Jamani watumieni na wengine,
kaka angu kaibiwa laptop 2 Mlimani City. Wamevunja kioo kama mnavyoona hapo. nilikua na meeting nae na tulikaa Silver Spoon kwa muda mrefu alipotoka ndo tayari.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. Poleni.

    Hata kwa Obama mambo hayo yapo.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. comment ya kwanza we ndio mwizi mwenyewe nini?manake mtu ametoa ili kututaadhari we unasema hata kwa obama hiyo ipo yahusuuuu?we umeona kwa obama tu????kuwa mstaarabu kidogo.au hujui gharama ya lap top moja?jiangalie weyeee.pole kaka uliyeibiwa.

    ReplyDelete
  3. njaaa ina uma!!

    ReplyDelete
  4. lakini sio kwenye car parking ambayo ina walinzi.acha kupotosha watu.haya michuzi bania na hii.cha mtu mavi........

    ReplyDelete
  5. pole sana ndugu kuibiwa.. Ila naona kama hicho kioo kilikuwa tofauti na hivo vioo vingine, au kilikuwa ni cha temporary?

    ReplyDelete
  6. MOJA YA TIPS ZA KUZUIA WIZI NI PAMOJA NA KUWEKA VITU VYA THAMANI MAHALI PASIPOONEKANA WAKATI UMEACHA GARI..... POLENI

    ReplyDelete
  7. Jamani ni wakati watu wakawa responsible....mimi hata 2000 siachi kwenye gari sembuse laptop 2....i leaved in london na kule ndio balaa, kuvunja vioo na wizi wa car accessories....BE RESPONSIBLE..kama tungekuwa makini tungeacha kununua hizo laptop mitaani

    ReplyDelete
  8. Imemkumba mke wangu Sea Cliff Village na rafiki yangu kwenye ule ukumbi wa kanisa la wagiriki. Inasemekana wezi ni watu ambao wako decent kabisa na sometimes sio raia wa bongo

    ReplyDelete
  9. poleni sana. lakini kumbukeni kutoka na vitu kama simu, laptops na vyote vinavyobebeka vya thamani kwenye gari. Ukiviacha on display, lazima hao watoto wa mbwa wakulize. Vizuri zaidi hakikisha gari in TINTED ya nguvu hasa vioo vya nyuma. Inakuwa ngumu mtu kuchungulia.

    ReplyDelete
  10. huyo kaka yako ni mjinga utaachaje laptop kwenye gari tena gari yenyewe station wagon. Hiyo ni ku attact wezi bora ingekua saloon kwenye boot hapa mtu anakua hawezi kuona. hapo umejitakia mwenyewe kwanini usingeshuka nayo ukaenda huko silverspoon nayo kwani laptop ina uzito gani?.
    Mdau Bongo Forever

    ReplyDelete
  11. Poleni sana.Haya mambo yanaudhi sana sana.Lakini naomba kuuliza,huyu ndugu yako ni mgeni hapa Bongo? Kaacha Laptop 2 ndani ya gari!!!au aliamini huo ulinzi feki wa hapo.Nchi imeoza hii kwa sasa usiache ndani ya gari hata mfuko wa sokoni wenye nyanya tu (attractions).

    ReplyDelete
  12. Unajua saa nyingine wabongo tubadilike maana comments zote zinamshushua jamaa kwa kuacha vitu vyake ndani ya gari badala ya ku address hii issue zisiendelee kutokea ni kama vile mnawaambia hawa vibaka tumewashindwa....cha msingi ni kuwapigia kelele polisi kwani sehemu za kuuzia hizo bidhaa zinajulikana kama vile za accessories za magari na kuna wakati mtu mmoja alishatoa lisy ya watu na location wanazouzia...kwani polisi walifuatilia na kuweka mitego ya kuwakamat...no

    Hawa wezi wanatumia magari na wanakuwa wengi wengine wanakufuatilia unakoenda na wengine wanabaki kwenye gari lako, ni watanashati na huwezi kuwahisi...bado kuna wanopora wakati unatembea kwa mguu na wao wako kwenye gari wakikwapua begi lako wakati unatemebea ukilingangania utaishia kuburuzwa barabarani...so bado sio solution kushuka na begi lako na kutmbea nalo...ila tukishirikiana tutawaangamiza badala y kuwapa sifa kuwa hatuwawezi....nadhani wengine wenu hamjaibiwa hivyo hujapata ile pinch...USINUNUE MALI ZA WIZI UNAWAPA SIFA HAO VIBAKA NA MTAJI WAO UNAKUA

    ReplyDelete
  13. Pole kaka lakini ungetumia akili maana kila siku wanazungumzia msiache vitu vya dhamani kwenye magari, mnadharau tu sasa matokeo yake ndiyo hayo. Na tunashukuru kwa kutukumbusha. Na hapo Mlimani kuna wezi sana naona hata askari wa hapo wanashirikiana nao kama wanazunguka kwa nini mambo hayo yanaendelea kwa kasi

    ReplyDelete
  14. Hilo ni fundisho maana kila siku mnatangaziwa kuwa msiweke vitu vya dhamani kwenye magari hamsikii.
    Na tunashukuru kutukumbusha. Na huko Mlimani kuna wezi sana naona wanashirikiana na walinzi wa huko kama wanazungukazunguka sasa hivyo vitendo vinafanyika namna gani?

