Mzee Yusuph na kundi lake la Jahazi Modern Taarab walipokuwa ziarani London
Gari iliyomchukua Mzee Yusuph kabla ya kumwahisha hospitali
Na Dina Marios
Leo mchana msanii maarufu wa muziki wa taarabu hapa nchini Mzee Yusuph alikuja hapa ofisini kwetu Clouds FM kwa ajili ya kulipia matangazo.Sasa bahati mbaya akiwa kwenye parking humu ndani ghafla akawa analalamika hawezi kutembea aletewe kiti akae. Baada ya kuletewa kiti akakaa lakini tena baadae akawa analalamika hawezi kukaa miguu inauma na kiuno kinauma ikabidi atandikiwe chini alale.Kadri muda ulivyokuwa ukienda akawa anazidi kulalamika maumivu mwili mzima. Basi ikabidi abebwe na kuingizwa kwenye gari na kukimbizwa hospitali.
Habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Pole mzee Yusuf kwa maradhi ya ghafla. Ukitaka kula walishwaaaaaaaa! ukitaka kubebwa wabebwaaaaaaaaaa! na hapo mjengoni umebebwaaaaaaaaaa! kuingizwa garini. pole kaka mwenyezi mungu atakuafu.

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu amnusuru. Hila zote dhidi yake, zishindwe na zilegee. Amina itikia.

    ReplyDelete
  3. Mla kwa NakshiApril 22, 2010

    Ashindwe Alegee Mrogaji Mja Walaana Amina Itikiaa. Kwa dua hii Inshaallah utapona Mzee...shaka ondoa.

    ReplyDelete
  4. Inaelekea ana matatizo ya mshipa wa fahamu. MpelekeniIndia kafanyiwe matibabu atapona Inshalah. Kupitia blog ninaelekeza dua zangu kwa Mungu Mwenyezi katika jinala Yesu Kristo ampe ponya ndugu yetu Mzee. Ninaomba na kuamini ameishapona Amen. Hii ni siri kubwa katika ulimwengu wa Roho. Wewe unayesoma hapa naomba elekeza mikono yako kwa Mzee ili apokee uponyanji katika jina la Yesu Amen.

    ReplyDelete
  5. Hivi mbona tunahukumu kuwa karogwa ilihali taarifa ya hivyo haijathibitika????

    Tuachane na hivi imani za kishirikina, Mzee Yusuph amefanyia service mwili wake siku za karibuni? Maana hizo ni dalili za magonjwa yanayohusiana na moyo, kwa upeo wangu mdogo.. Madaktari watazungumza zaidi kwenye hili...

    Lets be scientific tuachane na ushirikina....

    ReplyDelete
  6. Ashindwe Alegee Mrogaji Mja Walaana Amina Itikiaaaaaaaaaa!!!!!
    aramba, aramba, aramba, aaahhh..
    aramba tena, aaaaahhhhhh
    mzee yusufu aramba tenaa aaaaaaahhh

    ReplyDelete
  7. Duuh!!! Prado ambulance. That is malaria signs.

    ReplyDelete
  8. Mungu inshallah atampa afueni,
    inawezekana matatizo ya moyo,ninavyomuona kuwa anamwili mkubwa,inawezekana ikawa moyo.
    mwenyezi Mungu akimpa nafuu,lazima ajitaihidi sana sana kufanya japo Jogging.pia ambunguze kula vitu vya mafuta kama vile vyama.apendelee sana mboga mboga na matunda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...