Habari yako Anklal, pole na majukumu.
Natoka muda huu kwenye ATM walau kuchukua vijisenti kwenye ATM ya NBC pale sayansi imenifurahisha kukutana na huu ujumbe kufuatia ATM Machine kuwa out of service na askari wa ulinzi kuweka angalizo kwa wateja kama inavyosomeka "TANGAZO MASHINE HII INAMEZA KADI BILA SUPU" hakika huu ni ufanisi mzuri kwa huyu askari maana angetumia nguvu nyingi kumuelekeza kila mteja aliyefika yeye kaweka bango lake kama linavyosomeka ivyo wewe huna la kuuliza zaidi ya kutafuta ATM
iliyo karibu
Mdau- Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2010

    hilarious

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2010

    huyo mlinzi ana akili km mchwa! nimecheka sana!asante mdau uliyewakilisha

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2010

    KIELELEZO TOSHA CHA HUDUMA MBOVU ZA NBC BENKI ISIYOJALI WATEJA WAKE!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2010

    safi sana

    ReplyDelete
  5. Hii ATM za NBC kenge , hata mimi juzi ATM kadi yangu imemezwa pale KICHWELE Branch japokuwa pale hakuna tangazo kama hilo... ni vizuri matangazo kama hayo yakawekwa ATM machine zote za NBC kutusaidia sisi wateja.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2010

    ujinga mtupu halafu watu wanashabikia,tanzania tanzania tanzania unakwenda wapi?watu wako wapumbavu sana mpaka wamepitiliza...nyinyi mnacheka mambo haya mkidhani mazuri hamjui taswira ya watu wengine majirani zenu wanaichukuliaje ni sawa na kupata jeraha ukaanza kucheka na kutokwenda hospital matokeo yake jeraha linakuwa kubwa na usishangae ukaambiwa ukatwe kabisa kiungo kwani tayari umeshaoza.kwa kweli mimi sioni cha kuchekesha hapo zaidi ya kunidhi tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2010

    Anno wa Fri May 21, 10:48:00 AM...
    Mbona Hasira! easy! Inachekesha!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2010

    Cha kuchekesha ni "creativity" ya mlinzi na cha kusikitisha ni huduma mbovu ya NBC. Kwa walio wengi watakubaliana na mimi kuwa katika benki zinazoongoza kukimbiwa na wananchi/wateja hii ni mojawapo. Tatizo ni lilelile -HUDUMA MBOVUUUUUUU!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2010

    Ugomvi wangu kwa nini uanzishe huduma then uwatie watu matatani?

    Mie nilishawahi kuliwa hela yangu pale kimara kituo cha mafuta atm post.

    Hela ilihesabu lakini haikutoka, but ikawa deducted kwenye akaunti. Nilijaribu kufuatilia nikapewa mlolongo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2010

    Hongera bwana afande kwa ubunifu wa hali ya juu,hii inanikumbusha kwamba waweza kutumia kidogo ulicho nacho kuleta mabadiliko makubwa katika jamii:UJUMBE UMESOMEKA! ingawaje na wasiwasi na ajira yako si unajua jinsi tulivyo!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2010

    Huyu mlinzi lazima atakuwa chapombe tu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2010

    sina jinsi ya kucomment huo mfano wa benki.maofisa utafikiri ni wa enzi za kugawa bidhaa-ujamaa style.hawaendi na wakati.CRDB JUU

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2010

    hahahaha safi sana anatakiwa aongezewe cheo huyo mlinzi wa atm hapo

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 22, 2010

    Nchi nyingine (hasa USA) siku hizi wanaepuka hilo tatizo la kumezwa kadi kwa kuweka mashine ambazo kadi haiingii yote, inakuwa imetokeza kwa nje au kuna zile ambazo unaweka kadi na kuitoa ndio unaweka PIN number yako. Nadhani wakiweka hizo tatizo litakwisha kabisa na kuwaondolea wateja usumbufu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...