KAMPUNI ya Five Brothers Entertainment imezindua rasmi mchakato wa mashindano ya kumsaka Mlimbwende wa Tanga “Miss Tanga 2010”.
Uzinduzi huo uliofanyika juzi katika Hoteli ya Kola Prieto, ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wadau wa urembo, waandaji wa vitongoji, Afisa utamaduni wa jiji la Tanga Mh. Pius Semfuko, Meneja Masoko wa Vodacom mkoa wa Tanga Robert Mwaikombo pamoja na Miss Tanga wa mwaka 2009 Glory Chuwa aneyemaliza muda wake.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment Nassor Makau alisema kuwa mwaka huu wamejipanga vilivyo kumpata mrembo atakayeuwakilisha vyema mkoa huo katika mashindano hayo kitaifa Miss Tanzania.
Alivitangaza rasmi vitongoji vitakavyoshiriki kuendesha mchakato huo kuwa ni pamoja na Miss Usagara, Miss Ngaminani, Miss Central, Miss College, Miss Chumbageni, Miss Pangani na Miss Lushoto.
Nassor alisema kuwa tatu bora ya warembo kutoka kila kitogoji watapata tiketi ya moja kwa moja kushiriki shindano kuu la Miss Tanga 2010 lilipangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni.
Alisema shindano hilo linatazamiwa kuwa na lenye hadhi na limepangwa kufanyika katika hoteli ya kifahari Tanga Beach Resort iliyoko maeneo ya Sahere mjini Tanga.
Nassor alisema kuwa Kauli mbiu ya mshindano hayo kwa mwaka huu ni
TUKIO MARIDHAWA.
ama kweli kiswahili ni kigumu!!!!
ReplyDeleteAlisema shindano hilo linatazamiwa kuwa na lenye hadhi na limepangwa kufanyika katika hoteli ya kifahari Tanga Beach Resort iliyoko maeneo ya Sahere mjini Tanga.