MAHAKAMA NCHINI ZITAENDELEA KUTUMIA LUGHA YA KIINGLISHI LICHA YA WARAKA WA SERIKALI KUTAKA KILA IDARA YA SERIKALI IWE INATUMIA KIMATUMBI KATIKA SHUGHULI ZAKE.
JAJI MKUU MH. AUGUSTINO RAMADHANI AMESEMA LEO MJINI IRINGA KWAMBA WAO MAHAKAMA KAMA TAASISI INAYOFUATA SHERIA WATAFUATA MAELEKEZO KWA MUJIBU WA SHERIA ILIYOPO AMA ITAYOWEKWA NA SI KUFUATA WARAKA.
"SISI KAMA MAHAKAMA TUNAFANYA KAZI KWA KUFUATA SHERIA SIO WARAKA"ALISEMA JAJI MKUU, KWENYA HAFLA YA MASHINDANO YA VITIVO VYA SHERIA VYA VYUO VIKUU ILIYOFANYIKA CHUO KIKUU CHA RUAHA.
WIKI ILIYOPITA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO MH. GEORGE MKUCHIKA ALITOA WARAKA BUNGENI KUTAKA KILA IDARA YA SERIKALI KUENDESHA SHUGHULI ZAKE KWA KIMATUMBI, JAMBO AMBALO LILIPOKELEWA KWA HISIA TOFAUTI NA WADAU WENGI WAKISEMA HII NI HATUA NZURI KUKUZA KISWAHILI.
WENGINE WAMEBEZA WARAKA HUO KWA KUSEMA UTAIFANYA TANZANIA KUBAKI KISIWA KWANI KWENYE MASUALA YA KIMATAIFA AMBAPO KINATUMIKA KIMOMBO, NCHI HII ITAACHWA NYUMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. MMEJIBIWA
    The Tanzanian government is chirping loudly over the BAE scandal and the fact that the 46 million US dollar fine to be remitted back to Tanzania will be given to charitable organisations and not the Tanzanian government.

    So incensed is the Tanzanian government, that Bernard Membe, Minister of Foreign Affairs is reportedly sending a team of senior officials to London to negotiate the release of the money directly to central government.

    If indeed Mr. Membe’s plea is successful, this will mean that corrupt Tanzanian Ministers will be rewarded twice for their corruption taking corruption in Tanzania to an ingenious and uniquly high level, even for Africa!

    The Tanzanian government’s newspaper the Daily News, reported yesterday that Britain should return the money to central government suggesting any other course would be akin to conduct used by the British to colonise Tanzania and plunder it’s resources. It further suggested that the charities to which the money would be paid over would be British and ‘a perfect ploy to ensure the money returns to Britain’.

    The Daily News accuses Briton of arrogance and states ‘’ We think Mr Membe has made it abundantly clear that Britain has no right to impose conditions for the return of the money stolen from the Tanzania government ….the two countries enjoy cordial relations built on mutual respect and there is absolutely no reason for London to rock the boat’.

    Bizarrely, the Tanzanian government appear to be suggesting that the returning funds were stolen from the Tanzanian government. Let us be clear what these funds represent. The funds represent a bribe paid to the Tanzanian government, nothing more or nothing less. Those who accepted the bribe within the Tanzanian government have not been named or dealt with in accordance with Tanzanian law and there appears to be no investigation proceeding in this respect.

    Until such time as the Tanzanian government are prepared to be self effacing about the situation and publicly expose the Tanzanian Ministers involved in the corruption in this case then it may be more prudent of Mr. Member to simply be grateful that the money is being returned in any form!

    It is debatable whose arrogance is involved here. In any event, let us please be spared the colonial clap trap.

    ReplyDelete
  2. Doh! Mbona wanatutafutia sababu sie wengine? Hii haijatulia hata kidogo, kiingilish mahakamani? Sijui itakuwaje? Tupo hati hati. Au kwa vile sie ni ma-learned brothers and sisters?

    ReplyDelete
  3. SERIKALI YA TANZANIA HAIKUFANYA JUHUDI ZOZOTE KWA KUPATIKANA KWA PESA HIZO ZAIDI WALIENDELA KULINDANA, KWANZA NI HURUMA TU YA WAINGEREZA KURUDISHA PESA HIYO TANZANIA HAMNA SHERIA YOYOTE INAYOWALAZIMISHA WA KULETA PESA HIZO ZA FAINI TANZANIA WANAWEZA KUZIACHA HAPA UK NA KUZIPATIA CHARITY NYINGI TU HAPA. KINACHPFANYIKA HAPA NI SERIKALI WANATAKA HIZO PESA WAZITAVUNE TENA, KAMA MULIZITAKA KWA NINI HAMKUZIFUATILIA BEFORE, WAWAJIBISHENI WALIOZITAVUNA WAZILIRUDISHE SI UK. HII NI ISSUE INATAKIWA IZUNGUMZWE NA WATANZANIA WOTE.

