Ankal pole kwa kazi ngumu ya kutupa habari za kila siku.
Leo naomba uitoe hii kuhusu hospitali ya moja ya Wilaya tajiri sana hapa nchini kwetu. Namaanisha Wilaya ama ukitaka Manispaa ya Kinondoni.
Juzi tarehe 12 Machi, 2010 nilimsikia Mheshimiwa Billy Lukuvi akisema kuna mafanikio baada ya kuhamisha watumishi 57 na kuleta wapya 58. Nachelea kusema nampongeza RC au vinginevyo kwa sababu zifuatazo:
1. Sina uhakika kama uhamisho ni adhabu, zawadi ama ni njia ya kumrekebisha mtumishi.
2. Mheshimiwa hakutwambia hao 57 kawahamishia wapi na kama huko wanahitaji watumishi wabovu.
Mimi nafikiri watumishi wabovu wangefanyiwa yafuatayo:
1. Kupewa upya mafunzo ya kazi na hasa kukumbushwa nafasi zao katika jamii na kuzingatia Huduma kwa Mteja.
2. Kuwakumbusha kuamini kama Florence Nightingale (mwanzilishi wa huduma ya uuguzi) alivyoamini nanukuu 'I believe that God had called me to become a nurse to help those who needed it'
3. Kuwakumbusha kurudia viapo vya kazi zao walivyotoa wakati wanahitimu mafunzo.
4. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, usalama wa Taifa, PCCB zifanye kazi kwa karibu sana na hospitali hii.
5. Kuwe japo na Canteen ambayo watumishi wa hospitali watapata mlo kwa nusu ya bei na nusu ilipwe na Manispaa. Hili linawezekana ukasema kwa mfano wauziwe soda shs. 200/= ; chakula cha 2000/= wanunue kwa 1000/= kama motisha.
Makala haya yataendelea siku nyingine,
Philemon Muganyizi
0713 310 750
0767 310 750

Kaka Muganyizi nashukuru kwa maoni yako. Lakini naomba nikujulishe kuwa siku hizi hakuna kazi amabayo ni wito. Sote tunaganga njaa tu. Manesi kunyanyasa wagonjwa haijaanza leo. Akina mama hutukanwa,hupigwa vibao wakati wa kujifungua na manyanyaso ya kila aina. mheshimiwa Lukuvi hawezo kujua hilo kwa sabb labda mkewe hujifngulia hispitali za nchi zingine.
ReplyDeleteManesi hufanya haya yote kwa kuwa walishajua udhaifu wa viongozi ktk nyanja hii. Leo mheshimiwa anapowahamisha badala ya kuchukua hatua madhubuti inamaanisha anahamisha manyanyaso sehemu hii anapeleka sehemu nyingine.
Hawa jamaa (manesi ) sasa hivi wanajiona wako juu ya sheria. Mie huwachukia sana. Imefika wakati hata nikikutana na nesi, kumuona tu hasira hunijaa hata kama simjui. Hawa ni wa kuhamishia wilaya ya Tarime wakutane na wajita na wakurya ndi saizi yao.
Pole kaka Mug.
kwa hiyo hao waliohamishwa ndio wenye makosa? na kama ni hivyo kumhamisha mtu mwovu bila adhabu ataendelea na uovu wake huko anakoenda. si mwananyamala tu kwenye uovu ni hospitali nyingi tu hasa dsm,tulilaza mgonjwa pale ilala wadi ya watoto, alitakiwa dose drip ya quinine, manesi walisema inabidi itolewe hela kununua dawa na sindano kwani hawana, hela wakapewa, kufika usiku wakasema ile drip karibu inaisha wakadai hela tena kwenda kununua nyingine sijui walinunua wapi usiku huo wa manane hela wakapewa tena, usiku ule walikufa watoto watano, nahisi wazazi hawakuwa na hela za kununua dawa,kuja kuulizia kumbe zile dawa walizopewa kuhudumia watoto zinapelekwa kwenye pharmacy zao hao wafanyakazi. ni mtandao kuanzia walinzi mpaka daktari
ReplyDeleteNashukuru kwa mawazo ya wote hapo juu! Sasa tujiulize swali dogo kama ifuatavyo: KAMA HALI NI HII KWA WEWE, MKE WAKO, MTOTO WAKO, NDUGU YAKO NK, kweli kuna haja ya kwenda kumchagua kiongozi yeyote especially wale wote ambao wamekuwepo na wanaona haya MATATIZO? Hapa si mchezo ni maisha ya mtu ambapo hayawezi kununuliwa hata iweje! Basi mimi ninaona sasa wakati umefika wa KUWAKEMEA HATA HAO VIONGOZI WAKUBWA WANAPOKUJA KWENYE MIKUTANO YAO YA KUOMBA WACHAGULIWE TENA ILI WAENDELEZE HUU UZEMBE. CHA MSINGI NI KUWAZOMEA ILI WAJIONE HAWAFAI. HII NDIYO SILAHA YA MYONGE AMBAYE HANA MAHALI PA KWENDA.
