Mhe. Dkt. Batilda S. Burian (MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) akichangia mada katika Mkutano wa Pili wa Mawaziri kuhusu Udhibiti wa Maafa katika Bara la Afrika, uliofanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 14-16 Aprili 2010. Katika mada yake, alibaini ambavyo mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika kuleta majanga ikiwemo mafuriko, kuenea kwa hali ya jangwa na magonjwa. Hivyo, alisisitiza umuhimu wa kujumuisha masuala ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na udhibiti wa maafa kwa mtazamo mpana zaidi na kwa kuzingatia masuala mtambuka yakiwemo ya jinsia, umaskini, hifadhi ya mazingira na utamaduni na mila. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti kwa kuwa vizazi vijavyo havitatuhukumu kwa yale tuliyofanikiwa bali kwa yale tuliyoshindwa kutekeleza. Mhe. Dkt. Batilda na ujumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano ya mkutano.
Mhe. Dkt. Batilda (mstari wa mbele, mwenye mtandio wa njano) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano huo uliohudhuriwa na nchi zipatazo 40 kutoka barani Afrika.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Good to see waziri mchapa kazi.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. Wacha kujikombakomba wewe Yuesibulogaa! utabeba kiboksi maisha yako yote, kudaaadeeek!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...