Mh. Fred Mpendanzoe akitangaza kujiengua CCM na kujiunga na CCJ


Watanzania bado wana maswali juu ya Chama Cha Jamii (CCJ) hasa kama kweli hiki chama kimekuja kuziba pengo la uongozi nchini au ni geresha tu kama ya vyama vingine.


Kabla hata ya kwenda kuomba usajili wa muda tetesi zilishasambaa juu ya ujio wa chama hicho na ndani ya wiki chache tu CCJ kimepata kutangazwa sehemu mbalimbali kwa bure kabisa huku kikivuta mioyo ya wananchi wa kawaida kabisa waliochosha na vyama vya kisiasa vilivyopo ambao kwa muda mrefu wamesubiria kuona matamanio ya Baba wa Taifa kuhusu chama mbadala cha upinzani yakitimia.

Tetesi kubwa ni uwepo wa vigogo nyuma ya CCJ na wapo ambao hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe au kufikiri wenyewe kuhusu CCJ hadi waone kwanza nani ameondoka CCM. Kwa wale ambao wanasubiri wasikie “majina makubwa” yakitoka CCM ndio waamini basi kutoka kwa Bw. Fred Mpendazoe hakuwatoshi. Ni wazi vile vile hata likitoka kundi jingine ndani ya CCM bado wapo watu ambao hawataamini na wataendelea kutafutua ufafanuzi kwanini hao siyo “vigogo” au kwanini kuondoka kwao “ni nafuu kwa CCM”.

Vyovyote vile ilivyo, Watanzania wana haki na sababu ya kuipima CCJ kwa katiba yake, malengo yake, mapendekezo yake ya kushughulikia masuala ya taifa na itikadi yake. Itakuwa ni upungufu wa hekima, na uwezo wa kufikiri kama tutajaribu kukipima CCJ kwa kuangalia nani “anatoka CCM”!


Mtu mwenye hekima atachukua muda kusikiliza kile ambacho uongozi wa CCJ, mashabiki wake, Katiba na watunga sera wake wanasema juu yake na siyo kile ambacho waathirika wa uwepo wa CCJ wanasema juu yake.

Hivyo, mahojiano haya ya kwanza na Mhe. Fred Mpendazoe aliyekuwa Mbunge wa CCM wa kuchaguliwa kwa asilimia 81 (kura 64,000) na ambaye ameamua kuondoka CCM “mapema” yatatupa mwanga wa ni watu gani wako nyuma ya CCJ na kama tunaweza kukubali na kukumbatia uwepo wake katika kuendeleza demokrasia nchini na hasa katika kupatia uongozi “bora” ambao taifa limekuwa likiutamani na kuungojea kwa muda mrefu hasa baada ya kukatishwa tamaa na uongozi ulioingia 2005.


Sikiliza na uamue mwenyewe.
Please click the link below to view it.
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2010-04-11T20_50_38-07_00
See you there!
- Mzee
---------------------------------------------
Hii sehemu ya maelezo ya kujinga na CCJ...

nawezekana unasubiri uone vigogo watoke CCM ndio na wewe ufanye uamuzi na inawezekana unasubiri wengine waanze kuleta mabadiliko ili na wewe udandie mbele ya safari; lakini wengine wangependa kuwa sehemu ya mabadiliko wanayoyataka.. hivyo..

Ni namna rahisi yakujiunga na CCJ kwa haraka na kwa wepesi... Kwa kutumia simu yako:

Ingia kwenye "Message"

Andika neno "Sajili" weka nyota (*)
Andika Jina lako kamili kisha weka (*)
Andika Mkoa unaotoka kisha weka (*)
Andika mtaa unaotoka kisha weka (*)

Halafu tuma kwenda namba 15337

Mara moja utapata namba yako ya kadi, na maelekezo jinsi ya kupata kadi yako..

NB: Utakatwa Tsh..500 za ada..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera mkuu wa libeneke kwa kutoa habari za chama tofauti na tulichozoea. Wengine tulianza kupata mashaka globu ni ya vyama vyenye matawi ughaibuni tu.

    ReplyDelete
  2. Mbona tukituma meseji zinafeli? au wameiban?

    ReplyDelete
  3. WATU WANAKWENDA NA WAKATI NA MASLAHI BINAFSI NI JUU TA JAMII . SWALI JE UNAIPIGIA DEBE CHAMA KWA MASLAHI BINAFSI AU YA JAMII?
    NA IKIWA MASLAHI BINAFSI JE SISI VIPI TUNAWEZA KUSHIRIKI?

    ReplyDelete
  4. Kama maendeleo yangekuja kwa katiba, malengo, sera, na viongozi wanasema nini, Watanzania tungekuwa mbali saaaaana!!! Mmekwisha sahau 'maisha bora kwa kila Mtanzania?' au 'Haki sawa kwa wote?' au 'Nguvu ya Umma?' n.k.

    Huyo Mpendazoe alifanya nini akiwa huko CCM? Kama hakufanya chochote, ni kwa nini? Watanzania ni 'misukule' kiasi hichi?

    ReplyDelete
  5. Hatimaye tumepata kuanzisha chama tunachokitaka sisi wenyewe; Hivi vyama vingine vimezidi mno soga zao za kwanini wao wanastahili zaidi. Asante CCJ kuja kwa wakati muafaka.

    Hata hivyo serikali ya CCM isiwape usajili wa kudumu maana itakuwa ni mwiba!!

    ReplyDelete
  6. hawa ni matapeli,maana wakati wanaanza waliwesa hawatakubali fisadi aingie chma chao,watachunguza wote wanaotaka kujiunga na chama hicho,leo eti hata sura hawakuoni,wewe unatuma msg unaingia moja kwa moja,na wasi wasi,i think ni wanatafuta njia ya kula.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...