Nilipanda basi ya Ngorika asubuhi ya saa 12 Kituo cha mabasi ubungo kuelekea Arusha. Lilikuwa ni Ngorika la pili , Kila mtu alitaka kuwahi kupanda gari hilo kwasababu ni kati ya yale yanayowahi zaidi kuondoa kituo cha ubungo kuelekea Arusha na Moshi kila siku.

asi lilipoanza kuondoka kutoka nje mtu Abiria mmoja akaingizwa kwenye gari na Mkata tiketi ambaye hakuwa mwajiriwa wa basi lile akapelekwa mpaka nyuma ya gari akapewa sehemu ya kukaa alilipa hela na kupewa tiketi akaambiwa ataletewa chenji yake .

Mara gari ikawa inaondoka kufika mataa likasimama Yule mkata tiketi akashuka akamwacha abiria wa watu na tiketi yake , simulizi ya mkata tiketi ikaishia hapo hapo basi likawa kimya na tayari kwa safari.

ufika Mbezi mkaguzi wa tiketi akaanza kupita kumfikia Yule mzee ,akaambiwa kilichotokea na ndio akaanza kudai chenji yake mkaguzi akamwabia sio yeye aliyempa tiketi hiyo kwahiyo hawezi kumshugulikia mara moja.

imi nilikuwa mbele kidogo ya abiria huyo nikamwambia apige namba ya simu iliyowekwa kwenye tiketi za basi hilo alivyopiga na kusema kisa chake tu wale jamaa wakamwabia hawahusiki awasiliane na walio kwenye basi hilo.

aada ya majibu hayo nikamwambia akifika kibaha ashuke na kwenda kulipoti kwa askari wa usalama barabarani na kweli tulipofika pale lakini kwanza akaongea na utingo , dereva pamoja na kondakta na Yule mkaguzi wao wa basi lakini majibu yao yalikuwa yale yale kukataa.
akati majibizano hayo yakiendelea mimi nilishuka kwenye gari na kuanza kuwapiga picha pamoja na kuchukuwa picha za basi hilo haswa namba za gari , wale utingo na konda kuona vile wakaja kunikaba nikaulizwa kwa nini napiga picha na kama ni mwandishi wa habari nionyeshe kitambulisho changu halafu wakaanza kunipeleka kituo cha polisi pale kibaha kwa kupiga picha tukio lile.

tukufika kituo cha polisi mbele kidogo tukakutana na askari mwingine akatusimamisha nikamweleza kilichotokea askari akaamuru nirudi ndani ya gari tuendelee na safari hapo hawakufanikiwa kuchukuwa kamera yangu wala kuniumiza nilijitahidi kuzuia jitihada zote za wao kufanya jaribio hilo.

afari ikaendelea kufika mbele kidogo wakataka tena nifute picha au waje kuchukuwa kamera hiyo na kuivunja huku abiria wengi ndani ya basi wakinipigia kelele niache ubishi nifute picha na kuwaonyesha kweli nimefuta picha halafu niende mbele kuwaonyesha konda na dereva kwamba kweli nimefuta.

ikufanya hivyo badala yake nilibadilisha memory card ile niliyopiga hizo picha na kuweka nyingine ambayo ilikuwa tupu na kumpa jirani yangu kwenye basi ashike , tulipifika chalinze wakasimamisha gari na mmoja akashuka kwenda kutoa cha polisi chalinze kutoa taarifa kwa kile nilichofanya.

wingine akawa ndani ya gari akatishia kuniadhibu nakumbuka alirusha ngumi kama 3 hivi lakini nilimkwepa na kuendelea na msimamo wangu sitoi kamera kwao wala picha sifuti waende polisi kama walivyoahidi. Tulibishana kwa dakika kama 15 ndani ya basi mpaka polisi alivyokuja kunichukuwa ndani ya basi na kamera yangu kufika kule nikapekuliwa nikavuliwa viatu na mkanda wa suruani kisha nikapewa amri ya kukaa chini huku wakisikiliza maelezo ya Yule jamaa wa basi.

alivyomaliza kusikiliza maelezo yao nikaulizwa kwanini nilifanya vile nikawaambia tu nimeamua kuchukuwa picha zile kutokana na tukio lilitokea na nina haki zote za kupiga picha au kuchukuwa picha za tukio lolote kama raia kamili wa watanzania.

ikaendelea kuwaambia Tunatakiwa kuweka kumbukumbu ya vitu vinavyoendelea njiani kwa ajili yao polisi kama chochote kitatokea kama hivyo na mambo mengine mengine mengi ya kiusalama ile ilikuwa ni kumbukumbu tu nikaomba waniambie kama kuweka kumbukumbu ni kosa .

Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nikaombwa niwape kamera askari waangalie kamera yangu kama kweli picha zilikwepo nikawapa walipoangalia hawakukuta picha yoyote wala chochote , nikatoa vitu vyote nilivyokuwa navyo mfukoni hawakukuta chochote. Nikaambiwa niende kwenye gari na siku nyingine likitokea tukio kama hilo niwasiliane nao moja kwa moja nisianzie malumbano kwenye vyombo vya usafiri nikarudi kwenye gari kuendelea na safari .
Kuanzia hapo basi letu likawa linakaguliwa kwa kuingiliwa na polisi wa usalama barabarani kila linapofika kituoni na kuuliza maswali abiria kama kuna tatizo lolote limetokea.

ilikuwa fundisho Sikuhiyo nilivyorudi kwenye gari kila mtu alinishukuru kwa uamuzi niliouchukuwa na likawa funzo kwa dereva na konda wa basi lile kwasababu njiani kote walikuwa na heshima.

Vizuri abiria wajifunze kutetea haki zao na za wengine endapo wataona zinachezewa kwa makusudi , kama ukizarau siku itamkuta mtoto wako au hata ndugu yako akakosa mambo ya muhimu kwenye maisha yake na kazi zake zingine.
Mdau Yona Fares Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    sasa yona kama ulifanikiwa kuficha hizo picha za tukio kwanini hujatuwekea tukaona ama ni majungu tu unatuletea humu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2010

    na je mwenye chnge yake aliipta au ni all that for nothing?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2010

    Yona, tuoneshe hizo picha na utuambie hatua ifuatayo utakayoichukua.

    Mimi na abiria wenzangu tulikumbwa na ushenzi zaidi ya huo kutoka kwa wafanyakazi wa Tawfiq. Polisi wa sehemu fulani wakatunong'oneza kuwa kama vipi tuwape kichapo cha raia, jamaa wakashtuka na kutia adabu. Ila tulikuwa tumeshapanga timu ya kuanzisha kichapo cha haja. Wasingepona maana walikuwa wameshatukera kupita maelezo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2010

    leta picha na namba za gariii

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2010

    Yona Maro hongera kwa kuendeleza 'kipaji' chako.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2010

    yona ulichofanya ni kitu cha busara mno mana ni watu wachache sana ambao wanaweza kutetea haki zao na za wensao mana wabongo wengi tunaogopa hasa likifika swala la polisi ndo tunaona km vile tunaenda kuuliwa kumbe ni polisi ni binadam tuu km mtu mwingine kudai haki ni wajibu wa kila mtu. Ila sasa Yona mi umeniacha njia panda vipi huyo mzee alirudishiwa iyo change au laa? Na km alirudishiwa alirudishiwa baada au kabla ya ishu kuripotiwa kwa polisi na kama hakurudishiwa ni je hatua zipi zimechukuliwa? Km utaweza kutuma picha ya hilo tukio inakuwa visuri saidi walimwengu nao wajioneee

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    Wapi picha?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    Hujui hata kufupisha story,maelezo mareefuuu!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    mdau yona, pole kwa mkasa uliokukuta! hata hivyo hujatuelewesha km jitihada zako ziliwezesha yule abiria mwingine kurudishiwa chenji zake
    au la! maana mkasa wote huo kisa ilikuwa ni chenji!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2010

    Actually I cant imagine how illegaly you did the taking photoes whilst you not leagaly proven liable in the field. Ujinga una ngazi tofautitofauti(unazidiana) You were not to benefit anything even if the contract was for your benefit. You deserve to be SUED even though the act was for the beneficiary of the debting passenger that led for the best of the mass. I wish I could be the conductor as all the passangers were to face charges for the offends upon u before I could face mine from the Passanger to who was suffered the los. WATANZANIA MSIFATE MKUMBO. Mbele ya haki ni mmoja mmoja ndo huwajibishwa. Mathalani huyu Yona alivyostahili kuwajibishwa. Kuwa mtanzania sio ndo kuwa ju ya sheria. Ulichotakiwa ni kumsimamia abiria na si kumponza na kupata kesi ya pili Nk.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2010

    Huyu jamaa aliyeandika maoni siku na muda "Mon Jun 14, 08:54:00 AM", ni mjinga kupita kasi. English mbovu, Kiswahili kibovu na maoni yake hayana maana. Ni afadhali asichangie hoja humu ndani. Wadau hebu semeni ni nini alikuwa anataka kutuambia????

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2010

    Hongera ingawa juhudi zako hazijazaa matunda tangible zaidi ya kuwafundisha ujasiri hao abiria wenzako.

