Abdulkarim Haji Londa
Habari za leo,
Kaka issa nashukuru sana kwa msaada wako pia naomba uwaambie wanajamii nashukuru sana kwa faraja na upendo walionyesha kipindi chote nikiwa na tatizo la kupotelewa na mtoto.

Namshukuru mungu kwa wema wake. Jana nimefanikiwa kumpata mtoto wangu Abdulkarim Haji Londa. Alienda yeye mwenyewe kwa dada yangu na ktk kumuhoji akasema alikua anaishi mtaani Kariakoo! inauma sana ila ni mitihani ya Mungu tunapitia! Nakushukuru tena na tena na

Mungu akubariki sana mpendwa.
Kazi njema
Regards
Mdau Zawadi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Pole sana dada Zawadi, kweli kweli tunapita mitihani ya Mungu. Mungu Mwenyezi azidi mfunika na kuwafunika nyie familia yake kwa damu ya Yesu Kristu.

    ReplyDelete
  2. hongera kwa kumpata mwanao hivi kweli inakuaje umfanyie mwana wa mwenzio unyama kiasi hicho ? ulaaniwe ewe mtu uliyetaabisha roho ya mama wa watu punguzeni ushirikina

    ReplyDelete
  3. bi zawadi, pole sana na mshukuru mola kwa kuweza kukurudishia mwanao.

    Ingawa inauma lakini ni vyema sana ukamuweka kitako na taratibu sana tena sana ukajaribu kupata sababu hasa za kumfanya aondoke nyumbani na kuishi mitaani.

    Kadhalika pia kuna haja ya kujua ni kipi kilichomfanya arudi nyumbani.

    Si rahisi haya ninayokushauri na ni vyema kama utamtumia mtu wa tatu (third party) kuzungumza nae kwa kina, lakini kupata sababu zote zitasaidia sana kuepuka kutokea hayo tena kwake, na pia kutasaidia wazazi wengine kuweza kuepuka watoto wao kutoroka nyumbani.

    Zaidi ya hayo zidi kumshukuru mola kuwa mwanao yuhai na ni mzima alhamdulilah.

    Taymour

    ReplyDelete
  4. bi zawadi, pole sana na mshukuru mola kwa kuweza kukurudishia mwanao.

    Ingawa inauma lakini ni vyema sana ukamuweka kitako na taratibu sana tena sana ukajaribu kupata sababu hasa za kumfanya aondoke nyumbani na kuishi mitaani.

    Kadhalika pia kuna haja ya kujua ni kipi kilichomfanya arudi nyumbani.

    Si rahisi haya ninayokushauri na ni vyema kama utamtumia mtu wa tatu (third party) kuzungumza nae kwa kina, lakini kupata sababu zote zitasaidia sana kuepuka kutokea hayo tena kwake, na pia kutasaidia wazazi wengine kuweza kuepuka watoto wao kutoroka nyumbani.

    Zaidi ya hayo zidi kumshukuru mola kuwa mwanao yuhai na ni mzima alhamdulilah.

    Taymour

    ReplyDelete
  5. WAZAZI KAENI NA WATOTO MJUE NN ASWA KINA CHO WAKWAZA AMU WANAO KUA NA KTK MAISHA YAO YAKILA SIKU.KUWAPIGA WATOTO NI MOJA WAPO MTOTO KUTOROKA NYUMBANI MATUSI;KUTOKUA NA MDA WAKUCHEZA NA MMTOTO NA KUTO WAPA MOYO KWANI NIBINA DAMU WANAOKUA NA MAWAZO UBADILIKA!!!

    ReplyDelete
  6. Pole sana dada Zawadi na hongera kwa kushinda kwa mara nyingine tena mtihani huo. Mwenyezi Mungu akupe nguvu,ujasiri,afya njema na akulinde pamoja na familia yako.

    ReplyDelete
  7. Hongera Zawadi kwa kumpata mwanao.
    Ni raha iliyoje kumpata mwanao baada ya kumtafuta kwa muda.
    Hili pia ni funzo kwa wakaka na wadada waliotelekeza watoto wao.

