ankal akitoa tuzo ya Hall of Fame kwa mkongwe Zahir Ally Zorro huku akishuhudiwa na wanawe Banana (kulia) na Maunda pamoja na mzee mzima Kassim Mapili (shoto)
Baba na mwana na familia wakifurahia tuzo zao ambapo baba kapata ya Hall of Fame na mwana kaibuka mwimbaji bora wa kiume kwa mara ya pili mfululizo

Mwenyekiti wa African Stars entertainment Baraka Msiilwa akiwa ameshikilia tuzo tatu ambazo Twanga Pepeta wamepata, ikiwa ni pamoja na wimbo bora, albamu bora ya bendi na rapa bora iliyoenda kwa Khalidi Chokoraa
Bwana Misosi akishangilia tuzo ya wimbo bora wa Ragga aliyopewa na Sean Kingston






Mrisho Mpoto (shoto) aliondoka na tuzo ya wimbo bora wa asili na 'Mjomba'


Mzee Yusuf Alikomba tuzo za albamu bora ya taarab na ya mtunzi bora


Gadna G. Habash akipokea toka kwa Tajiri Mpoki tuzo ya mwanamuziki bora wa kike ya Lady JD aliyopokea kwa niaba ya mai waifu wake Jide


Khalidi Chokoraa akipokea tuzo ya Twanga pepeta wa Bendi bora


King Kikii akimkabidhi kwa Twanga Pepeta tuzo ya wimbo bora wa bendi


Lwiza Mbutu akisogea kutoa shukrani baada ya kupokea tuzo ya albamu bora ya bendi iliyoenda kwa Twanga Pepeta


Prodyuza bora wa mwaka akipokea tuzo


Diamond akisherehekea moja ya tuzo zake ikiwa ni pamoja na msanii bora anayechipukia, wimbo bora wa R& B toka kwa mwenyekiti wa Yanga Imani Madega







AY akisherehekea tuzo yake ya wimbo bora reggae


Lady JD akipozi na mai hazbendi wake na tuzo yake ya mwanamuziki bora wa kike


Marlaw akitamba na tuzo yake ya wimbo bora wa afro pop


Mwana FA na wenzake wakimtuza Diamond kwa kuwa msanii bora chipukizi

Hasheem Thabeet akimkabidhi C-Pwaaa tuzo ya video bora


Mwamvita Makamba na Ephraim Mafuru wakimkabidhi Banana Ally Zorro tuzo ya msanii bora wa kiume


Ras Inno Nganyagwa akimkabidhi AT tuzo ya wimbo bora wa kolabo aliofanya na Stara Thomas wa 'Nipigie'



























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2010

    Hebu niulize..hapo umesema huyo mume wa mtu alikua anapokea kwa niaba ya mke wake. Nilizania mkewew hakuwapo? Mbona namwona anapiga picha na mumewew siku hiyo hiyo...Nilizania ukiwa haupo ndio mtu mwingine anapoke akwa niaba yako lakini upo hapa kwenye sherehe halafu usipokee ni kama umeidharau hiyo zawadi...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2010

    Huyo MwanaFA si aliwaandikia barua kuwa hataki kujihusisha na Kili Music Award. Sasa anafanya nini tena humo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2010

    aaah nimefurahi saaaana mjomba mpoto kupata tuzo kweli ulikuwa unastahili kubebaaaa hongera mjombaaaaa nikipata nauli nitakuja kukupa hongera zako mjomba
    mdau canada

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2010

    Hivi Raggae na Ragga ni tofauti??maana mmenipoteza hapo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2010

    Mimi nadhani Jay Dee alimdharau huyo mpoki kutoa hiyo tuzo.Labda alitaka Sean Kingston ndiyo ampatie hiyo tuzo.Ushamba tu na majivuno ndio yanayomsumbua. Sijawahi kusikia mtu unakuwepo kwny event halfu kwa niaba anaenda kuchukua m2 mwingine tuzo labda kama ni mgongwa wa miguu!

