Mtoto anayedaiwa kutekwa nyara mjini moshi na kupelekwa nchini uganda akiwa amebebwa juu kwa juu muda mfupi baada ya kuwasili kwenye stendi ya basi ya kampuni ya Mabasi ya Kampala Coach Ijumaa hii.
Basi la Kampuni ya Kampala Couch lilipowasili jana mjini moshi kutokea Uganda ambalo lilikuwa na mtoto anayedaiwa kutekwa nyara watu wasio julikana na kupelekwa nchini Uganda .Hapa ni baadhi ya mamia ya watu waliojitokeza kumpokea mtoto huyo.
Pichani ni mtoto faraji Harun (8)anayedaiwa kutekwa nyara mjini moshi na kuepelekwa nchini uganda akiwa amebebwa juu kwa juu alipowasili Ijumaa
Picha zote na Habari na
Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi

Mamia ya wakazi wa mji wa Moshi jana Ijumaa walikusanyika kumpokea mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Korongoni, mjini Moshi, alitekwa nyara Jumapili ya April 18, mwaka huu, muda wa saa 10 jioni, akiwa nyumbani kwao eneo la Oysterbay Mbuyuni, ambapo imedaiwa alisafirishwa kwa lori hadi nchini Uganda.

Baba wa mtoto huyo Haruni Ayoub (35), ambaye ni mfanyabiashara wa mjini Moshi, alisema kuwa mtoto wake huyo alitekwa nyara na watu hao wakati yeye na mama mzazi wa mtoto huyo Bi Bisina Abedi (32) wakiwa wamekwenda shamba.

Alisema alilazimika kwenda nchini Uganda kumwokoa mtoto wake, ambapo alisema wamefanikiwa kumwokoa baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa na watekaji.

Imedaiwa kwamba watekaji hao, walifanya mawasiliano na wazazi wa mtoto huyo, na kumtaka kutoa fedha kiasi cha dola 1,000, ili waweze kumwachia mtoto huyo, lakini haijafahamika njia wazotumia kupata mawasiliano hayo.

Kwa mujibu wake Haruna walilazimika kutoa taarifa za tukio hilo katika kituo cha polisi mjini Moshi, lakini baadaye walilazimika kuandaa mchakato wa kutafuta fedha hizo, kutokana na vitisho na masharti magumu waliyoendelea kutolewa na watekaji hao, kwamba wameshampata mteja wa kumnunua mtoto huyo na wakichelewa hawataweza kumpata tena.

Kutokana na suala hilo kuelezewa kuwa gumu wazazi hao, kwa ushirikiano na wafanyabiashara wa soko la Mbuyuni, mjini Moshi, walichanga kiasi cha shilingi milioni 1.5, na kulazimika kusafiri hadi nchini Uganda wakifuata maelekezo ya watekaji hao, kwani waliambiwa mteja alishatoa shilingi milioni mbili ili kuweza kumnunua mtoto huyo

“Nilielekezwa kuweka fedha hizo kwenye akaunti katika benki ya Stanbic iliyopo eneo la Busia nchini Uganda kwenye akaunti namba 0140592455501 yenye jina la Salai Kaya na baadae tulisubiri kwa saa tisa, ambapo tulielekezwa kumchukua katika kituo cha mabasi cha Busia”, alisema.

Mtoto huyo, ambaye aliwasili mjini Moshi jana muda wa saa 6: 20 mchana, akiwa kwenye basi la kampuni ya Kampala Coach, lenye namba za usajili KBJ 989E, alimsha hisia za wafanyabiashara na wananchi wengine ambao walilitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kutoa ushirikiano wa kumpata mtoto huyo na kuwakamata watekaji.

Mara baada ya kupokelewa mtoto huyo huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, alizungushwa katika maeneo mbali mbali ya mji wa Moshi, na baadaye kufikishwa nyumbani kwao, kwa ajili ya mapumziko.

Hata hivyo juhudi za askari kanzu waliofika nyumbani hapo kutaka mtoto huyo, kufikishwa katika kituo cha polisi ili kutoa maelezo, zilikutana na upinzani mkubwa wa wananchi, waliokuwa wakihoji kuwa walikuwa wapi hadi mtoto huyo anapatikana.

Akizungumza kwa taabu huku akibubujikwa na machozi ya furaha kwenye mahojiano na waandishi wa habari mtoto Faraji, alisema kuwa alipelekwa katika eneo asilolijua baada ya kuchukuliwa nyumbani kwao kwa ahadi ya kununuliwa mhindi wa kuchoma. Alisema amewaacha wenzake watatu, nchini Uganda , ambapo walikuwa wakiishi pamoja kwa muda wote huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Kilimanjaro Bw. Linus Sinzumwa alithibitisha kupokea taarifa za kutekwa mtoto huyo na kueleza kuwa walikuwa wanaendesha uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na askari wa mtandao wa kimataifa wa Interpol, kuwabaini watekaji hao.