    ReplyDelete
  8. mtumzimadawaApril 26, 2010

    Maelezo yako hayajitoshelezi, kwanini arudi kwa dada yako na si kwako? Na kwanini akimbie akaishi mtaani kariakoo? Hapa kuna tatizo!
    1. Huende humpi malezi mazuri mtoto wako.

    2. Unamnyanyasa

    3. Huna muda wakumuangalia

    Sasa ulipoona ameshakimbia nyumbani ndo ukaja ukaona umuhimu au ukaona aibu!

    ReplyDelete
  9. Alhamdulillah, roho iliniuma sana nilipoona kule kwa Jide kuwa bado alikuwa hajapatikana mtoto huyu. Jamani jaribuni kuwa nae karibu mjue nini kinamtatiza mpaka akatoroka wakati mwengine wazazi tunajisahau na kuwa mbali na watoto madam tunaona kala kashiba kalala kaamka basi ndo imetoka hiyo tuweni karibu na kuwaonyesha upendo watoto na kujua nini wanawaza nini kinawasumbua na kujaribu kuwatatulia matatizo yao.
    Poleni sana kwa usumbufu mliopata nakutakieni maisha mema, afya, maelewano na mapenzi.

    ReplyDelete
  10. Mwenyezi Mungu na awarudishe wote waliotoweshwa kimazingara ya aina hii. Watoto kwa watu wazima. Imetosha sasa. Amen.

    Tuachane na ushirikina jama. Tuambatane na mambo ya maana. Kwani mtu unaona raha gani kutesa viumbe vya watu? Au kuvifisha kabisa kimazingara? Tuelekeze nguvu kwenye mambo ya kimaendeleo.

    ReplyDelete
  11. NA WEE 26,05,3400pm IVI UNA AKILI WEWE?UNAELEKEA MSHIRIKINA SN WEWE! MTOTO UYO ANAONYESHA KABISA WAZAZI WAKE AWAMJALI NDIO NANAKE KAKIMBIA NYUMBANI,AYA?YAUSHIRIKINA NDIO UNAYALETA WEWE UMU NDANI KAMA UNA LAKU CHANGIA SIUNYAMAZE,

    ReplyDelete
  12. JAMANI NAPENDA KUWAREKEBISHA, MUNGU WETU SI MUNGU WA MITIHANI. NI MKAMILIFU YEYE, SI WA KUGEUKAGEUKA. HAENDI KINYUME NA AHADI YAKE. ALITUUMBA NA ANAPENDA TUISHI VEMA, RAHA MUSTAREHE, TENA BILA KUTANGATANGA.
    MHARIBIFU WETU NI IBILISI SHETANI, HUYO NDIYE MWENYE MITIHANI. KWA TAARIFA YENU NI KWAMBA HAPO MLIPOMKOSEA MUNGU KWA KUSEMA KUWA ANAWALETEA MITIHANI, YEYE ANAFURAHI MAANA AMESHAPATA KITU CHA KUTUSHITAKI KWA BWANA KUWA ONA WATU WAKO WANAKUAMBIA UNAWAPA MITIHANI.
    MUNGU NI MWEMA NA MWAMINFU SANA NA ANATUPENDA. KAMA DADA ZAWADI ANAVYOMPENDA MWANAYE, BASI MUNGU NI ZAIDI SANA MAANA YEYE NI UPENDO.

    TUMSHUKURU SANA MUNGU MAANA AMEWEZESHA MTOTO KUPATIKANA.

    ReplyDelete
  13. annon wa Mon Apr 26, 12:15:00 PM ni wapi ulipopata habari yakuwa kuna mtu aliemfanyia huo unaouita unyama? na ni unyama gani?

    inaonyesha kama unajua zaidi habari hii, na kama ni kweli basi inafaa uripoti kwenye vyombo vya sheria.

    kinachonishangaza mimi ni kuwa taarifa zote za huko nyuma ni kuwa alipotea, na taarifa ya mzazi wake baada ya kupatikana amesema kuwa amewaambia kuwa alikuwa anaishi mitaani, hakusema kama alikamatwa au kulazimishwa na mtu. sasa wewe hiyo idea yako umeipata wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...