    ReplyDelete
  4. The World Economic Forum mwezi ujao Dar. hebu tuwaone wataongea kiswahili. Huyo Waziri wa Habari mwenyewe hata siku moja hajakutana na waandishi wa kigeni. Yamemshinda sasa ataka wote tume mbumbumbu!!! Hebu wasiturudishe nyuma. Hongera Jaji Mkuu.

    ReplyDelete
  5. NENDA UENDAKO GLOBAL ENGLISH NI TOP

    ReplyDelete
  6. Hata CHINA expoter namba wani duniani bidhaa zake zote zinaandikwa kwa kiinglishi hicho kimatumbi hakina misamiati ya kutosha

    ReplyDelete
  7. HIGH COURT NEVER KISWAHILI POLENI MNAPIGANIA LUGHA YA LOCAL

    ReplyDelete
  8. Guys,

    this government leaders are pulling us back...As everybody knows,English is a lingua franca...I am wondering while others like Rwanda,China etc go forward 10 steps we Tanzania we are backpedaling. What make me wonder is that,those who make such a decisions are the one who use our tax money to educate their child in abrod,where English is a major means of communication. Hell no,this is in-tolerate and heaven forbid....!!!!!

    hey you leades,EAC is on the way..where do you guys want to put Tanzanian citizen in this race...Kiswahili,yes but cutting out English usage in day to day activities...You are killing us....Imagine I am a master degree holder from UD and yet my English isnt persuasive....where else I can keep practice if you will let it go.....

    As the adage said..."You sow what you reap"....this decision will turn us Tanzania to a shadow to Kenyan and Ugandan. They will come to our land and grab all foreigner opportunities available there...Come on Mkuchika...your killing the country...

    ReplyDelete
  9. Huyu Jaji Mkuu kweli ameenda Shule...Mahakama ni Mhimili Huru, tangu lini Serikali ikapata madaraka ya kuiambia itumie lugha hii au ile. Serikali ilitakiwa ipeleke Sheria Bungeni, bunge lipitishe na kisha Raisi aweke Sahihi. Hapo ndipo Mahakama inatii kwa sababu imeshakuwa Sheria.

    Sio waziri tu anaamua kujitafutia umaarufu na kusema Mahakama ifanye hivi au vile.

    Mahakama kazi yake ni kusimamia Sheria na si vingenevyo. Leo hii wakianza kusimamia Waraka, tutakuwa tunaelekea kubaya.

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  10. Anon 26: 04: 03: 00, hiyo ngeli yako haijakaa ki-UDSM UDSM. You can't possibly be a graduate from that Uni. Tumegoma. Ungeandika tu kwa kiswahili. Ngeli yako imekaa ki-Nalitolela Nalitolela, if you know what I mean. Ila una vijihoja vya msingi katika ujumbe wako.

    ReplyDelete
  11. Wewe mdau wa Sun Apr 25 11:41 unaesema High Court Never Kiswahili ndio nini?

    Ni nani anaesomewa zile hukumu, kuna Mwingereza pale? Mfano ile kesi ya Zombe waliokuwepo pale walikuwa ni Waswahili watupu na Jaji anasoma mahukumu yake kwa masaa matano bila ya asilimia 99 kuelewa nini kinaongelewa. Sasa hiyo kwa manufaa ya nani? Au kijijini mtu amehukumiwa lakini maelezo yameandikwa kwa kiingereza, na kiingereza wenyewe ni Mhhhhhhhhhhhhhh! Sasa hiyo ni kwa faida ya nani?

    Wacheni ukoloni mamboleo huo hautawafikisha mbali

    ReplyDelete
  12. Candid ScopeApril 26, 2010

    THANA MUHIMU HAPA NI UJUMBE MUHIMU KATIKA MAWASILIANO UELEWEKE KWA WATANZANIA WOTE MILIONI KARIBU 40 NA SI KWA WACHACHE WANAOJUA LUGHA YA KIINGEREZA.
    MAHAKAMA ZINAENDESHA MASHAURI YA RAIA WA TANZANIA WANAOFAHAMU LUGHA YA KISWAHILI, SASA MAHAKAMA INAPOGEUKIA KUENDESHA LUGHA YA UK WAKATI WASHTAKIWA NA WASHTAKI HAWAIJUI LUGHA YA UK HAPO NI UBABE WA KUONYESHANA UMBEA WA KUJUA KIMOMBO AU TUMWUNGE MKONO WAZIRI ALIYETUTAHADHARISHA UMUHIMU WA KUTUMIA LUGHA YA TAIFA KATIKA MASUALA YA KITAIFA KWA WANATAIFA WANAOIJUA LUGHA YAO YA KITAIFA.