    ReplyDelete
  15. Mdau weka tinted huwa inasaidia sana kuzuia vibaka wasione kuna nini ndani.

    ReplyDelete
  16. wezi wa pale ni walinzi ndio ajira yao ni vema tule sahani moja na uongozi wa mlimani ndio wanafuga tatizo

    ReplyDelete
  17. Pole sana acha uzembe wa kuweka vitu vya thamani ndani ya gari.

    ReplyDelete
  18. Pole sana kaka acha uzembe, mnaambiwa hacheni kuweka vitu vya thamani ndani ya magari.

    ReplyDelete
  19. Anonymous ulieuliza kwamba hicho kioo kilichovunjwa mbona kikotofauti na wenzake, hicho kiko shattered ndio maana kinaonekana na rangi tofauti. Kuhusu kuibiwa laptop kwenye gari inaonekana ni uzembe ila unajua sio kila mtu anachukulia laptop kama ni kitu cha ku make a statement with kama jamaa zangu wengine utawaona wameshikilia laptop kila sehemu kuonesha na wao sijui wasomi na kadhalika.

    Kwa kweli si wazo la busara kuacha valuables katika gari unattended ila sidhani kama huyu mdau ndio peke yake anaefanya hivyo. Mimi binafsi yangu baadhi ya siku nikirudi nyumbani jioni nimechoka nashuka mwenyewe tu na kusahau kila kitu kwenye gari hadi baadae itakapotokezea nimehitaji kutumia computer ndio hukumbuka ipo garini, na wala gari halali kwenye garage.

    ReplyDelete
  20. pole kaka umekuwa mzembe, siku nyingine usiweke vitu vya thamani kwenye gari

    ReplyDelete
  21. jamani ehh hawa watu kama vile jame bond hawashindwi kitu mimi nillibibiwa seacliff village kama utani nimeotka kwenye gari nikaingia ndani kuchukua mkate kurudi hakuna kitu it was like a 5min job

    ila nimepanga na washkji kuwawekea mtego nikimkamata mmoja hasira zangu zote zitaishia hapo

    ila watu wana njaaaaa sana

    sijui ili kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania imeishia wapi ???? aahhh bongo bana !!!

    villager

    ReplyDelete
  22. Nafikiri kuna mambo mawili ya kuangalia hapa. Kwanza uvunjaji wa hicho kioo kidogo ni kwa ajili ya kuweza kupata access ya kufungua locks za mlango au buti nk. Kwa hiyo hata tusemeje huu ni uvunjaji kama ulivyo mwingine wowote kwa ajili ya kupata unauthorised access. La pili hivi jamani hawa Mlimani City management wameamua kulizibia masikio suala hili. Je na hawa walinzi sasa kazi yao ni nini kugawa hizo parking cards tu? unless they are part of the conspiracy... kwa nini kama wizi unapotokea sehemu nyingine za kazi walinzi wanakuwa taken to task as firast suspects isiwe hapa au sehemu nyingine. Au mpaka email nyingine ya 'manyoya' isambazwe kuboycott the place. Asante

    ReplyDelete
  23. Laptop mbili kwenye gari alikua anaenda nazo wapi? na kwanini asingeshuka nazo
    hivi hapo si ndo waliposema PARK AT YOUR OWN RISK? sasa kelele za nini? tumieni akili nina uhakika hizo laptop alikua kazi display

    ReplyDelete
  24. ALAFU WANA JAMII MNAPINGA SWALA LA MWIZI KUPIGWA MOTO

    KAMA ULIWAHI KUUMIZWA KWA UCHUNGU WA KUIBIWA HUWEZI KUPINGA SWALA LA MWIZI KUPIGWA MOTO

    HAWA WEZI WANATIA UCHUNGU SANA MTU UMETOKA KUPIGIKA KWA KAZI ILI UPATE KITU FULANI ALAFU WAO WANACHUKUA KIULAINI

    ALAFU HAO WALINZI WA NCHI WAPO WAPI???

    POLISI WANAJESHI KULA KULALA WANANCHI WANAKOSA AMANI KWA HAWA WEZI VIBAKA NA MAJAMBAZI

    WATU WOTE MACHO KWENYE UCHAGUZI KUFATILIA ULAJI LAKINI SIO KUJENGA NCHI

    BULSHIT SIRUDI HUKO HATA ANKAL AWE RAIS.