    ReplyDelete
  6. Mume Wangu, mikanjuni TangaMay 15, 2010

    Jamani zawadi zote hizo ina maana Professor Jay hakuambulia chochote safari hii?? Au bado kuna washindi wengine hawajatangazwa?? Nawasihi mumpe angalau ile ya kushiriki mara nyingi au mwanamuziki mwenye wapenzi wengi hapo Bongo>

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 15, 2010

    jide mwanamuziki bora wa kike!?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2010

    Either of the two is true:

    Mpoki was snubbed by JD or Kili Award was snubb by JD.

    I presume it is Mpoki who got it. What's wrong with him? au wa vile anachekesha chekesha?

    ReplyDelete
  9. Mie nipo Hoii na kivazi cha Maunda, arafu yupo na mshua wake,.ebwana daaa ndo udhungu zaidi au?

    ReplyDelete
  10. NautiakasiMay 15, 2010

    Kwakweli sioni cha maana kwa miaka hii alichokifanya JIDE katika tasnia ya muziki, mpaka afikie kuwa mwanamuziki bora wa kike! I dont agree 100%, ni kubebana tu! Wako wadada wamechangamka sana kwa miaka hii, na wako na tungo bomba kama akina mwasiti,maundo zoro n.k! HII YA JIDE NI USHKAJI tu ndo maana aliona AIBU kujitokeza kwa jukwaa!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 15, 2010

    Mpaka TBL watakapojitoa na kuwa si wazungumzaji wa hii award ndo mizengwe itaisha. priority no 1 ya TBL ni kuuza bia, hivyo ikitokea conflict of interest ni wazi jibu liko wapi

    ReplyDelete
  12. kuntry boyMay 16, 2010

    HIZI AWARDS ZA KIFISADI.....
    WHERE IS MY FAVORITE ARTIST MATONYA.....hata kama sijakuona u still the winner homie....
    mississippi 4EVER!!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 16, 2010

    Wadau naombeni msaada wenu kwa yeyote anayejua. Nini maana ya kuweka vidole viwili(Chadema)juu wakati wa kupiga picha?Wakati mwingine kidole kimoja au vitatu mi nachanganyikiwa kabisa.

    Wanamaanisha au kuashiria nini?Ukiangalia picha hizo hapo juu utaelewa namaanisha nini.

    Naombeni msaada wenu

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 16, 2010

    Ankali we malizia tuuu apo kutoa tuzo zako na ze Fulanaz yako apo.....lakini tunaomba uje utuandikie maelezo ya kina kuhusu ze fulanazi tafadhali maaana watu tusha jitambishia sana kua tumeshinda ze fulanazi hahaaaa....Ankali ama lilikua changa la macho???si mchezo Ankali apo kweli naamnini Globu ya jamii inafanya kazi maana si rahisi kuona mutu anampa msanii tuzo apo Hongera sana
    mwisho mimi ni mwana libeneke ambae glob ya jamii ni kama maji kwangu kila dakika kazaa zisizo zidi tano au kumio nafungua globu ya jamii maana ata simu yangu home page yake ni ya Globu ya jamii
    aminia mzee wa Fulanazzzzzziii

    Mdau Nakadharika apa

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 16, 2010

    HAPO waliopata tuzo za halali ni mjomba na joe makini. wengine wote wizi mtuuuuupuuuuuuuu!!!!! JD keshachoka, AY hamna KITU. RUSHWA TU.
    mithupu usiibanie!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 16, 2010

    HOngereni Afrcan Stars Band wana WA KUTWANGA NA KUPEPETA KWA KUJIZOLEA TUZO TATU.
    HAKUNA UBISHI ALBUM YENU YA MWANA DAR ES SALAAM NI YA KIWANGO CHA JUU AMBAPO HAKUNA BENDI ILIYOWAKARIBIA KWA MWAKA HUU.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 16, 2010

    Lady JD siyo kwamba alimdharau MPOKE au KILI MUSIC AWARD. Ila aliindika mapema kwenda kuwahi contract performance yake ya kule ZOUNGH GARDEN anakopiga kila ijumaa. Mlitaka aharibu contract yake inayomuweka mjini?.Atakula kwenu?. Acheni hizo

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 16, 2010

    INO KUMBE UPO? MBONA KIMYA MSHIKAJIWANGU?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...