    KUNA MAANA GANI KWA MAHAKAMA ZILIZO ZA KIZALENDO NA ZAENDESHWA NA WAZALENO WANAOJUA KISWAHILI, NA KISHA WAZALENDO WAENDAO MAHAKAMANI WATAFUTE WAKALIMANI ETI KWA VILE MAHAKAMA TUTAENDESHA KWA LUGHA ZA KIMOMBO?

    MIMI KWA MAONI YANGU HUO NI UKIRITIMBA USIOKUBALIKA KWA MANUFAA YA WATANZANIA WENGI WANAOJUA NA KUJIVUNIA LUGHA YAO. PILI NI KASUMBUA ILIYOTAWALA KWA WENGI WA WALIO NA NYADHIFA KATIKA KUENDESHA SHUGHULI MUHIMU ZA KIJAMII KWA KUFIKIRIA KIINGEREZA NDO USOMI KUMBE NI LUGHA KAMA ILIVYO KIMATUMI.

    HAO WANAOTETEA KIINGEREZA MAHAKAMA NI WALE WANAOPENDA WAZALENDO WASIELEWE MAMBO YANAVYOPINDISHWA KISHERIA ETI KWA VILE LUGHA WATUMIAYO HAWATAIJU.

    MMATUMBI MWENZANGU ANAYEJUA KIMATUMBI ATUMIE LUGHA YA KIGENI KWA MAMBO YA MSINGI KATIKA MAISHA YA MIE MMATUMBI KISHA NIAJIRI MKALIMANI ANITAFSIRIE NI KITU KISICHOINGIA AKILINI MWANGU.

    BADALA YA KUPIGA HATUA MBELE NDO WENGINE WANAJITAHIDI KUKUVUTA SHATI UBAKI KATIKA MWENYE POLE.

    HIZO NI MOJA YA HUJUMA ZA KUWAHUJUMU WAZALENDO KATIKA MAMBO YAO YA MSINGI WAKIWA KAMA RAIA HURU WENYE HAKI KATIKA NCHI YENYE UTAMADUNI WAO NA LUGHA MOJA INAYOELEWEKA KWA WATANZANIA WOTE.

    Nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo wote, nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni kheri yangu, Tanzania nakupenda kwa kwa moyo wote

    ReplyDelete
  13. Mdau

    Fill me in please..."ki-Nalitolela Nalitolela"....

    ReplyDelete
  14. Ki-Nalitolela Nalitolela, means Ki-mzumbe Mzumbe, au ki vyuo vya kipori pori vilivyo chini ya viwango. Hii ina maanisha vyuo karibia vyote vya Bongo isipokuwa UDSM.

    Kwa hayo machache, natumai I have filled you in.

    ReplyDelete
  15. NDUGU WASOMAJI WA BLOG YA MICHUZI HAPA CHINI NIME "COPY" NA KU"PASTE" HABARI KAMA ILIVYO KUTOKA KWENYE GAZETI LA NIPASHE LA LEO KUHUSU HILO SUALA LA JAJI MKUU.

    SASA MAANA SISI WATANZANIA TUMEKUWA NA TABIA MBAYA SANA YA KUHUKUMU KWA KUSIKILIZA HABARI ZA UPANDE MMOJA

    HAPA NATAKA NYIE WENYEWE WANA BLOG YA MICHUZI NANI MKWELI KUHUSU ALICHOKISEMA JAJI MKUU. JE NI HABARI ILIYOPO KWENYE BLOG YA MICHUZI AU NI HABARI ILIYOPO KWENYE GAZETI LA NIPASHE LA LEO?
    SOMENI HABARI HIYO KAMA ILIVYO KWENYE GAZETI LA NIPASHE LA LEO

    Jaji Mkuu: Mahakama ziko mbioni kutumia Kiswahili
    Na Selina Ilunga
    26th April 2010B-pepeChapaMaoni
    Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani.
    Mahakama inatarajia kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli zake za kila siku ili kurahishisha utendaji wake.

    Hayo yalisemwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani, wakati akizungumza na wanajumuiya ya Chuo kikuu cha Ruaha (RUCo), wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostine (SAUT) cha Mwanza na wale wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa. Hiyo ilikuwa ni baada ya kushuhudia shindano la uendeshaji wa mahakama ya rufaa ya mfano (Moot Court) lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha RUCo.

    Alisema mahakama itaendelea kutumia Kingereza hadi hapo vitabu husika vitakapobadilika baada ya taratibu zote kukamilika

    Jaji Mkuu alitoa mtazamo huo ikiwa ni siku chache baada ya Serikali kutangaza bungeni katika mkutano wa 19 ulioisha hivi karibuni kuwa shughuli zake zote zitaanza kufanyika kwa lugha ya Kiswahili.

    Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, alisema kuwa shughuli hizo ni pamoja na matangazo ya kazi, usaili, barua na nyaraka zote za serikali pamoja na shughuli za mahakama. Pia alisema magazeti ya serikali yanatakiwa pia kuandika Kiswahili fasaha ili kukuza lugha hiyo.

    Jaji Mkuu alisema kuwa angependa siku moja kuona shughuli zote za kimahakama zikiendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, jambo ambalo alisema linawezekana na liko mbioni kufanyika.

    “Ni mara chache sana ninazungumza Kiingereza, hasa nikiwa kwenye shughuli za kitaaluma na zile zinazohusisha taasisi za elimu ya juu kama vyuo vikuu. Ninafanya hivi kutokana na mapenzi yangu kwa lugha ya Kiswahili,” alisema Jaji mkuu Ramadhani.

    Katika shindano hilo, jumla ya vyuo sita vilitarajiwa kushiriki lakini ni vyuo vitatu tu vilivyojitokeza kushiriki. Vyuo ambavyo vilialikwa lakini havikuhudhuria ni Chuo Kikuu kishiriki Zanzibar, Mzumbe na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

    Chuo cha RUCo ambacho ni wenyeji kilishinda kwa kupata alama 62 na kufuatiwa na Tumaini kilichopata alama 52. SAUT kilikuwa cha mwisho.

    Mzungumzaji bora katika mashindano hayo alikuwa Francis Magali kutoka Tumaini.

    Jaji mkuu alisema kushinda ama kushindwa katika shindano hilo si hoja ya msingi sana bali jambo lililo muhimu ni kushiriki katika zoezi zima ambalo linamfanya mwanafunzi kujifunza kwa vitendo masuala ya uendeshaji wa kesi. Hivyo aliwapongeza washiriki wote wa shindano hilo. Hata hivyo, alisikitika kuona hakukuwa na mwanafunzi wa kike kati ya walioshiriki mashindano.

    Kwa upande wake, Mkuu wa kitivo cha Sheria wa RUCo, Dk. Romuald Haule, alisema mwanasheria bora anatakiwa kusoma darasani pamoja na kufanya mazoezi ya vitendo katika mahakama za mfano.

    Alisema kuwa mahakama za mfano ndio njia bora ya kupima uwezo wa mwanafunzi na kuitumia kujifunzia kwa vitendo kile anachojifunza darasani.

    Mahakama za mfano zilianza kutumika mwaka 1997 nchini Uingereza na zimeendelea kutumika duniani kote ili kukuza uelewa wa wanafunzi.


    CHANZO: NIPASHE
    0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni

    ReplyDelete
  16. Anon uliyetujia na hilo limgazeti lako kuhusu hiyo issue ya matumizi ya Kiswahili mahakamani, sijui nikoonee huruma au vipi.

    Kwa kifupi ni kwamba, hiyo pledge kuwa kiswahili kitaanza kutumika mahakamani iko qualified, you know what I mean? Yaani hapo kwa watu wanaojua kuchambua mambo ni sawa sawa na kuambiwa kuwa Kiingereza kitaendelea kutumika, au kitu kama hicho. Hembu jiulize, mpaka hivyo vitabu vyote vinavyotumika mahakamani vimalizike kutafsiriwa ni leo? Hiyo ni lugha ya kukataa kitu kiutu uzima ndugu yangu ukiisoma vizuri. I stand to be corrected maana mi sikuwepo. Au pengine Jaji Mkuu aliongea hivyo kwa sababu pengine baada ya kuwasikiliza hao ma-non-UDSM wakiwasilisha hoja zao kiingereza, aliiwaonea huruma kwa jinsi walivyokuwa wakijiuma uma na kuji-Nalitolela, so akaamua kusema hivyo just in the passing ili wasijisikie vibaya. Anyway, time will tell.

    ReplyDelete
  17. eti except UDSM vingine vyote ki-nalitolela-nalitolela"

    nimecheka saaana,watu humu??

    ReplyDelete
  18. Hivi kweli uwezo utapimwa kwa mtu kasoma wapi? Nadhani kipimo chafaa kuwa "subjective test" majigambo si mazuri kwani yanatoa picha ya upungufu wa busara yako sidhani kama hivyo vyote vya "kin-nalitolela-nalitolela" visingekuwepo our whole system as a national ingestand. Tuna wataalamu bora tena wanaoweza kuongea kiingereza kizuri kutoka huko. Naamini as long as vyote ni vyuo vinayotambulika na mamlaka husika basi hizo kauli zitabaki kuwa za kijinga na kutoka kwa watu wasioelimika, wasiokubali mabadiliko, wasioitakia mema sekta ya elimu na taifa kwa ujumla na watu walio wabinafsi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...