    ReplyDelete
  25. Uizi wa namna hiyo hata ulaya upo.cha msingi ni kutoacha simu au laptop au bastola kwenye gari.Nina research kama hizi ambazo zipo uholanzi.electronics equipment sio za kuacha kwenye gari.

    ReplyDelete
  26. wezi hawa hupaka kemikali fulani kwenye kioo halafu kioo kinajikunja na kusinyaa halafu puuuh! wanapiga nakamkono tu! kioo chini.

    Ficha mali yako kwa gari, usii[e misi itoke mate iibe!

    ReplyDelete
  27. Inasikitisha jinsi watu mnavyokumbaita upumbavu. Wizi ni wizi tu. Hakuna cha uzembe, tabia ya wizi ni mbaya. Watanzania sasa mnakuwa na vichwa vya punguani sana. Kuna ubaya gani kucha laptop kwenye gari. Mimi niliibiwa laptop mbili ndani ya nyumba. Nyinyi washenzi acheni kutoa comments zinazoudhi kama akili zenu haziwatoshi. Pumbafu zenu!!!! I wish ningepewa Nafasi ya pinda siku moja tu niwaonyeshe nini maana ya ustaarabu. Na natamani rais afuataye awe dictator mpenda maendelea awakate vichwa watu wote wenye tabia za kimbwa kuiba na kutetea ujinga!!!

    ReplyDelete
  28. We anno. lazima uwe ni limbukeni sana wewe......kwa obama ili nini ?
    Yaaani unaona kikishakuwepo kwa obama ni lulu, hakina tatizo kwanza rudi bongo utakuwa utia aibu tu huko.....stupid !!!

    ReplyDelete
  29. We ahmed....si unajidaidi unakuwa umechoka so unaacha laptop kwenye gari c o ? subiri zamu yako.....utafurahi.

    ReplyDelete
  30. POLE SANA LAKINI NEXT TIME MALI YENYE THAMANI KUBWA KAMA HIYO FUNGIA KWENYE BUTI HUKO NDIO SALAMA OK,NIPO USA

    ReplyDelete
  31. Guyz msimlaumu jamaa kwa kuibiwa kizembe cha msingi ni kuwa makini thats it thn Mlimani city ni jina na majengo tuu wizi upo kwani watu wanaibiwa Magari kila kukicha noma sana pande hizo.

    ReplyDelete
  32. mwambie kaka yako aache ushamba, kwa nini anatembea na laptop mbili?

    ReplyDelete
  33. Bwana Ahmed ee, samahani, hiyo Laptop unayoizungumzia hapo ni laptop kweli au umeamua kutumia kasfida kuweka mambo hadharani?

    ReplyDelete
  34. MTOA MAONI APRIL 15 2:00PM ACHA JAZIBA NA JARIBU KUWA MSTAARABU HII NI BLOG YA JAMII NA INASOMWA DUNIA NZIMA NAKUSHAURI KAMA UNA JAZIBA TAKE A BREAK KIDOGO KABLA YA KUTOA MAONI YAKO KWANI HAKUNA MTANZANIA ANYETETEA MWIZI ILA NCHI YETU INAFUATA UTAWALA WA KISHERIA NDIO MAANA TUNA POLICE,MAHAKAMA NA JELA HATURUHUSIWI KUUA MTU ETI KISA AMEIBA LAP TOP HATA KAMA INA THAMANI YA MAMILIONI,MAANA THAMANI YA BINADAMU NI KUBWA KULIKO HATA HAYO MAMILIONI YOTE YA USA,CHINA NA JAPAN NDIO MAANA KATIKA AMRI 10 ZA MUNGU IMEANDIKWA USIUE(YOU SHALL NOT MURDER)HAYO NI MAFUNDISHO YA MWENYEZI MUNGU KWA MUSA KATIKA AGANO LA KALE NA WALA SIYO MAFUNDISHO YA MTUME PAULO

    ReplyDelete
  35. Pole sana ndugu yangu uliyeibiwa ingawa una uzembe ndani yake lakini kuua au kukata mikono wezi siyo tiba ya kuzuia uharifu kama huo mbona waarabu wanatumia adhabu kali kabisa kama hizo lakini bado kuna vibaka huko kwao

    ReplyDelete
  36. Pole sana, hata mie nishachapwa kwenye gari tena maeneo ya mikocheni B, nimepaki gatini kwa mtu na gari kioo tinted..kinchouma sana wanakutia hasara hadi kwa gari,
    kwa kupenda cheap things ndiyo inatucost sasa,mtu ukiletewa laptop mkononi kwa bei poa unajiona mjanja unanunua
    kuna mtu alinunua laptop kumbe iliibiwa mahali mlinzi aliuwawa mwisho wa siku yy kaswekwa ndani.