Afande Sinzumwa, aliwaambia waandishi wa habari kuwa baba wa mtoto Haruna Ayoub, alitoa taarifa ya kupotelewa mtoto wake Mei 4, mwaka huu, baada ya kugundua amepotea tangu Aprili 18, mwaka huu.

Alisema jeshi hilo la polisi lilikuwa kwenye harakati za kutaka kuwasiliana na Interpol, ili kufanyia uchunguzi suala hilo , lakini baadaye mtoto huyo amepatikana wakati juhudi hizo zikiendelea, na kwamba bado juhudi zaidi za kuwasiliana na Interpol zinaendelea ili kuweza kubaini namba za simu zilizotumiwa na watekaji hao.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2010

    POLISI KWA VISINGIZIO HAWAJAMBO...ETI NDIYO TULIKUWA TUNATAKA KUWASILIANA NA WENZETU WA INTERPOL ILI TUANZE KUMTAFUTA HUYO MTOTO.JAMANI POLISI WA TANZANIA MBONA WANA MANENO MENGI YASIYO NA MAANA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2010

    Masikini nchi yangu. Poleni wazazi lakini kweli Tanzania saa nyingine inanifanya nilie sana.

    Mtu hakuna msaada kwa police wala nini. Watu wameshapigiwa simu yakutaka hela bado police hawaamini kuwa ni kweli.

    Kila mtu ni kujilinda kivyake vyake tu...I am happy watu waliosimama kidedea na kuwatoa mkuku hao police kanzu wanaokuja baada ya mtoto kupatikana ili iwe nini...Walikua wapi...

    Ila hawa waganda wakianza hivi basi itakua shida sana. Huko kwenye hiyo bank ingetakiwa serikali iwajibike kuwauliza waganda ni nani amechukua hizo hela...

    ReplyDelete
  3. Polisi wa tanzania hawana quick response katika matukio magumu na ya kusikitisha kama haya. Utekaji nyara wa watoto, na ambao ni wa mawasiliano unatoa fursa ya kuwakamata waarifu. Na huu uzembe wa mtu mmmoja au wawili waliokuwa zaamu, unapelekea taifa letu lionekane kushindwa kulinda haki za raia wake. Nashauri hatua kali zichukuliwe dhid ya olisi kituone hapo aliporiport.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2010

    This is so sad, eti walikuwa wanawasilian na Interpol. Ningekuwa na naweza nisingekaa nilipe kodi Tanzania hadi huduma za jamii ziboreshwe. Haya endeleeni kuwasiliana na interpol mmeambiwa kuna wengine wawili wamebaki huko

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2010

    Kweli Bongo usalama wa raia ni sifuri! Hii sio skendo ya mkuu wa polisi kujiuzulu kweli? Facts zote ziko wazi, mpaka account number wamepewa, wanashindwaje kuwatia mbaroni wahusika?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2010

    mimi sijui u-detective lakini ningeanza na mwenye account ambayo hio hela ya kumkomboa mtoto imewekwa,tena wana jina la mwenye account!!its not rocket science

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 15, 2010

    Jamani nchi yetu viongozi wanatia huruma. walipita wapi na lori lao hao watekaji? si walipita boader zote? hakuna kukaguliwa kwenye mipakani? na kama ni hivi ikipitishwa hiyo sheria ya EAC si watoto wetu wataishia wote huko? Viongozi kuweni makini. sasa hivi hata watanzania kupata kazi imekuwa ngumu sababu ya hawa wageni. mnaendelea kuwale sasa wanakuja kuwaibia na watoto wenu. Serikali, Rais wetu uko wapiiiii?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2010

    KUNA WATOTO WENGINE WAMEBAKI. WAZAZI WAO WAKO KATIKA HALI GANI?
    Maigizo first class.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 15, 2010

    Hili swala lote lina utata, kwanza wazazi hawakutoa taarifa ya kupotea mtoto zaidi ya wiki mbili...kwa nini? ukilifuatilia jambo lenyewe kiumakini utaona kuwa halihitaji akili za ziada kugundua kuwa wazazi wamehusika kwa aina moja au ni uzembe...kwa nini nasema hivyo,hao watekaji waliijuaje namba yao ya simu (ni watu wanaofaamiana),kiasi kilichotakiwa ni kidogo ukilinganisha na maisha ya mtoto, mara nyingi watekaji uwateka watoto wa matajiri- kwa nini wao... kwa nini hawataki police kumuhoji mtoto hata kama hawakufanya kazi yao wakati wanajua kuwa mtoto anadai kuwa kuna watoto wengine wawili wamebaki huko? I smell a dead fish on all this songombingo...dont conderm before you know the whole story.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...