Habari Mkuu wa nanihii,Natumai una afya njema na libeneke linaendelea vizuri. Naomba unitundikie hili suala langu ili nipate kujua uzoefu wa wajumbe wengine kuhusu TCU central admission system.
Najaribu kumsaidia dogo kutuma maombi ya chuo kikuu kupitia TCU Central Admission System kwa wiki sasa bila mafanikio. Tatizo kubwa ni kua nashindwa kufika katika mahali ninapotakiwa kuchagua course/programme na kukamilisha zoezi zima (nilifanikiwa kuregister kwa shida sana). Napenda kuhakikishia kua speed ya internet ninayoitumia ni kubwa sana kiasi naweza kutumia internet calls. Pia nimejaribu kutumia web browser tofauti bila mafanikio (window explorer 8, mozila firefox 3.6 na google chrome).
Nadhani tatizo liko katika system yenyewe. Kuhakikisha hili naomba wajumbe ambao wamefanikiwa kukamilisha zoezi watupe uzoefu wao. Je kuna mtu yeyote aliyewahi kufanikiwa.
Nimejaribu kuwasiliana na TCU kwa njia ya email lakini hadi naandika email hii bado hawajanijibu.

Natanguliza shukrani kwako na wajumbe wote watakaochangia.
Mdau Kapongola, Njombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2010

    .....kweli hapo kuna tatizo sana na kwa upande wangu naona ni kuwa watu wengi wanakuwa wanajaribu kwenda huku hasa muda wa mchana na hivyo kusababisha tatizo hilo kutokea. Nimegundua hilo baada ya kuamua kufanya hiyo muda wa usiku yapata majira ya saa sita usiku na haikuwa na shida sana vile kama ilivyokuwa muda wa mchana. Hivyo nadhani hiyo ni kuzidiwa tu kwa server kutokana na request nyingi zinazotumwa hasa wakati wa mchana...!Jaribu kwa muda wa usiku sana unaweza ukafanikiwa.

    ReplyDelete
  2. Proma, DarMay 26, 2010

    Pole mdau. Hili ni tatizo lililowakumba na linaendelea kuwakabili karibu watu wote wanao-access CAS ya TCU.

    Mi nilijaribu kumsaidia dogolas wangu na kwa bahati nzuri tulifaulu japo ilitusumbua pia.

    Nadhani tatizo, mbali ya internet zetu za magumashi, ni server za TCU ambazo kwa kuwa watu wengi wana-access huduma hii kwa sasa,server zao zinashindwa ku-accomodate watu wengi kwa mara moja.

    Nadhani jaribu nyakati ambazo watumiaji watakuwa wamepungua, hasa nyakati za usiku mnene (sasa hapa kama unatumia internet cafe au public internet itakuwa shida). Nna hakika utafanikiwa.

    Kwa ujumla mimi nimefurahia huduma hii kwani imepunguza ulazima wa applicant kulazimika kusafiri na kuwasilisha maombi yake kwa kila chuo anachodhani yuko eligible, na hivyo kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kununua mafomu na nauli. Pia itaondoa kabisa mambo ya kughushi vyeti kwani taarifa za wanafunzi wote tayari ziko kwenye mtandao. Ukiingiza index number ya mtihani ambayo si yako umekamatwa.

    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2010

    mi nilijaribu kuanzia saa tano usiku ikakubali vizuri. kama alivyosema mdau hapo awali kuna ishu ya speed, watu wanao access hiyo web kwa wakati mmoja ni wengi inabidi ipewe bandwidth kubwa kidogo. mi baada ya kujalibu siku mbili bila mafanikio nilikaamua kuitembelea usiku. kuanzia saa tano unatereza bila wasiwasi.
    asante

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2010

    hata mi ilinisumbua kidogo, ila si lazima kusubiri hadi usiku, jaribu kuchukua soda cocacola ya baridi then mwagia nusu chupa kwenye keyboard yote huku ukiwa umeipindua monitor ya computer yako upside down, wait for about five minutes then restore the monitor in its normal position then endelea na kazi, hapo itakubali haraka bila shida tena speed inaongezeka. ikiendelea kuleta shida basi ile nusu chupa iliyobaki ya cocacola baridi nayo imalizie juu ya keyboard kisha endelea utaona mambo yanakuwa mazuri, mi nilifanya huo utaalamu tena ilikuwa saa nane mchana na sikupata shida kabisa. sema wakati wa kumwagia cocacola kwenye keyboard jitahidi mwenye internet cafe asikuone itakuwa mshikemshike ndege tunduni manake wengi huwa hawapendelei cocacola wanasema zinaleta kutu baadae, wao huwa wanapendekeza mteja atumie spirit zaidi, so ukiona shida kupata cocacola basi nenda kwenye duka la dawa waambie wakupe spirit uende nayo internet cafe, ila kwa spirit inabidi umwagie kichupa kizima kwa mkupuo. nadhani nimekusaidia vya kutosha. pole kwa usumbufu uliokupata.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2010

    Hivi ni kweli huyo mtu wa 2:36 anavyosema u ni hadithi zake. Blog ya michuzi ndio nakua addicted kwa comments kama hizi. Tanzania ni uchumi tu mmbaya kuna macomedian huku kishenzi

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2010

    Huyu jamaa wa 02:36 ni chizi nakuombeni msisikilize huo ushauri wake huyo ni mwehu kabisa. unatoa ushauri kama huo kwa vijana hawa ( Watoto) watafanya hivyo hivyo waziuwe keyboard zao. sio lazima aende cyber cafe.
    Please msichukue huo ushauri 'HATA COMEDIAN SIO USHAURI WA KUTOA KWA WATU WANAOFANYA MAMBO MUHIMU KWA MAISHA YAO'
    Ameni bore sana huyo jamaa.
    Michuzi Zuia ujinga kama huo siku zingine.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2010

    annon may 27,02.36am nimecheka hadi basi wezangu hapa wanafikiri nawehuka lol

    watu mna wazimu humu???

    ila hii system ime=prove failure waziri nafikiri yule amekiri apa juzi kuhusu hii system inavosumbua,hasa ukitegemea majority twatumia public caffe au uibie ofisini napo km ni mfanyakazi,so muda wa usiku ni wale wenye nazo(moderm,blackbery)

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2010

    Huyu jamaa wa 02:36 ni mngese achana naye anarwafi siku mojamoja!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...