    TUPIGEN VITA UNUNUZI WA LAPTOP USED ONE

    ReplyDelete
  37. mnaoshabikia kuua wezi wote hamna Mungu kabisa yaani kutoa roho ya mtu kisa kaiba lap top acheni mambo ya kizamani hiyo lap top jamaa si atafanya kazi na kunua nyingine kama hiyo hiyo?

    ReplyDelete
  38. Watu mnaotoa maoni kama vile kilichotokea ni hali ya kawaida mnachekelea uchafu. Kumbukeni vijijini miaka ya nyuma watu walikuwa wanaacha nyumba zao wazi, wakifunga ni kwa ajili ya kuzuia wanyama wasiingie nyumbani. Ughaibuni yapo maeneo mtu unasahau wallet barabarani na unaweza kuikuta kama watu hawajaja kufanya usafi bado. Wakipita wafanya usafi bado watafanya jitihada kukutafuta. Ndivyo mambo yanavyopaswa kuwa. Tubadilike.
    Mlimani City kwa nini msiweke teknolojia ya kamera kwenye parking lot? Walau mtapata sura zao vibaka hao washtakiwe mnusuru roho zao.

    ReplyDelete
  39. sasa nyie mnaosema jamaa mzembe kuacha laptop kwenye gari na wanaoibiwa magari hapo mlimani city ni uzembe wa nani? watu watembee na magari yao kama mnavyosema watu watembee na laptop zao? hebu kuweni ni fikra za maana ebo!

    ReplyDelete
  40. DU HII KALI MANAKE NA MIMI SIKU YA JUMAMOSI NILIENDA MLIMANI CITY NA MY WIFE WANGU KUFANYA SHOPPING NIKAWA NAMWELEZA KUWA HUAGA NAPENDA KWENDA PALE KWA SABABU KUNA SECURITY YA KUTOSHA KULIKO KWENDA MAHALI KAMA K/KOO,KUMBE NA PALE PAMESHAKUA BOMU,NA MARA NYINGI TU NILIKUA NAACHAGA LAPTOP NDANI YA GARI NA INAKUA SALAMA,MDAU THANKS VERY MUCH FOR INFO ITANISAIDIA SANA.NA HAWA WABEBA BOX WANANIBOA SANA NA STATMENTS ZAO ZA KUSEMA KUA HATA HUKO WALIPO KUNA WIZI SASA KAMA HUKO KUNA WIZI NDIO KUHALALISHE WIZI TZ?ACHENI UJINGA.

    ReplyDelete
  41. Pole sana ila next time kuwa makini maana kwa vitu kama hivyo vya thamani popote pale duniani vinavutia wezi.

    ReplyDelete
  42. Mi nafikiri mlimani city waajiri mateja na wale jamaa wengine wa temeke wale,ambako tunaacha magari yetu takribani masaa manne tukuangalia mechi uwanja wa Taifa na tukitoka tunayakuta salama salimini, sio hawa walinzi takataka kabisa wa hapo Mlimani City. Vinginevyo tutaendelea kulalamika hadi siku akiibiwa Mh. Rais pale nadhani tutasikilizwa. Nashauri wizara husika au halmashauri iubane uongozi wa Mlimani city kwani kwa uelewa wangu mdogo nadhani gari ikishaingia ndani ya eneo rasmi la mipaka ya Mlimani city basi wao wanajukumu la kumhakikishia usalama mteja wao. Pale Blue Pearl hotel ubungo plaza wameweka tangazo parking at owners risk sababu ile parking ipo kwenye hifadhi ya barabara na si eneo la Hotel. Ila ukiweka nyuma ya Ubungo plaza kwenye parking basi suala la ulinzi ni jukumu la utawala na sijasikia wizi ukilipotiwa kule.

    ReplyDelete
  43. wezi wapo ulimwenguni kote kuna habari hata peponi kuna wezi motoni tu ndio hawapo kwa kuwa SIR GOD, yuko bize kuwakaanga.
    sasa hizi kashfa za hapa na pale kuhusu wapi kuna wezi na zikome,pia kama kuna uzembe kwa upande wa muhusika ni kawaida kuelezwa ukweli badala ya bubembelezwa kitoto ili aweze kuwa makini next time.
    haya ni mapambano mikakati ni lazima tupeane kwani hawa wezi pia wana vikao vyao kujadili mafanikio,mbinu,hasara,new targets,kuwaombea wenzao walio kufa kazini,majeruhi etc
    mimi msimamo wangu ikibidi tukaripiane humu na iwe hivyo kwanihumu ukumbini hamna mwizi kama yumo muwakilishi wao then tumekwisha.
    salaam
    maalim kibaka mgeni.
    tandale gengeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...