ReplyDeleteAhsanteni sana ndg Muganyizi
Watakufa kifo kibaya sana..
ReplyDeleteKUWASOMEA HAITOSHI. DAWA NI KURA YAKO. VIONGOZI NA VYAMA VYAO WASICHUGULIWE TENA.
ReplyDeleteKAKA MICHUZI POLE SANA,NAAMINI KTK BLOG ZOTE WEWE UPO JUU SANA,KWANI HATA MAONI YETU HAYATOKI HADI UYA PITIE.SI KULAUMU NA HISISI NI WINGI WA KAZI ZAKO,SASA HUYU ULIYE M DELEGATE KUHAKIKI MAONI KACHOKA.MFANO NI MAONI YA HUYO MCHANGIAJI WA KWANZA (ANONYMOUS WA 14 .07:16AM)NI MJINGA KWANI ANAUWELEWA MDOGO SANA JUU YA MAMBO YA KIJAMII.HUWEZI KUCHUKIA MTU USIYE MJUA,ETI KISA YEYE NI MUUGUZI,HUWEZI KUSIFU YALIYO TOKEA TARIME KWA MWENYE AKILI TIMAMU,WAPUNGUFU WA FIKKRA KAMA HAWA HATUFAI NA MAONI YAO NAOMBA YAWE MIONGONI MWA MAONI YANAYO KOSA NAFASI KTK BLOG HII YA JAMII.HIKI NN CHOMBO MUHIMU SANA KINACHO TUSAIDIA KUJUA TAARIFA MUHIMU NA KUCHANGIA MAWAZO YATAKAYO LETA TIJA KTK JAMII.MANESI DUNIANI NI WATU MUHIMU SANA TENA SANA KULIKO ANAVYO FIKIRI HUYU MPUMBAVU,NANI YUPO TAYARI KUZOA MATAPISHI/KINYESI CHA MGONJWA KWA MSHAHARA WA MATUSI DHARAU NA KEJELI MBALI MBALI?KAMA SIO NESI?ACHENI KUDHARAU HAWA WATU,BILA WAO TUSINGEKUWEPO AU LAA MAMA ZETU WANGE KUFA/BAKI NA ULEMAVU BAADA YA KUZALIWA KWETU KWA KUKOSA HUDUMA.
ReplyDeleteANGALIZO:
NESI NI BINADAMU NA NI MTOA HUDUMA SAWA NA MTU MWINGINE YEYOTE KTK JAMII,MAPUNGUFU YAKE NI YA KIBINADAMU SAWA NA MWINGINE.ACHENI USEMI WA ZAMANI SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE WAMEOZA,AKIOZA MMOJA MTOE UMTUPE WALIO BAKI SAFISHA ENDELEA NA BUSINESS
BY Mr.Mhina
zamani kulikuwa habari pale muhimbili mlinzi kwenye gate alimkamata mkewe kabeba(kaiba) dawa wadini, watu walimshangaa na kumcheka, na kuna mkuu wa wilaya aliyechapa waalim viboko kwa uzembe, kama mwajiriwa anachezea maisha ya binadamu na hajali kama huyo binadamu anakufa au hasomi, sioni kwa nini asitokee mtu kujifanya kichaa au kuchekwa kuchapa watu viboko. maana watu na akili zao wameshindwa kudhibiti maonevu
ReplyDelete