Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kanali John Antonyo Mzurikwao akiwasha taa katika Chumba cha Kujifungulia kina mama, katika Kituo cha Afya cha Mpui, Sumbawanga mkoani Rukwa, kuzindua rasmi Mradi wa Umeme wa Jua, hivi karibuni.
Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Hosea Mbise, akiangalia taa (haionekani pichani) inayotumia umeme wa jua, katika moja ya vyumba vya Kituo cha Afya cha Mpui, Sumbawanga mkoani Rukwa, muda mfupi baada ya uzinduzi wa mradi wa umeme wa jua wilayani humo uliofanyika hivi karibuni. Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Mbise, Mradi huo mkubwa wa aina yake ni wa kwanza kuzinduliwa barani Afrika, na Sumbawanga imebahatika kuwa ya kwanza kupata huduma hiyo. Kuzinduliwa kwa mradi huo kutasaidia kuchochea shughuli za maendeleo kwa wananchi wa Sumbawanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ni hatua nzuri na ninawapongeza sana kuipa Sumbawanga kipaumbele, maana ni miongoni mwa maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo. Sasa muangalie na sehemu nyingine kama hizo zenye uhitaji, siyo kuishia hapo tu.

    ReplyDelete
  2. hongera sana mzee Hosea Mbise.

    ReplyDelete
  3. Je mradi huo utaishia Sumbawanga tu au mna mpango wa kuufikisha sehemu nyingine pia? Kama mtafika sehemu nyingine pia tukumbukeni nasi huku Kigoma vijijini.

    ReplyDelete
  4. Safi sana. Now let see if we can do the same thing for the rest of TZ.

    ReplyDelete
  5. say no to tanesco!April 21, 2010

    now lets see all households use this and we will see how long before Tanesco is History!

    ReplyDelete
  6. nilitarajia picha zingetuonyesha huo umeme unavyofanya kazi, siyo watu wenye suti wakishangaa kitu tusichokiona.

    promote the product, or in this case the initiative; badala ya personalities.

    lack of journalistic view kwa aliyepiga picha

    ReplyDelete
  7. Mh! Nimecheka kweli, yaani watu wengine wameumbwa kuponda tu kila kitu. Sio siri anony unayelalamikia picha inaonyesha huwapendi hao waheshimiwa kwenye picha, una bifu nao nini? Mdau uliyetuletea habari na picha usikate tamaa, hao ndo waosha vinywa bwana. Ila nami niulize kitu kwa wahusika, sote tunafahamu umeme wa solar ulivyo gharama kuweka, sasa huo mradi unawasaidia vipi wananchi hawa maskini kuhakikisha wana-afford gharama zake?

    ReplyDelete
  8. Mdau uliye concerned na picha, nashukuru kwa changamoto. Picha zaidi zitatumwa.

    ReplyDelete
  9. Hongera sana Meshimiwa HOSEA MBISE,haya ndo majukumu ya kiongozi hodari na shupavu TANZANIA.Mungu akubariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...