    Wabongo wengi tu waoga sana kutetea haki zetu. Siku moja niliwahi gombana na abiria wa coaster kisa nimekatalia konda kuruhusu abiria 2 tukae mahali anapopaswa kukaa abiria mmoja. Konda akawaambia abiria wenginean kua mimi ndo nilikua nawachelewesha kwani haondoi gari hadi nimpishe mtu akae nami. Abiria wote wakanigeuka, kunilazimisha nikubaliane na konda

    www.kapongola.wordpress.com

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 14, 2010

    Tarehe Mon Jun 14, 08:54:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Huyu jamaa ni mpuuzi inatakiwa kujua Nyerere, Kwame, Ben Bella, Kenyata hawakupigania uhuru wao walitetea haki za wanyonge, Weldone Yona Keep it up achana na hawa vibaraka wanaojifanya kukukosoa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 14, 2010

    Nafikiri kuna watu wengine unashindwa kuwatafutia jina au tusi linalofaa kama mdau wa hapo 14:08:54! Wewe hata kama umesoma sheria basi ulikuwa unaibia tu wala hakuna chochote! Wala uelewi unachokifanya au unachoongea. Nafikiri unatakiwa ukapimwe kwanza kwani inwezekana kuna screw katika kichwa chako imelegea! What kind of sheria you are trying to teach us?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2010

    anon wa Mon Jun 14, 08:54:00 AM kwanza kajifundishe english au mara nyengine andika kwa kiswahili. Pili i hope wewe si mwanasheri otherwise god help us, ikiwa wanasheria wetu tanzania ni kama wewe.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2010

    Kwanini uwapige watu picha bila ridhaa yao??!! Ndio ukome siku nyingine. Raia wanayo haki ya kutopigwa picha kama wamekataa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 14, 2010

    http://www.youtube.com/watch?v=rB8BdRNVnEI&feature=player_embedded#!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 14, 2010

    http://www.youtube.com/watch?v=rB8BdRNVnEI&feature=player_embedded#!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 14, 2010

    Huyo Anony wa Mon Jun 14, 08:54:00 AM atafute mtoto yeyote wa chekechea amfundishe Kiingereza. Alichoandika hapo juu ni kituko cha mwaka. Jamaa hajui Kiingereza hata cha kuombea maji.

    ReplyDelete
  20. Baba UbayaJune 14, 2010

    hahaha..huyo mdau aliyemwaga UNG'ENG'E nadhani alikuwa anataipu huku anamwangalia mwenzie akila ukwaju ama embe mbichi(yenye ile pilipili nyekundu pa1 na chumvi).domo lilikuwa linatoka UDENDA muda wote.
    next time just read some posts and shut up!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 14, 2010

    8:54 kwanza anza na kidhungu halafu umalizie na law. Hakuna sheira inayomkataza mtu kuchukua picha kama sehemu ni public. Na haina tangazo lolote linalozuia kuchukua picha. Wenzako sikuhizi hapa wale wanaume wanaojishika shika kwenye subway wanakomeshwa si wangesema sio halali kuchukua picha... kama sehemu ni ppublic you can do aythingyou want to do as long you don't touch anybody.

    kama nchi haiwi update na sheria kutokana na technologia inavyokwenda let people do what they think it is right...

    Mimi naona kila siku sijui wanasemina wa kutunga seheria sijui wanakua wanatunga au kuzirekebisaha sheria kwenda na wakati...

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 15, 2010

    Inachekesha lakini pia inasikitisha sana kuona watu wengiii mmeondoka kwenye mada na kuanza kuongelea kiingereza cha huyo jamaa wa hilo basi, yaani amefanikiwa kumzima Yona kabisaaa! STAY FOCUSED, FOOLS!!!!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 15, 2010

    "......you did the taking photoes whilst you not leagaly proven liable in the field...." Mimi ni mwanasheria lakini huyu mtu anon. Mon Jun 14, 08:54:00 AM kwa asilimia mia si mwansheria, anashindwa hata kuandika neno 'legally' ambalo ndilo msingi wa jina taaluma. Napenda kumshauri kutovamia fani za watu, pia kama alipitapita kimakosa mpaka akakwaa digrii basi aombe kibali cha kurudia ili wampike vizuri mpaka aive.
    Kuhusu upigaji wa picha si kosa labda kama unaipiga ukiwa na nia ya kuisambaza ili kuharibu jina la mhusika,na kosa litakuja bada ya kuisambaza, lakini kwa ishu hii ya kutaka kufichua maovu sioni kama kulikuwa na haja ya kumsumbua mpigaji picha.


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...