Michael Richard Wambura

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa muda wa Klabu ya Simba, Michael Richald Wambura leo ametangaza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe hapa nchini yenye maskani katika mtaa aa Msimbazi jijini Dar.

Wambura aliitisha mkutano wa wanahabari leo mchana na kutangaza nia yake ya kuwania kiti hicho ambacho kwa sasa kinashikiriwa na 'Field Marshal' Hassani Dalali.

Wambura alibainisha hayo katika klabu maarufu ya Break Point iliyopo katika viunga vya Posta mpya jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Simba ilitangaza kutoa fomu kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti na Makamu wake na tayari fomu hizo zimeanza kutolewa katika makao makuu ya klabu hiyo. Mwisho wa kutoa fomu na kurejesha itakuwa tarehe 10 mwezi aprili wakati uchaguzi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Mei 9.

Mpaka sasa wanasimba waliochukua fomu ni Mwina Kaduguda, Geofrey Nyange Kaburu, Ismail Aden Rage na Wambura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Huyu jamaa ninachompendea mimi ni kitu kimoja he's a FIGHTER. Never give up easily

    Nakutakia kila kheri bro.

    ReplyDelete
  2. Mkata IssueApril 05, 2010

    Kuna tofauti kubwa kati ya Mpiganaji na Kingáng'anizi.

    Ni ajabu kuona watu wale wale walioiangusha 'FAT' wanang'ang'ana na vilabu na Shirikisho wakati hawana matunda yeyote ya kuonesha!

    Hivi katika nchi yenye watu wazima wenye uwezo wa kuongoza vilabu vya michezo (tuseme yapata millioni moja) hakuna watu wengine?

    Kukosa utamaduni wa kujiuzuru, kupisha wengine wajaribu na au kung'atuka kwa hiyari ni zao la ukosefu wa tathmini binafsi ya kweli, uwepo wa ulafi fulani na kiwango cha chini cha wanachama (watu husika) katika kujua haki zao. dy/dx.

    ReplyDelete
  3. Ankal, nakushauri kabla haujarusha habari kwenye blog uwe unaihariri kwanza. Mfano makosa hayaninayoorodhesha ni ya kizembe sana.

    wambura akitosa kugombea uenyekiti Simba SC


    Mpaka sasa wanasimba waliochukua fomu ni Mwina Kaduguda Makamu Geofrey Nyange Kaburu


    Kuna watu makini, wasomi na watafiti wengi tunasoma hii blog ya jamii, nadhani si kila habari unaandika wewe, kama dhana yangu ni ya kweli ninaomba uhariri habari zote kabla ya kuzirusha hewani. Mtu makini hafanyi makosa kama hayo, na habari makini uandikwa na mtu makini.Naamini wewe ankal ni mtu makini na huu ni ushauri tu.Husije kushusha hadhi ya blog ya jamii.

    ReplyDelete
  4. hana lolote ni kutafuta ulaji tuu mlivyoifanya fat kwani hatukumbuki? tafuta dili lingine hili liache kwa sura mpya sio zile zileee hamna jipya labda mbinu mpya za kifisadi

    ReplyDelete
  5. Anon 12:39 kidogo umechemka bwana mdogo.

    Sisi wasomi na watafiti hatuangalia vitu kama comma, full stop au upungufu wa herufi kwenye neno. Tunachoangalia ni maudhui ya habari au ujumbe.

    Kazi ya kuhariri maneno tumekuachieni wewe na wenzako.

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo juu Michuzi ameweka disclaimer pale juu uwe unasoma usimsumbue. Anapost habari kama ulivyompelekea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...