika chama hawa. Lakini inapofikia kugombea, hawagombei hawa.

    Lakini, JK ndani ya CCM alikuwa na wagombea wenza katika chama kupata nafasi ya kuwakilisha chama katika kugombea kiti cha urais, nao walikuwa akina Salimu A. Salimu, Mark Mwandyosa, na wale wote ambao walikuwapo katika mchujo ule.

    Nadhani hapa katika dhana ya mgombea mwenza imeeleweka. Na hivyo mtaalamu wa kiswahili yuko sahihi.
    Lazima tukubali, wapo wataalamu wa lugha, ubishi wa nini?

    ReplyDelete
  12. MBWEGELEMBWEGELEApril 30, 2010

    KUNA LUGHA, NA SANAA YA LUGHA . IKINYAMBULISHA MANENO KWA STAILI YA HUYU BWANA MTAALAM BASI UNAPOTOKA .

    JAMII KONGWE KAMA CHINA WANA KICHINA CHA KISASA NA CHA ZAMANI , WAONGEAJI WOTE WANAPATIA TU.

    LABDA NIMWULIZE HUYU BWANA NA WEWE MICHUZI UNIFIKISHIE SWALI HILI KWAKE. ...kABLA HATUJAPATA USTAARABU WA POSTA, NENO BAHASHA LILIKUWA LINATUMIKAJE . JE MTU ATAYETUMIA NENO HILO KIZAMANI MTAMWAMBIA YEYE HAJUI LUGHA ?

    INAPENDEZA KUONA WATU KAMA HAWA WAKIFANYA JUHUDI ZA KUKUZA KISWAHILI, ILA WATAMBUE ASILI NA MISINGI YA LUGHA YETU .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...