Taifa Queens na viongozi wa netball Scotland
Timu ya Tanzania ipo Scotland kwa sasa. Matokeao ya michezo ya kirafiki hadi sasa:
1. Tanzania vs Leeds City = TZ 28: Leeds 63
2. Tanzania vs Braford City: = TZ 50: Bradford 36
3. Tanzania vs Scotland = TZ 37: Scotland 43
Hali ya wachezaji:
1. Agness Simkonda: Amepasuka sana sehemu ya chini ya mdomo na kuchukina mkono na vidole baada ya kugongwa vibaya katika mechi ya jana. Hategemia kuendelea kucheza.
2. Lilian Sylidion: Ameumia kifundo cha mguu na mguu umevimba sana toka mechi na Leeds: Anajitahidi kucheza kwa vipindi vifupi kama dk 20 tu za mchezo.
3. Semeni Mathew: Ameumia sehemu ya unyayo wa mguu toka mechi na Leeds. Anaendelea kucheza kwa vipindi vifupi.
Kutokana na kuwa na majeruhi watatu timu inakuwa na upungufu mkubwa kwani wachezaji wanatotakiwa kucheza ni saba na timu iliyopo inawachezaji tisa na watatu ni majeruhi hivyo tunapata ugumu sana katika kuziba pengo la wachezaji hao watatu na hivyo kulazimika kuwachezesha huku wakiwa wagonjwa ili kukamilisha idadi ya wachezaji saba ambao ndio wanaotakiwa. Tunawashukuru sana vijana wetu kwa kujitoa kucheza huku wakiwa wagonjwa kwa kutambua uzalendo ni muhimu katika kufanikisha utaifa wetu.
Hili litakuwa fundisho kwetu. Serikali ya Tanzania na Watanzania wapenda michezo kujitoa kikamilifu katika masuala ya kitaifa kwani kazi inayofanywa na timu hii ni kwa faida ya Tanzania.

Tunawashukuru baadhi ya watanzania wanaoishi Scotland, Bradford na London na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza waliosikia kuwa Timu ya Tanzania ipo Uingereza wakaamua kututafuta na kuja kutuona na kutupa moyo katika mazoezi na michezo yetu. Huo ndio uzalendo, tupo pamoja tunawawakilisha.
Mechi zilizobaki:
Tumebakiza mechi moja na British Universities utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 16/04/10 katika Chuo Kikuu cha Edinbugh katika ukumbi wa Pleasance kuanzia saa nane mchana.
Aksanteni
Joel Mwakitalu
Kiongozi wa Msafara
On Behalf of:
Tanzania Netball Association - CHANETA
P.O. BOX 60240, Dar es Salaam
Tel: +255 732 994587/654 209954 - Office
Tel: +255 754 613651 - Chairman
Tel: +255 754 297830 - Secretary General
Fax +255 22 2420178/22 2850972

Poleni kwa safari ndefu ya mafunzo na pia pole kwa wachezaji walioumia. lakini ni fundisho kwetu kuwa wakati mwingine tunapokuwa nan safari nje ya nchi au hata mkoa, tuwe na wachezaji wa kutosha.tufanye kama timu ya mpira wa miguu ambapo pamoja na kuwa timu ni watu 11 lakin msafara unakuwa na wachezaji wasiopungua 18 mpaka 20. hivyo hata ninyi wa netiboli itapendeza katika ziara zenu kuwa na wachezaji wasiopungua 14.
ReplyDeleteHapo mnaweza kukabili ajali na majeruhi yatakayo jitokeza katika michezo yenu.
Hii timu ilipokuwa inakwenda huko haikujuwa itacheza mechi ngapi? nashangazwa na idadi ndogo ya wachezaji waliokwenda na idadi ya mechi wanazotegemewa kucheza. hivyo uongozi haukufikiria muwa kuna kuumia na kuchoka pia? na mbona naona idadi kubwa sana ya uongozi wa msafara? kulikuwa na haja ya hao wote kusafiri na timu ndogo namna hiyo?
ReplyDeleteinaonyesha kama kwamba idadu ya wachezaji ilikatwa ili maofisa wengi waweze kusafiri.
Mmmnh... hayo maumivu / majeraha waliyoyapata mbona kama ya kutunga-tunga vile?
ReplyDeleteIla kama ni kweli, poleni.
Huyo Joel Mwakitalu kaenda fanya nini, huo ndio ............. sometime, viongozi wangapi wanatakiwa kwenda na timu? coach, doctor, na moderator kama number ya wachezaji ni ndogo lakini sisi pasu kwa pasu, wachezaji 9 na viongozi nao 9 yaani kila mchazaji na kiongozi wake. Inaudhi
ReplyDeleteAhaaaaa...!!!! Kumbe ndivyo mnavyo vaa mkiwa ulaya!!???
ReplyDeletewachezaji ni tisa, viongozi waliokwenda na timu ni wangapi? kwa nini wakaenda na timu ndogo ilhali wakijuwa wanakabiliwa na mechi nyingi? jee hawakufikiria kuumia kwa wachezaji au kuwa na machofu?
ReplyDeleteTafuteni timu msirudi,ingieni mitini,kama kuna timu zinaonyesha zinataka kuwasajilini fanyeni hivyi Tanzania imeshauzwa.
ReplyDeletebulshit just kusafiri tu hamna lingine limewafanya watengeneze hizo safari za kipuuzi wachezaji 9 viongozi 9 kweli bongo ujanja kuwahi
ReplyDeletekwanza poleni sana wachezaji mloumia na pili hongereni nyooote mlocheza kwani mmeonyesha jitihada kubwa sana, kuweza kucheza na timu kubwa mbalimbali za UK. Halafu wabongo acheni kupondea mambo msoyajua sio mtu akiandika tu jambo we unadakia bila kujua. Nashukuru Mungu nimewaona kwa macho timu hiyo na viongozi watatu tu walokuwa muhimu. Cha muhimu Taifa letu lilipe swala la michezo kipaumbele na wananchi tu wa support wawakilishi wetu hawa kokote waendako kwa hali na mali. Mama HJ Glasgow- Scotland
ReplyDeleteje michuzi unahabari Taifa Queens bado wako Glasgow wamekwama safari, baada ya ndege zote kuzuiwa ndani au nje ya UK. Basi bado tuko nao na tungeomba wabongo wa Glasgow wajitokeze kuwaunga mkono michizi wape taarifa wadau wenzako. Ahsante Bro!
ReplyDeleteMama HJ --Glasgow , Scotland