Toka kushoto ni Shaban Nhende, Mwambata Fedha, Saidi Mussa, Minister Counsellor, Abdallah Kilima, Mkuu wa Utawala, Balozi Hussein Khatib, Mke wa Balozi Mama Zawadi Khatib, Agricolla Assenga, Mwambata Utawala na Ismail Majimoto
Ubalozi wa Tanzania mjini Muscat, Oman chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Balozi Hussein Said Khatib, jana tarehe 26 Aprili siku ya kilele cha sherehe za muungano, uliandaa sherehe iliyofana sana ya kuadhimisha miaka 46 ya Muungano. Sherehe hii ilifanyika katika ukumbi wa Sindbad kwenye hotel ya kitalii ya Crowne Plaza Muscat.
Mgeni rasmi katika sherehe hii alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Oman anayeshughulikia masuala ya kidiplomasia Mheshimiwa Ahmed bin Yousuf bin Obaid Al Harthy, aliyeongoza ujumbe mzito wa Serikali ya Oman ambao uliojumuisha Mtukufu Sayyed Mohammed bin Salim Al Said , Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje, Oman , Mheshimiwa Salim bin Mohammed Al Riyami, Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje, Oman , Mheshimiwa Mohammed bin Ali Al Khusaiby,, Mkurugenzi Idara ya Marekani Kaskazini , Wizara ya Mambo ya Nje, Oman , Mheshimiwa Dr. Waheed bin Ali Al Kharoosi, , Mkurugenzi Idara ya Afrika , Wizara ya Mambo ya Nje, Oman , na Counsellor Tahira bint Humoud Al Zidjaliya , Naibu Mkurugenzi Idara ya masuala ya Konsula , Wizara ya Mambo ya Nje, Oman.
Sherehe hii pia ilihudhuriwa na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Oman , wananchi wa Oman , wafanyabiashara , watanzania waishio Oman , pamoja na waomani wenye asili ya Tanzania.
Katika hotuba yake Mheshimiwa Balozi Hussein Said Khatib alisifu juhudi za serikali za Tanzania na Oman katika kukuza uhusiano bina ya nchi mbili ambo ni wa kihistoria na unazidi kuimarika kadri siku zinavyoenda.
Mheshimiwa Balozi pia aliishukuru Serikali ya Oman na shirika la ndege la Oman Air kwa uamuzi wa kurudisha safari za moja kwa moja kati ya Dar Es Salaam na Muscat mara nne kwa wiki kuanzia tarehe moja Juni 2010.
Kurudi kwa safari hizi kutakuza biashara, uwekezaji na utalii baina ya Tanzania na Oman. Mheshimiwa Balozi na mgeni Rasmi walikata keki ikiwa ni ishara kuzitakia mema Tanzania na Oman.
Hongereni sana.huko Oman.
ReplyDeletekaka Said na Kilima tunawakumbuka sana.
why is it only men mbele and women follow behind?
ReplyDeletemweee mimi sielewagi wakati mwingine.
Is it women are not smart enough, to be in one of those top position or what.
It’s not right and its okay
mdau
Canada
yani mdau canada wee acha tu...
ReplyDeleteafadhali kuna jina AGRICOLLA ASSENGA
maana nilitaka nipigie red-line
loooh
Hongereni sana Ubalozi wetu huko Oman.
ReplyDeleteLet us be great thinkers, so that we can talk ideas.
Mdau